Mchungaji vs Mwalimu wa Kwaya

Red Scorpion

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,736
4,252
NDANI YA KANISA:

MCHUNGAJI: Ningekuwa na uwezo ningechukua Guiness zote na kuzimwaga mtoni!"
Waamini wakajibu Ameen!

MCHUNGAJI: Ningechukua Safari zote na kuzimwaga mtoni!
WAAMINI: Ameen!

MCHUNGAJI: Ningechukua Konyagi zote na kuzimwaga mtoni!
WAAMINI: Ameen!

MCHUNGAJI: Ningechukua Banana zote na kuzimwaga mtoni!
WAAMINI: Ameen!

MCHUNGAJI: Ningechukua Whisky zote na kuzimwaga mtoni!
WAAMINI: Ameen!

Baada ya MCHUNGAJI kumaliza mahubiri, mara Mwalimu wa Kwaya akasimama na kuwaambia Waamini, "Fungueni vitabu vyenu tuimbe wimbo namba 152 usemao NASI TUTAKUNYWA MAJI YA MTO HUO!"

Waamini wakashangilia: HALELUYAAA!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom