Mdahalo uliondaliwa na TAHLSO wa Kujadili hotuba ya rais Star TV

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,034
144,387
Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Nchini(TAHLISO), leo wameandaa Mdahalo utakaofanyika katika Ukumbi wa Nkruma wa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kujadili Hotuba ya Raisi aliyeito Bungeni hivi karibuni.

Mdahalo huo umepangwa kuanza saa 7:30 mchana mpaka saa 11:00 jioni ya leo na utarushwa live na Star tv pamoja na TBC1.

Wazungumzaji wakuu watakuwa ni Prof.Ngowi wa Mzumbe ambae ni Prof.wa uchumi, Dr.John Jingu wa UD na mzungumzaji mwingine atakuwa ni Mwanadiplomasia Balozi Christopher Liundi. Mdahalo huo utaongozwa na Dr. Ayoub Rioba wa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam.

Chanzo: Star tv

Mkutano huu nikiuangalia sitaki kabisa kuamini kuwa umeandaliwa na TAHLSO bali nahisi vinginevyo.

Update:
Mdahalo utaanza saa 8:30 mchana huu
 
Kama ni tbc na star tv nazani unajua utakuwaje...
Ila nasikitika Dr Ryoba mtu makini kuongoza mdahalo wa aina hii
 
hao wazungumzaji ni wanafunzi, au ni maprofesa kama jk na jpm
 
Badala ya kuujadili umafia wa NEC wanakalia mijadala hewa yenye lengo la kujipendekeza zaidi kulikoni kuangalia na kuzitafutia muarobaini kero za kuongozwa na viongozi ambao pengine hatukuwachagua.
 
Badala ya kuujadili umafia wa NEC wanakalia mijadala hewa yenye lengo la kujipendekeza zaidi kulikoni kuangalia na kuzitafutia muarobaini kero za kuongozwa na viongozi ambao pengine hatukuwachagua.

Leo watakuwa na kazi moja tu nayo ni kupamba hotuba ya mh.
 
Siwezi kupoteza muda wangu kuangalia mdahalo wa kijinga ulioandaliwa na watu na vituo vile vile vya utangazaji tunavyovifahamu mrengo wake. TBC na STAR TV si vyombo vigeni na hakuna asiyejua kuwa wapo biased.
Walioandaa na mawakala wao wakawasikilize na wanaofanana na wao kifikra.
 
Vipi Diallo ajapewa shavu na na taasisi si alipamba sana wakati wa kampeni kupitia media yake make wizara zimebaki chache!
 
Nilifikiri wazungumzaji wakuu na wengineo wawe members wa TAHLSO sasa naona imekaa kama UDASA vile!

Hapana UDASA haijahusika hata kidogo na members wa UDASA wametumiwa tu mwaliko kama watu wengine. Ukumbi wa Nkurumah unakodishwa kwa mtu au Taasisi yoyote ili mradi kusiwe na shughuli inayofanyika hapo kwa siku husika. Kama walivyosema wengine ni kwamba huo mdahalo kuna watu kwenye system wako nyuma yake na si UDASA.
 
Badala ya kuujadili umafia wa NEC wanakalia mijadala hewa yenye lengo la kujipendekeza zaidi kulikoni kuangalia na kuzitafutia muarobaini kero za kuongozwa na viongozi ambao pengine hatukuwachagua.[/QUOTE

Naomba usiwasemee watu walio wengi sema kama wewe hukuwachagua maana sie tunaojitambua na ndiyo wengi nikiwemo Mimi niliwachagua na nina imani nao
 
Matapeli hawa wanatafuta sehemu ya matumizi..hizo pesa wapeleke kuchangia wale wanaotengeneza bara bara ya mwenge moro oco
 
Andaeni basi na nyinyi wa kwenu tuone tofauti na hao mnaowaponda.Maanake kila kitu ni kulalamika tu kama watoto wa kambo.
 
Kuanzia Ayoub Ryoba mpk hao wazungumzaji wakuu wote waganga njaa. Wanatafuta kick ya kuteuliwa kama Dr. Possy ktk nafasi ama za uwaziri zilizobakia ama nyinginezo.
Halafu Ayoub Ryoba hanaga point ana kariri kariri tu. Doctorate za kibongo ni za kupaste na kukariri maandiko ya watu.
 
hapo tegemea sifa tu,wala kulikuwa hakuna aja ya kuita kuijadili ilitakiwa uitwe mjadala wa kusifia hutuba ya Makufuli kama unabisha subiri ujisikilizie mwenyewe
 
Watu wa hovyo sana humu...wivu na chuki vitawaandama sana.
Kwahyo mnachukia hotuba ya rais?
TBC na Star tv wamekubali kurusha bure...ile tv yenu imepotezea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom