Mdahalo wa UDA Live on Star TV: Updates

Mkuu are you serious...!!! ???, kweli tunakwamishana wenyewe......
Hivi wewe shida yako ni kuona kampuni inafanya kazi kwa manufaa ya watanzania au ni kuona mzaliendo anamiliki kampuni hata kama inakufa ?
Alafu hii notion ya kwamba Muhindi sio mtanzania imetoka wapi?
Na hapa issue sio kumpa kampuni muhindi kwa sasa ni kampuni ibaki kwa wananchi na sio kupeana kimagumashi.

Much thanks kwa kusimamia Show kwa kiwango cha juu. Mwenye macho kasoma

ALUTA CONTINUA
 
Wanamazingaombwe wote duniani wanafanana. Wanauwezo wa kuwaaminisha watazamaji kitu kisichokuwepo kwamba kipo na kile kilichopo kwamba hakipo. Mwisho wa show watazamaji hubakia impressed! Siri kuu ya wanamichezi hao iko kwenye matumizi ya maneno na wepesi wa vidole.

Hoja za Msingi zinajibiwa kwa ufafanuzi mwepesi saaana, watu wana tuhuma nzito anakwambia aaah mbona haka ni kajishamba hujaona mashamba wewe. Huu mchezo hatari sana.

I wish Star TV waibebe mada hii katika mjadala Mkali wa Tuongee Asubuhi na JF ipate nafasi ya maoni ya Washiriki kusomwa. Wakiyasikia haya watatambua mchezo wao mchafu ushapata tiba yake.
 
Mkuu are you serious...!!! ???, kweli tunakwamishana wenyewe......
Hivi wewe shida yako ni kuona kampuni inafanya kazi kwa manufaa ya watanzania au ni kuona mzaliendo anamiliki kampuni hata kama inakufa ?
Alafu hii notion ya kwamba Muhindi sio mtanzania imetoka wapi?
Na hapa issue sio kumpa kampuni muhindi kwa sasa ni kampuni ibaki kwa wananchi na sio kupeana kimagumashi.

Muhindi != Mtanzania.

ndiyo. hata mie siungi mkono kupeana kampuni kimagumashi. kama kuna taratibu zilikiukwa, heri basi Simon Group na wadau wengine warudi mezani waweke mambo sawa ili wananchi tujiridhishe kwamba Simon Group tumemkabidhi kampuni yetu na tuone kile anachotarajia kutupatia hapo baadaye.

kusema tu kampuni irudi kwa wananchi ni too general. Watanzania tuna utaratibu wa kula bila kuendeleza. ndiyo maana leo uda ina mabasi mawili. kama itarudishwa kwa wananchi kwa mtindo wa kutokufafanua hao wananchi ni kina nani utajikuta uda haina basi hata moja na huna mtu wa kumuwajibisha.
 
Back
Top Bottom