Swali la great thinkers linajibiwa na light thinkers ..lost urgument
Ahadi za lowasa zinatekelezeka hata kwa short-run, viwanda vya magufuli inakuwa ngumu make nishati za kuendesha mitambo ya viwanda haipo, kama nishati ya kumulikia taa za nyumbani hivyo viwanda vitakula loss ya hatari kwa huu mgao wa umeme.
Hatutaki maneno, tumeyachoka, kila siku maneno, maneno. Mi kura yangu nampa mwenye sura nzuri kuliko mwenzie, ndo uamuzi mgumu kabisa katika maisha yangu, hutaki kajinyonge.
#sifa yangu kubwa kwa mgombea uraisi wa JMTZ sura nzuri, vigezo na masharti kuzingatiwa.
mungu atusaidie tupate iyo elimu ILI TUWEZE KULA KWA KALAMU ninavyojuwa wa Tanzania wakipata elimu safi mama yangu wa NIGERIA WATAKUWA WATOTO WA WATANZANIA MAANA KUNA BAADHI YA WA TANZANIA WANAELIMU NDOGO ILA NI HATARI
Lowassa kipao mbele chake namba moja Elimu, namba mbili Elimu na namba tatu elimu.
Magufuli yeye kipao mbele chake Viwanda, Viwanda Tanzania nzima.
Wote hao juu wanaomba kazi kwetu, sisi ndio mabosi wao. Wametuambia watatufanyia hayo tukiwapa ridhaa ya kutuongoza.
Sasa tujadili yupi kati ya hao atakaye weza kutuvusha. Je Elimu itawezekana? Viwanda vitawezekana?
Nondo zenu zitasaidia sana kutushawishi sisi ambao bado atujaamua tumpigie kura nani.
Karibuni kwa mjadala wa maslai mapana ya Tanzania yetu. Mungu ibariki Tanzania, Ibariki Africa
Afadhali mwenye elimu kwa sabab hyo hyo elimu itatusaidia kuongeza wataalamu wa kuviendesha hvyo vwanda 2. Tukifanya vwanda 2taishia kuajiri 2 wataalamu kutoka nje kama ilivyo uwanja wa taifa na c ndan ya nchi na watanzania watakuwa kama ma day worker 2
Mchango wangu....Elimu Kwanza. Wasomi watakaopatikana wataanzisha hivyo viwanda. Serikali iandae tu mazingira mazuri ya uwekezaji wa ndani.
Afadhali mwenye elimu kwa sabab hyo hyo elimu itatusaidia kuongeza wataalamu wa kuviendesha hvyo vwanda 2. Tukifanya vwanda 2taishia kuajiri 2 wataalamu kutoka nje kama ilivyo uwanja wa taifa na c ndan ya nchi na watanzania watakuwa kama ma day worker 2
SERA YA MAGUFULI YA VIWANDA INA KASORO KUBWA SANA, NA KAMWE HAIWEZI KUTEKELEZEKA KWA SABABU.
1/Magufuli anasema serikali yake itajenga viwanda vingi.
Hii kitu haiwezekani kabisa kwa kuwa Sera na mfumo wa sasa wa dunia na nchini kwetu ni soko huria na serikali haiwajibiki kufanya biashara. Serikali kazi yake ni Kutunga sera kutoa huduma, kusimamia sheria, kukusanya kodi. Ujenzi Wa viwanda ni suala la kibiashara kabisa.
2/Magufuli anasema atafufua viwanda vingi vilivyokufa.
Hili nalo ni la kisiasa kabisa. Viwanda vingi vimekufa na kuzikwa kabisa(Hata Magofu hayapo tena), vipo vilivyokufa kwa sababu za kiuchumi(soko la bidhaa) vingine vimekufa kwa sababu ya ushindani wa kibiashara, vingine vimekufa kwa sababu ya technolojia ya kizamani, Uhaba wa malighafi, management mbovu nk. Sasa unafufua kipi na unaacha kipi?
3/Magufuli anasema atavirudisha viwanda vyote vilivyobinafsishwa na vikashindwa kuendelezwa. Hii nayo haiwezekani(kwa sababu wamiliki walivinunua kihalali hivyo kuvirudisha serikalini inabidi upatane nao na sio kuvipora) na kama ikiwezekana itakuwa ni hasara kubwa sana kwa serikali(kwa sababu vingi havina chochote kile cha kuzalisha, vina madeni balaa, ni magofu matupu)
4/Magufuli anasema atajengwa uchumi wa Viwanda. Hii nayo haiwezekani kabisa. Uchumi Wa viwanda ni matokeo ya kufanya mambo mengine ya kiuchumi na Sio kujenga viwanda vingi. Kujenga viwanda ni jambo moja tena rahisi, lakini kuviendesha viwanda ni jambo lingine tena gumu sana. Kuna mambo kadhaa yanafaa kwanza kufanyika kwanza kiuchumi ili kuzaa uchumi Wa viwanda. Kwa mfano Nishati ya Uhakika na nafuu, SOKO la uhakika na pana, TECHNOLOGIA ya Uhakika na kisiasa, WATAALAMU bora na wakutosha, KODI zikusanywe kwa uhakika kwa bidhaa zinazoingizws nchini ili kulinda viwanda vya ndani, MALIGHAFI nyingi na ya uhakika nk.
Elimu kwanza. viwanda baadae.bila elimu hivyo viwanda utaviendeshaje pia tuacheni ushabiki lowassa.niyo anafaa kuingia ikulu.