Mdahalo wa UDA Live on Star TV: Updates

Swali: manunuzi ya hisa umelipia kodi Jibu: yamelipiwa
Swali: Idd Simba anasema pesa ulizolipa na consultation fee Jibu: Swali ni la Idd Simba sio langu
Swali: Umeshiriki baada ya kuongea na wanasheria wako kwamba benki isilipwe huoni kwamba wewe ni muhalifu Jibu: Sio wajibu wetu sisi
Huyo Iddi Simba ni mshauri kweli na hizo pesa alizolipwa kodi imelipwa? au mdio Taperi wa Saigon

Na kukwepa kulipa benki nadhani ni uhalifu hana la kijutetea

Kisena ni Mjanja Mno,
Katumia ile trick ya kutafuta sympathy kwa wamatumbi wenzie, kwamba yeye ni mwekezaji wa kizalendo na wapo watu wanampinga hivyo wanawatumia wananchi kumdhoofisha na alipotaja muhindi (Manji) ndio kamaliza kabisa

Kuna Maswali mengi ambayo bado yanaleta kizunguzungu, mpaka sasa sijaona jibu la kueleweka ni kwa nini pesa ziende kwenye Account binafsi? japo anazungumzia barua inavyodai alkini kuna walakini

Hilo swali la kushindanishwa na wengine pia bado halina majibu ya kuridhisha

kwa kweli huo ndio mwanzo hasa wa issue nzima

Mkuu tuko pamoja. Tukiangilia hii issue ya UDA kwa 'usisi' against 'wao' tutakuwa tunajidanganya vibaya mno. Kisena is the original conman na anachokifanya ni kutuchezea akili watanzania kwa hiki anachokiita 'mtanzania mwenzetu'. Mwenzetu kivipi? Kwa kupindisha sheria? Linapokuja swala la ufisadi I dont care kama mtu ni mchina, msukuma, mnyamwezi, muhindi, mrusi or whatever. Fisadi ni fisadi tu. Hata kama mmatumbi atajichubua kama Michael Jackson na kuwa mweupe kama ni fisadi atabakia fisadi tu.

Kisena ana maswali ya msingi ya kujibu bahati yake leo kapata muulizaji mlaini. Kwa mfano.
1. Ni lini alianza mchakato wa kununua hisa za UDA?
2. Alisikia wapi na kwa nani kuwa hisa za UDA zinauzwa?
3. Nani ni wamiliki wa Simon Group (past and present)
4. Uhusiano wake yeye kibiashara ni Mzee Idd Simba umeanzia kwenye hii issue ya UDA? kama hapana, ulianzia kwenye biashara gani?
6. Cheque iliyolipwa kwenye account ya Mzee Idd Simba imeandikwa transportation charges - ali-transport nini? ana evidence ya hivyo vilivyosafirishwa?
7. Kwa nini amefungua kesi mahakamani kuhusiana na malipo kwenye account ya Mzee Simba?
8. Alishawahi kuongea na Ridhwani Kikwete au waziri, naibu waziri, katibu wa wizara yeyote kuhusu ununuzi wa hisa za UDA? lini na waliongea nini? na waliafikiana nini?
9. Ana uwezo wa kuendesha UDA (nasisitiza - uwezo sio MKAKATI). atoe ushahidi wa uwezo huo - bank records, assets, kampuni anazomiliki
10. Kuna kampuni yake yoyote ilifadika na stimulus package? (hili swali ajibu under oath)
11. Simon Group ina experience gani kwenye sector ya CITY TRANSPORTATION?

Narudia, madai ya 'mimi mtanazania mwenzenu' ni kutufanya sisi majuha. Hii nchi haiongozwi na wachina au wazungu. Inaongozwa na hawa hawa 'watanzania wenzetu' Ni hawa hawa wanaojiita watanzania wenzetu ndio wametufikisha hapa. Ni hawa hawa wametengeneza mikataba mibovu ya madini. Ni hawa hawa wametuweka kwenye giza na kusababisha mgomo wa wauza mafuta.

Na kwa nini jiji lisiendeshe UDA? why? Kama Kisena anajiona ana akili za ziada za kuendesha UDA kwa nini asitoe consultancy kwa jiji kwenye uendeshaji wa UDA? UDA imefikia hapo ilipo kwa sababu 'watanzania wenzetu' wamekusudia ifike hapo ili hawa watanzania wenzetu wengine waindeshe kwa maslahi binafsi.

Napinga kwa nguvu zote UDA kuendeshwa na kampuni binafsi. JIJI liendeshe na kwa viongozi wa jijo hawawezi WATIMULIWE like Yesterday.

Jamaa anamiliki mabilioni alafu haoni tatizo kuyataja ujue huyo anajua anachofanya,kiukweli nimewashangaa sana wanahabari kwa maswali ya kijinga kiasi kile yaan wanauliza maswali ambayo hawajayafania research wala nn full kukurupuka

Swali zuri, ambalo ungekua wewe ungeuliza ni lipi? tupe hayo maswali angalau tusaidiane kutafakari

Swali: manunuzi ya hisa umelipia kodi Jibu: yamelipiwa

Swali: Idd Simba anasema pesa ulizolipa na consultation fee Jibu: Swali ni la Idd Simba sio langu

Swali: Umeshiriki baada ya kuongea na wanasheria wako kwamba benki isilipwe huoni kwamba wewe ni muhalifu Jibu: Sio wajibu wetu sisi

swali la kukubali maelekezo kufanikisha benki isilipwe lilionyesha kumshtua mkurugenzi wa simon group

Nipo hapa naona mafundi mitambo wanafunga mitambo mpaka wamevua mashati yao! Ingawa mimi simtaalamu wa mitambo maeneo waliyofungia hili dish lao hapa Moven Pick msishangae mitambo kukatikakatika!!

Mkuu kwa bahati nzuri quality ya matangazo imekuwa nzuri sana

Ndugu zangu mbona mnashangaa sana kwa hizo hekari 12 kulipiwa kodi ya milioni 10 for more than 10 years. Mmewahi kulitafakari la Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) unahekari ngapi lakini serikali inalipwa US $ 1000 kwa mwaka na mtu anayejiita mwekezaji aliyesema angejenga hotels, etc lakini pakavu hadi leo?

Sihalalishi aina yeyote ya ubadhirifu/utapeli na ukwapuaji kwa kuliandika hilo la hapo juu.

Ndugu zangu mbona mnashangaa sana kwa hizo hekari 12 kulipiwa kodi ya milioni 10 for more than 10 years. Mmewahi kulitafakari la Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) unahekari ngapi lakini serikali inalipwa US $ 1000 kwa mwaka na mtu anayejiita mwekezaji aliyesema angejenga hotels, etc lakini pakavu hadi leo?

Sihalalishi aina yeyote ya ubadhirifu/utapeli na ukwapuaji kwa kuliandika hilo la hapo juu.

eti wamesema alishawahi kuua mradi wa Mabasi ya Wanafunzi Dar miaka ile? Duh! Na huyu kisena mabasi ya Wanafunzi yaliyotolewa na CRDB Yatakuwa chini yake pia? maana hayo mabasi yana thamani kuzidi pesa alizoinunua Uda!

napenda taifa langu lisipoteze fedha kwenye makampuni ya simu na madini baada ya hapo basi tupate mengine kama UDA

kwa faida ya wahindi siyo?

kumbe jamaa alivosema tunakwamishana wenyewe alikuwa ana hoja.

heri mtanzania amiliki kampeni kitapeli kuliko Mhindi kumiliki kampuni kihalali.

That is my verdict

Mkuu are you serious...!!! ???, kweli tunakwamishana wenyewe......
Hivi wewe shida yako ni kuona kampuni inafanya kazi kwa manufaa ya watanzania au ni kuona mzaliendo anamiliki kampuni hata kama inakufa ?
Alafu hii notion ya kwamba Muhindi sio mtanzania imetoka wapi?
Na hapa issue sio kumpa kampuni muhindi kwa sasa ni kampuni ibaki kwa wananchi na sio kupeana kimagumashi.

Jamaa wa Simon Group wako njema sana, nimewakubali. Amejieleza vizuri wale wasiomuelewa waanze upya kufungua bongo zao.

Back
Top Bottom