Mchungaji Mwanasiasa aliyeambulia patupu

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Haya ndiyo maneno aliyobwabwaja huyu mchungaji mwaka 2005, aliutamani ufalme wa siasa na kuambulia patupu
TV ya INJILI Kwenye Internet -
WWW.GOSPELGTV.COM
Tel. 254722602445 E-mail: munishi@munishi.com or info@munishi.comKikwete siyo Wetu

Wakati Waislamu wameanza kumshuku Kikwete, Wakristo nao wanasema kikwete
siyo wao. Magazeti yenye misimamo mikali ya Kiislamu yamemtaka Jakaya
Mrisho Kikwete atangaze msimamo. Ama aachane na Uislamu abatizwe awe
Mkristo, au abaki Mwislamu. Walihoji kwamba kikwete hawezi kuwa na dini
zote mbili. Yaani hawezi kuwa Mwislamu Mkristo. Nao Wakristo kwa upande
ule mwingine wanashindwa kabisa kumwamini Kikwete kwani wanajua wazi
kwamba yeye ni Mwislamu.

Kwa Lugha inayoeleweka, Waislamu wanapomuona Kikwete na maaskofu,
wanahisi kwamba huko amepewa nyama ya nguruwe awaletee msikitini. Nao
Wakristo wanapomuona Kikwete kanisani kabla ya kubatizwa na kuukana
Uislamu, Wanaona kama ametumwa na wenzao walete majini kanisani. Tayari
Bwana Kikwete ana kibarua kigumu kuhusu imani yake kwa Mungu. Urais
anautaka na Uislamu bado anaupenda. Ujanja wa wanasiasa kuwatapeli watu
wa dini unafikia mwisho. Nyerere alifanikiwa kuwadanganya Watanzania
kwamba CCM na serikali yake havina dini, Lakini baada ya Mkapa Mkristo
kuwaua Waislamu Zanzibar, Watanzania wamejua kumbe serikali na CCM zina
dini. Wanapotafuta mpaka wa dini na siasa wanakosa. Kwani wenye dini
ndio wapiga kura. Tena kwa CCM kumteua Kikwete Mwislamu baada ya Mkapa
Mkristo aliyekuja baada ya Mwinyi Mwislamu, Aliyechaguliwa na Nyerere
Mkristo, sasa ni wazi kwamba dini mbili ndizo zinazopokezana uongozi
Tanzania. Waumini wa dini nyingine wanaona wananyimwa haki na dini mbili
ambazo zimeitawala
Tanzania tangu tupate kile walichokiita UHURU. Kwa wale wasio na dini
pamoja dini nyingine ambazo siyo Wakristo wala Waislamu, wakati sasa
umefika nao wapewe nafasi ya kuiongoza Tanzania. Imegunduliwa kwamba
Lugha ya Serikali haina dini ilitumiwa kuwapumbaza Watanzania kumbe
kinachotawala ni DINI. Mbona baada ya Nyerere Mkristo alifuata Mwinyi
Mwiislamu? Tena mbona baada ya Mwinyi Mwiislamu alifuatiwa na Mkapa
Mkristo? Au tuseme yote ni bahati mbaya kwamba baada ya Mkapa, CCM
wameona vyema wamteue Mwislamu Kikwete? Kama tutalazimishiwa Kikwete
basi duara la Waislamu na Wakristo kuitawala Tanzania sijui litaishia
wapi.Tunashangazwa na ukimya wa dini zilizoachwa nje ya uongozi huku
wakidanganywa kwamba "Serikali haina DINI. Suluhu ni KATIBA iwaruhusu
wagombea binafsi ili kila dini iteue mgombea wake. Magazeti ya kiislamu
yana haki ya kujua kama kweli Kikwete wa CCM ni Mwislamu mwenzao.
Badala ya magazeti ya Kikristo kuhoji kama Kikwete atalipiza kisasi cha
Mkapa kuwaua Waislamu, wao wanapayuka hovyo. Mfano ni gazeti la "Habari
Njema" Linalokosoa gazeti la kiislamu.Kikwete ni wa CCM
Kikwete wa Jakaya ni uteuzi wa CCM. Tanzania ni nchi ya vyama vingi.
Kwamba CCM wamemteua mtu wao, hiyo siyo sababu tosha kulifanya Gazeti la
Kikristo kuanza kupayuka. Mbona? Habari Njema wanasahau kwamba wanasiasa
ni WAONGO. Sasa wanalitapeli Kanisa. Badala ya Gazeti la kidini kuwaonya
kondoo dhidi ya MBWA MWITU wanasiasa, Wao wanaanza kufurahia posho
wanayotupiwa kama KUKU atupiwavyo mahindi kumbe yanaashiria mwisho wake.
GTV Tumekataa kumeza ndoano ya CCM hata waweke chambo gani. Tutatumia
kila lililo ndani ya uwezo wetu kuwaonya Watanzania wajihadhari na
mnyama huyu CCM. Amewameza wenzetu kwa zaidi ya miaka arobaini, na sasa
anatutapeli tumwachie nafasi aendelee kutumeza kwa miaka mitano ijayo.
Haiwezekani, Hatukubali, Hatutaki, Tena tumekataa.

Uhuru wa CCM kumteua Kikwete wa Jakaya, unapaswa kuishia pale uhuru wetu
kuteuliwa kama wagombea binafsi unapoanzia. Kuanza kushangilia na
kutumia pesa za walipa kodi kununua nafasi kwenye vyombo vya habari ili
kutoa kauli za kiburi, Hakutaisaidia CCM. Ikiwa gazeti la kiislamu
liliandika kwamba Waislamu hawamtaki Kikwete kwani ni kibaraka wa
KANISA, "Habari Njema" Wangepaswa kumkemea Kikwete aache kulitumia
Kanisa kwa manufaa yake kisiasa. Akifikiri anajitengenezea mazingara ya
kukubaliwa na Wakristo, atajikuta pabaya. Waislamu wameanza tayari
kumkana kwamba yeye kikwete si mwenzao. Wakristo nao sidhani kwamba
watadanganyika na tabia ya ghafla ya Kikwete kuwa mgeni makanisani.
Wengi wameanza kuifananisha tabia hiyo na pipi apewazo mtoto aache
kulia. Wanasiasa Tanzania bado wanafikiri kwamba Watanzania ni watu
wasioweza kuchambua mambo. Mwislamu Kikwete anapoanza kuingia kwenye
majumba ya ibada {MAKANISA} bila kuukana uislamu ni sawa na kuwatania
wenye imani hizo. Kifupi niseme
"ANAKUFURU." Sambamba na hilo, Mkristo Benjamin Mkapa anapojifanya
kuingia misikitini bila kusilimu awe Mwislamu, hiyo ni KUFURU kwa dini
ya Kiislamu. Nasema hivyo kwa sababu wote wanajua nini kinapaswa
kufanyika ndipo mtu awe muumini wa dini. Kuyakataa masharti ya dini
husika na uingie humo ukiwa KAFIRI, kisha utoke humo ukiwa
umewadanganya, hiyo inaonyesha kukosa adabu kwa Mungu anayeabudiwa na
watu hao. Ikiwa wanasiasa hawawezi kuikosea adabu bendera ya nchi, Vipi
wakose adabu kwenye sehemu za kuabudia??? Wanakuja makanisani na ahadi
za uongo. Wachungaji na Mashehe wanakubali vipi wanasiasa waingize
unajisi Makanisani na Misikitini? Sehemu Takatifu mnakubalije Kikwete
aingie na uchafu wake na atoke akiwa amewachafua? Kulingana na imani ya
Kikristo Kikwete Mwislamu lazima aukane uislamu ndipo apewe nafasi ya
kufanya chochote Kanisani. Mambo ni hivyo hivyo Misikitini. Kafiri
hawezi kuruhusiwa kuingia Msikitini akiwa amevalia viatu, huku amebeba
nyama ya nguruwe. Hiyo ni KUFURU na kuikosea adabu KORAN TUKUFU.
Wanasiasa wanapoingia Misikitini kwa lengo la kuwadanganya Waislamu
wawaunge mkono, ni sawa na kuingia na nguruwe msikitini. Wanakuja na
pesa za Rushwa na wanawanunua wakuu wa dini. Hilo ni kosa linalopaswa
kukemewa na magazeti yote ya kidini. Tunalishangaa "Habari Njema"
Gazeti la Kikristo kuanza kumpigia Debe Kikwete wa Jakaya na kusema ni
wa wote. Wangefanya vizuri kusahihisha hilo na kusema Kikwete ni wa
Jakaya na tena wa CCM. Watanzania wana mtu wao.Tunachoomba ni kwamba
Watanzania wapewe nafasi ya kumchagua yule watakaeona anawafaa
kuwaongoza. Kujaribu kuwalazimishia Kikwete, msishangae akiwa kiwete
kama Mkapa. Nyerere alitulazimishia Mkapa, akatoka akiwa kiwete, Mkapa
asijaribu kutulazimishia Kikwete kwani Mungu anajua nini cha kufanya na
wale wanaowatesa Watanzania. Sina tatizo na uteuzi wa CCM, lakini
namuomba Bwana Kikwete asije Kanisani kwangu kututapeli kwamba yeye
anatupenda Wakristo. Ikiwa anaupenda kweli Ukristo, Kipimo chake ni
aikubali Injili ya Yesu, Kisha amwamini Yesu badala ya Mtume Mohamad,
Halafu tumbatize aitwe jina lolote hata kama akipenda kubaki na jina
lake Kikwete hatuna tatizo hapo. Akikubali hayo tunamkaribisha
kanisani. Lakini siyo aje kutuletea pesa za wizi.Huku akijifanya
anachangia miradi ya dini ya Kikristo. Gospel TV tunaunga mkono gazeti
lililomkosoa Kikwete na kusema kwamba Waislamu wamemshitukia Kikwete.
Nasi GTV tunasema kwamba hata Wakristo wa kweli, Tumemshitukia Kikwete.
Labda ajaribu mbinu nyingine. Lakini hii ya kuja Kanisani mwenye dhambi
halafu aondoke ametuingiza dhambini tumeikataa sawa na tulivyomkataa
shetani na mambo yake yote.

Wanasiasa Huaribu taratibu za ibada

Aliyekuwa Rais wa mabavu na Jazba Tanazania Mzee Mkapa akiwatapeli
Maaskofu kwamba serikali haina dini.

Kuwakubali wanasiasa wasiyoiamini Injili makanisani, ni sawa na
kumwalika Shetani Kanisani. Fikiri usumbufu Waumini wanaoupata wakati
mtu kama Kikwete anapolitembelea Kanisa. Kwanza askari kanzu
wanalitembelea kanisa siku tatu kabla ya ziara. Kanisa linapekuliwa kila
kona. Wanaofanya kazi hiyo ni askari walevi wasio na sare za kazi. Eti
wanahakikisha kwamba Kikwete atakuwa salama Kanisani hapo. Siku ya ziara
ikifika, Kanisa linavamiwa na askari wenye silaha kali. Nusu ya watu
watakaolijaza kanisa siku hiyo ni maofisa usalama wa Taifa, Pamoja na
maofisa usalama wa Kikwete. Watakuwa wamevalia kiraia, lakini nyuso zao
zitakwambia hawa siyo waumini wa kawaida. Hata ibada itawashinda kufuata
kwani hawajui chochote kuhusu Kanisa. Mchungaji wa Kanisa ambaye
alipaswa kuandaa mahubiri kwa waumini, analazimika kuandaa ujumbe
uliojaa sifa kwa Kikwete badala ya Mungu. Usisahau kwamba mchungaji huyo
alilazimika kusimama nje kwa masaa zaidi ya mawili akimngoja mgeni rasmi
Kikwete aingie Kanisani
hapo. Huu ndio usumbufu tunaoufananisha na kumwabudu mwanadamu badala
ya Mungu. Ibada ya siku hiyo inageuka kutoka kumwabudu Mungu, na
inakuwa ibada ya kumwabudu kikwete. Ndio maana tunapinga tabia ya
wanasiasa kutumia sehemu za ibada kuabudiwa badala ya Mungu. Hatupingi
mtu yeyote kuingia kanisani au msikitini, lakini mtu huyo hata akiwa
nani, anatakiwa afuate utaratibu wa dini husika. Kutatanisha ibada za
watu eti ni Kikwete anakuja, Hiyo ni tabia wakuu wa dini wanapaswa
kuipinga kwa nguvu zote. Kikwete hawezi kuchukua nafasi ya Mungu. Akija
Kanisani aje kama muumini mwingine yeyote. Mambo ya kuingia kanisani na
kikosi kizima cha kumlinda huku wakiwa na silaha kali, pamoja na macho
ya kuwatisha waumini yanatakiwa yakomeshwe mara moja. Kwa nini Kikwete
awasumbue waumini kwa vishindo vya kuingia Kanisani na kuichukua nafasi
ya Mungu? Viongozi wa dini wangejua ibada inavurugwa kiasi gani
anapoingia mtu kama kikwete, wangemsihi akome kuingia humo na mbwembwe
za kuwatisha waumini.Wanasiasa ni watu wanaopenda kutisha. Mahali pa
kutembea kwa miguu wao watatumia gari zaidi ya kumi. Askari wa usalama
barabarani watatangulia na pikipiki zaidi ya tano, halafu zitafuatiwa
na Land Rover mbili zilizojaa wana FFU na bunduki pande zote, Halafu
yafuate magari zaidi ya kumi na bado la Bwana Kikwete halijawasili.
Mchungaji atalazimika kusimama kwa muda mrefu akisubiri Kikwete aingie.
Akiingia, Utaratibu wa Ibada unavurugika na wa Kikwete unaanza.
Usumbufu huu ndio tunaosema kwamba hatuutaki. Wanasiasa wafanyie
kampeni zao nje ya majumba ya ibada.


Kikwete na Kanisa Kwa muda gani?

Tunajua wazi kwamba Kikwete na kanisa sasa watakuwa kama pete na kidole.
Lakini kwa muda gani? Wanasiasa huwaadaa watu wa dini wanapotafuta kura.
Lugha kama Kikwete ni wa wote hazitaisha midomoni wakati wa uchaguzi.
Unafiki huu tunataka ukome. Uongozi siyo kuikana dini. Inawezekana mtu
akawa kiongozi bila kuikana dini yake. Ukija kanisani kwa kuwa unataka
kuchaguliwa, huo ni UNAFIKI. Kama kweli ulikuwa mtu wa dini zote, basi
tungekuona kanisani tangu mwanzo na siyo wakati wa uchaguzi. Hivi
wanasiasa wanamdanganya nani? Mungu au wanadamu? Watu wa dini
wakiwakosoa wanasiasa wanaowaua watu bila sababu, wanaambiwa
wasichanganye dini na siasa. Kwa maneno mengine, Mkapa Mkristo ana uhuru
wa kuwaua waislamu Zanzibar, na asiulizwe chochote na waislamu wala
Wakristo. Eti wakiuliza, wanachanganya dini na siasa. Mgombea urais
akiwa Mkristo, Ataanza kuwatapeli waislamu kwa kujifanya anachangia
miradi ya maendeleo misikitini. Akishachaguliwa mambo yanakuwa kinyume.
Mfano mzuri ni Mkapa. Alipokuwa
akiomba kura, alisema yeye ni Rais wa wote. Alipochaguliwa alianza
kuwabagua Waislamu. Aliungana na Amerika kuamini kwamba kila Mwislamu
ni Ghaidi. Ikawa kupata hati ya kusafiria ukiwa Mwislamu ni sawa na
ndoto. Hayo yote yanafanyika chini chini, huku Mkapa akihubiri kwamba
yeye ni Rais wa waislamu na Wakristo. Huu ni unafiki tunaotaka ufike
kikomo. Ikafika siku ya siku. Ndugu zetu Zanzibar wakatumia haki yao ya
kikatiba kusema kwamba hawaitaki CCM. Mkapa Rais Mkristo, akaamuru
Waislamu zaidi ya sabini wauawe, na wengine wakakatwa viungo vyao ili
kuwafundisha adabu. Wakristo wenye mtazamo kama wa gazeti la Habari
Njema wakashangilia. Walichosahau ni kwamba wanasiasa katika kulinda
maslahi yao wanaweza kuua yeyote. Munishi Mkristo niliposema kwamba si
haki Mkapa kuwaua Waislamu, Kanda zangu zilipigwa marufuku Tanzania,
Mkapa Huyo huyo Mkristo, akaamuru nikamatwe, na Polisi Tanzania
wakatangaza kwamba wananisaka. Rais Mkristo anamtafuta Mchungaji
Mkristo amuue kwani Mchungaji alimkemea alipowaua Waislamu. Hiyo ndiyo
siasa. CCM na huyo waliyemteua wawadanganye wengine lakini GTV
Hatudanganyiki na unafiki wao.Kinachotushangaza zaidi ni kwamba wakati
wa KAMPENI ni bado. Tena uchaguzi ni bado. Isitoshe vyama vingine
havijatangaza wagombea wao. Gazeti la dini limeanza KUPAYUKA. Serikali
nayo inafurahishwa na habari hizo. Ikiwa kanda za Munishi zilifungiwa
kwa kusema Mkapa ni MUUAJI, Vipi gazeti la Habari njema halijafungiwa
kwa kusema kwamba Kikwete ni wa watu wote? Si hapo pia wamechanganya
siasa na dini? Ikiwa mnapokea SIFA, Mbona maonyo mnayafungia nje? Ni
unafiki huu ndio ulionifikisha mahali pa kusema, "Siasa ni uongo, na
kwamba wakati umefika kwa watu wa dini zote kujitenga na siasa. Kila
dini ianze harakati za kujikomboa kutoka minyororo ya wanasiasa.
Tutafanikiwa hilo kwa kuishinikiza serikali ya CCM kuibadili KATIBA ili
iwaruhusu wagombea BINAFSI. Katiba ya sasa inasema mtu hawezi kuwa Rais
bila kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa. Nasi tunasema, Huwezi
kujiunga na uongo ili uwatoe waongo.Kwani siasa ni uongo.

Uvumi Mitaani

Kuna uvumi kwamba Kikwete wa CCM anapenda sana kwenda DISCO usiku. CCM
hawakukosea waliposema Jakaya Kikwete ni kijana. Miaka 55 na kufanya
mazoezi pamoja na kula vizuri, kumemfanya Kikwete audanganye umri wake.
Kweli anaonekana kijana jambo linalompatia marafiki wengi wa kike na wa
kiume. Sura yake ikilinganishwa na Mkapa, Kikwete anaweza samehewa mengi
kwa kuangaliwa usoni tu. Wakati Mkapa akiongea tu watoto wanaingia
uvunguni kwa kuiogopa sura tu. Duru kutoka wanaomfahamu Kikwete kwa
karibu, Wanasema huyo Bwana siyo mchezo. Wanasema ukikutana naye akiwa
amevalia JEANS na fulana nyepesi jioni, Labda mtu fulani akushitue huyu
ni Mheshimiwa Kikwete. Lakini hivi hivi tu, huwezi kumtambua. Wanasema
Jakaya Kikwete alichangia sana katika kusababisha Mwanamuziki mmoja
nchini Tanzania kufungwa jela maisha pamoja na Familia yake yote..
Inadaiwa mwanamuziki huyo alimbusu mmoja wa marafiki wa kike wa Kikwete.
Duru hizo zilitufahamisha kwamba Kikwete akitumia ushawishi mkubwa alio
nao
Serikalini aliwaamuru Polisi wamsukie kesi nzito mwanamuziki huyo.
Kweli mwanamuziki huyo alikamatwa pamoja na jamii yake yote na
kufunguliwa shtaka la kuwabaka watoto zaidi ya kumi Akiwa yeye na jamii
yake. Hukumu ya kesi hiyo ilikuwa kifungo cha MAISHA kwa familia yote.
Hiyo ni hukumu ya kwanza duniani. Kwenye ulimwengu wa Siasa na
Wanasiasa chochote chaweza kutokea. Ama kweli CCM safari hii,
wametuletea kijana kweli. Ikiwa Kikwete waziri anaweza sababisha
Familia nzima kwenda jela maisha. Akiwa Rais Mungu apishe mbali asije
akaamuru mkoa mzima uchomwe moto. GTV tunasema kama ni kweli
Mwanamuziki huyo alifungwa kwa sababu za kisiasa, Tunaitaka Serikali
imwachie huru mara moja bila masharti yeyote.


"Kikwete Tosha" asema Mchungaji

Mchungaji Paul M.K. Mduma aliyekuwa Mkurugenzi wa Muziki kwaya ya
Uinjilisti Arusha mjini kabla ya kuhamia Kenya na kutawazwa kuwa
Mchungaji wa kanisa la AIC (Afirican Inland Church) Ameishi Kenya kwa
miaka 10 na Kwa sasa hivi yuko Arusha Mjini kama Mhubiri wa kujitegemea
akifanya kazi na makanisa yote yanayomwalika, huku bado akiwa msharika
wa KKKT Usharika wa Arusha Mjini.

Kufuatia malumbano kati ya magazeti ya Kiislamu na Kikristo kumhusu
Kikwete, Mchungaji Paul Mduma amejitokeza kusema "Kikwete Tosha." Akiwa
katika Ofisi za GTV Nairobi Kenya mchungaji Mduma alielezea masikitiko
yake kwamba, vyombo vya habari vimeanza kumchafua Kikwete aliyemjua
tangu akiwa mwanafunzi Kibaha Secondary School. Alidai kwamba walisoma
wote kwa muda wa miaka minne. Tangu mwaka 1966 hadi 1969 wakati Kikwete
alipochaguliwa kwenda Tanga High School kidato cha tano na sita.
Mchungaji mduma aliongeza kusema: "Japo sikuchaguliwa kuendelea na
masomo ya juu kama Kikwete, Sina chuki binafsi naye na nitamsifu
inapostahili. Kwa hiyo kuhusu masuala ya kumjua Kikwete hakuna wa
kufananishwa nami Mchungaji mduma." Alisisitiza mchungaji.

Akizungumzia uhusiano wa Kikwete na wanafunzi wenzake Mduma alisema: "
Kikwete alikuwa mpigania haki shuleni jambo lililopelekea kuchaguliwa
kuwa Rais wa shule (School President) Aliitumia nafasi hiyo vyema na
alitokea kupendwa sana na wanafunzi na hata waalimu, Hususan Mwalimu wa
michezo Mr. Konic Pamoja na Head Master wetu Paul Figveg. Siyo kwamba
Kikwete alikuwa maarufu kwa masomo pekee, bali alikuwa mpenda michezo
hasa mchezo wa mpira pamoja na kupokezana vijiti. Shuleni wanafunzi
walikuwa wakimwita "OJUE" Jina lake maarufu la michezo.


Ni sababu hizo na nyingine ndizo zinazomfanya Mchungaji Mduma aseme
Kikwete Tosha. Anadai kwamba Watanzania watakosea sana kumchagua mtu
mwingine isipokuwa Kikwete, Tena anausifu umaarufu wa Kikwete kutatua
matatizo jambo alilosema liliwafanya wakuu wa Chuo Kikuu kumwita atatue
mizozo ya wanafunzi wakati Kikwete alikuwa Sekondari. Mduma anadai
kwamba uwezo huo wa Kikwete atautumia kutatua matatizo mengi duniani
kama watanzania watampa kura.

Kauli ya Mchungaji Mduma itapokelewa kwa hisia tofauti hasa tukizingatia
kwamba Waislamu wanamuona Kikwete kama Kibaraka wa Kanisa, Huku Wakristo
wakishindwa kumwamini kwani wanadai Kikwete ni Mwislamu anayeweza
kutumia nafasi yake kama Rais kuisilimu Tanzania. Mchungaji Mduma
alisema hiyo siyo sababu. Kikwete alienda kuchangia Kanisa na siyo
kuendesha ibada za Kanisa. Kanisa ni chombo cha jamii kwa hiyo siyo kosa
kwa kiongozi kuchangia miradi ya kijamii bila kujali dini yake.
Aliongeza kusema kwamba Kwa Kikwete kuyachangia Makanisa ni kama
kurudisha shukrani kwani yeye Kikwete alisomea shule za misheni. Lakini
mbona kurudisha shukrani huku kumekuja wakati wa uchaguzi? wengi
wanajiuliza kwa nini Kikwete asingefanya hivyo wakati akiwa waziri?

GTV Tulipomuuliza Mchungaji Mduma nini maoni yake kuhusu wachungaji
wanaomsakama Kikwete kwa sababu za udini? Yeye aliwaita wachungaji kama
hao WANAFIKI. Alihoji kwamba wakati wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi,
Maaskofu walikuwa wakimwalika katika sherehe za kuwasimika Maaskofu
kwenye kazi ya Mungu. Hawakuita waziri Mkristo bali walimwita Rais wa
wakati huo Mwinyi. Iweje sasa ubaya ambao hawakuuona kwa Mwinyi wauone
kwa Kikwete? Aliwataka kuachana na mawazo potovu ya UDINI ambayo
yanaweza kuitumbukiza Tanzania katika matata yasiyo na sababu. Alimaliza
kwa kusema kwamba Tanzania ni nchi ya amani na hawezi kukubali watu
wachache kutumia dini kuvuruga amani.Mchungaji Faustin Munishi Rais Mtarajiwa Tanzania Amesema kwamba Hakuna
uchaguzi Tanzania bila ya Katiba mpya. Watakaowaburuza Watanzania
kuingia kwenye uchaguzi bila katiba kubadilishwa, wajue wanafanya hivyo
kinyume na matakwa ya Watanzania walio wengi. Alisema: "Nia yangu ya
kuwa Rais wa Tanzania bado iko pale pale. Kwamba katiba hairuhusu
wagombea binafsi, hiyo hainifanyi nijiunge na chama chochote cha kisiasa
ili nitimize masharti ya KATIBA. Kwangu siasa ni uongo, na siwezi
kujiunga na uongo niwatoe waongo. Ikiwa CCM hawataibadili Katiba iruhusu
wagombea binafsi, basi tutaiasi katiba tuandike yetu. Wakichaguana nasi
tutachaguana. Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa KATIBA ya Injili na
serikali ya Injili, Rais wa Injili na Bunge la kiinjili. Hapo ndipo
tunapoelekea. Siyo ajabu kwani tayari tuna nyimbo za GOSPEL kilichokuwa
kimebaki ni KATIBA ya Gospel Itakayounda tume ya Gospel ya uchaguzi
utakaomchagua Rais wa Gospel atakayeunda Serikali ya Gospel akitumia
wabunge wa Gospel. Waislamu wakiona vyema wajiunge na Gospel
tutawakaribisha. Wakiona waunde yao ya SHARIA, ni sawa. Pia kwa mara ya
kwanza Tanzania itakuwa nchi ya serikali zaidi ya kumi. nayote hayo
yatafanyika kwa amani. Kikwazo cha amani Tanzania kitakuwa ni CCM pale
watakapokataa mabadiliko, na kungangania madaraka.Kama kawaida yao
wataanza kuwalaumu wengine. Lakini wananchi safari hii wameerevuka na
wanamjua mbaya wao ni nani.CCM ndiye nyoka anayestahili kupondwa
kichwa."

KATIBA SIYO MALI YA CCM

Katiba ya Tanzania ni ya watanzania. Siyo mali ya CCM. Lazima kila
mtanzania ahusike katika kuirekebisha au kuibadili. Kuna mengi
yanayohitaji marekebisho na mengine yatatolewa kabisa. Najua kwamba
nikiingia ikulu na katiba ya sasa itanikwamisha mengi. Tanzania ni sawa
na gari iliyonoki injini. Inataka matengenezo kamili ndani ya injini.
Siwezi kuifanyia Tanzania MAREKEBISHO INAYOSTAHILI bila ya katiba mpya.
Hata kama kipengele kimoja kitabadilishwa niweze kugombea bila chama cha
kisiasa, hilo siyo lengo langu.

Lengo langu ni kuleta mabadiliko ambayo ndiyo kiu ya watanzania wengi
wakubwa kwa wadogo. Hatuwezi kuwa na nchi yetu, bila katiba yetu. Tena
katiba haiwezi kuwa yetu kama haina mchango wa mawazo yetu. Tunahimiza
zoezi la kukusanya mawazo kutoka kwa watanzania wote lianze ndipo katiba
irekebishwe. Bila hilo kufanyika hakuna sababu ya kufanya uchaguzi
kwani CCM watatumia mapungufu yaliyoko kwenye katiba kushinda uchaguzi
kiulaini.

Tumeliona hilo. Ndiyo maana tunasema kwamba hakuna aliyehitimu kuingia
katika uchaguzi na katiba ya sasa. Ina mapungufu mengi, Hatuitaki, Ni
batili. Yeyote atakaeingia kwenye uchaguzi na katiba ya sasa ajue
anafanya hivyo kinyume cha sheria. Ndiyo ni kinyume cha sheria kwa
sababu Watanzania wengi wanataka KATIBA MPYA. Kujaribu kuwaburuza ili
waingie kwenye uchaguzi bila ya kuibadili katiba ni mbaya kuliko wao
kuchukua silaha na kuanza kudai haki zao kwa mtutu wa bunduki. Hatuombi
hali ifikie hapo kwani itatuumiza wote. Lakini ikibidi, Hakuna jinsi.


Kuhusu baraza la mawaziri, nilisema wazi kwamba mimi sitakuwa na uwezo
wa kuunda baraza la mawaziri. Katiba ya sasa inamruhusu rais kuunda
baraza lake la mawaziri. Katiba mpya italiruhusu bunge kuunda baraza
letu la mawaziri. Sifa za watakaogombea nafasi za uwaziri lazima
ziambatane na taaluma zao katika wizara husika. Wakati wa kuchaguliwa
waziri kwa sababu za kikabila, kiundugu na kirafiki, UMEKWISHA. Hata
hapa kuna wengi tayari nimeona wataifaa Tanzania katika baraza la
mawaziri. Mtu kama Augostino Moshi ukisoma posti zake utaona uanasheria
ndani yake.


Hawa ndio tunaotaka kuwahimiza wagombee nafasi za waziri wa sheria na
katiba. Wabunge wakiridhishwa na kuhitimu kwao katika fani husika
watawachagua. Nimemtaja Moshi siyo kwa sababu ni mchagga, bali nipate
nafasi ya kujibu swali lake. Aliniuliza kama nakimudu kiingereza. Ukweli
ni kwamba kiingereza nakimudu vizuri.

Lakini nilijifunza kwa njia ngumu zaidi. Nikija Nairobi mwaka 1984
nilikuwa siwezi kabisa kuwasiliana kwa kiingereza. Jambo hilo lilinikera
sana. Niakaamua kuanzia mahali. Biblia ndicho kitabu kilichokuwa
hakibanduki mikononi mwangu. Nilikuwa nimemaliza kuisoma na kuirudia
mara tatu. Nikanunua madaftari makubwa ya kuandikia kama matano, halafu
nikanunua Biblia ya kiingereza. Nilianza kuandika neno hadi neno,
nikamaliza kuandika agano jipya. Mengi nilielewa maana kutokana na
ukweli kwamba nilikuwa nimeyasoma katika Biblia ya kiswahili.
Yaliyonishinda matamshi ilinibidi ninunue biblia katika kaseti. Yale
ambayo sikuelewa kuyatamka, Biblia ya kaseti ilinisaidia kujua
yanatamkwa vipi.

Hata kabla ya kumaliza agano la kale tayari nilikuwa na kiingereza kingi
sana akilini mwangu. Tayari niliweza kuwasiliana kwa kiingereza kuliko.
Nasita kusema kuliko wasomi wengi Tanzania, lakini ukweli unabaki hivyo.
Sasa hivi ndipo kasi ya kujifunza kiingereza imeongezeka Tanzania.
Wakenya na Waganda wamefungua shule uchwara na wanaziita za kimataifa
kwa sababu tu wanazingatia somo la kiingereza. Ningekuwa najua kutumia
kompyuta wakati huo, nisingepitia njia ngumu hivyo kukijua kiingereza.

Lakini sijuti kwani maneno mazito ndani ya Bibilia yamekiongezea uzito
kiingereza ninachotumia kuzungumza na hata kuandika. Sitaki nijisifu
kwamba Kiingereza changu ni sawa na kile cha malkia wa UINGEREZA, lakini
nitakuwa mpumbavu gani nishindwe kujieleza kwa lugha rahisi kuliko zote
duniani? Kiingereza kwa sasa ndiyo lugha rahisi kuitumia kuliko hata
kiswahili. Haya niliyoyaandika hapa hakuna mahali katika kompyuta
naweza kufanya "SPELL CHECKING", sababu ni kiswahili. Lakini ingekuwa
kiingereza, bila kujali natumia programu gani nitapata mahali pa
kuisahihisha kazi yangu kiulaini.

Ni urahisi huo ndio unaonipa mashaka kwamba wengi hawajui kiingereza.
Kuna rafiki yangu simtaji. Ni mwandishi wa habari katika gazeti la
NATION lichapishwalo kwa kiingereza kila siku nchini Kenya. Ukisoma
makala zake, utapenda. Mpangilio wa lugha, usahihi wa maneno, NK. Lakini
wacha akuandikie barua ya mkono, Au akutumie ujumbe mfupi kwa simu za
kipepesi. Utashangaa mbona kiingereza chake kibovu?

Kumbe amelemazwa na kompyuta ambayo inamfanyia kila kitu kuanzia "SPELL
CHEKING" mpaka na mtiririko wa lugha. Je ni kitu cha kujivunia kujua
kiingereza? Hapana. Hata wanaokiongea au kukiandika vibaya siyo makosa
yao. Siyo lugha yao ya kwanza maishani.

Pamoja na umuhimu wa kiingereza duniani leo, Siungi mkono kasi
watanzania waliyo nayo katika kukikimbilia kiingereza. Wengi wanalipa
pesa za kutisha kwenye shule ambazo zinatilia mkazo kiingereza, Wengine
wanawapeleka watoto wao nje Kenya Uganda, Na hapo nimetaja sehemu chache
sana. Yote ni watoto wajue kiingereza. Kuna tofauti kati ya kuelimika na
kujua lugha. Lakini kwa watanzania wengi hilo hawalijui. Wanafikiri
kuelimika ni kujua Lugha. Kuna uwezekano wa kuzijua lugha tofauti bila
kuwa na elimu. Lakini kiingereza tu, sioni ulazima wa wazazi Tanzania
kwenda kasi wanayokwenda kukifukuzia kiingereza. Kuna njia nyingi za
kuweza kuijua lugha yeyote bila kuingia gharama kubwa wanazoingia
watanzania.Nimalize kwa kusema kuna njia nyingi za kumuua panya. Ukiweka
mtego utamnasa atakufa. Ukiweka dawa ya sumu jikoni, panya atakula na
atakufa. Lakini ole wako mtoto wako akidhani hiyo uliyoweka jikoni ni
peremende. Uliyotarajia yampate panya yatampata mtoto wako.

Watanzania wengi wameamua kumuua panya wa kiingereza wakitumia sumu
jikoni. Tayari nimeiona hatari mbele yao. Nani awaambie njia nyingine
rahisi ambayo ni kumchagua Munishi awe rais wa Tanzania chini ya katiba
mpya nitainua kiwango cha elimu. Kiwango cha elimu kikiinuka Lugha
zozote hazitakuwa ngumu watanzania kuzitumia. Naujua ugumu nilioupata
kujua niyajuwayo, sitopenda mtoto wa kitanzania apitie niliyoyapitia
kupata elimu.

Bwana Moshi nafikiri nimekujibu. Nashukuru kuniuliza hilo, kwani CCM
wamekuwa wakimtesa sana Mrema kwa hilo. Najua hata mimi wataanza kutumia
hilo kama mtaji wa kunipinga nisiwe rais. Lakini hata Mkapa kiingereza
chake ni cha kubabaisha pamoja na kwamba alisomea lugha ya kiingereza
kama somo ili aweze kuwa mhariri wa DAILY NEWS. Kwa mtaji wa lugha tena
ya kiingereza hapa wamefika. Watafute jingine. Ikulu nitaingia tu. Nia
na sababu ninazo. Kama walifikiria kwamba uwezo ni kiingereza, basi hata
uwezo ninao.

Kuhusu swali la uraia, maoni yangu ni kwamba Mtanzania anayetaka kurudi
kuuchukua uraia wake, itabidi aukane uraia aliouchukua ugenini. Ni maoni
yangu binafsi. Lakini kwa sababu tutabadili katiba, sijui maoni ya
watanzania yatakuwaje kuhusu hilo. Kulingana na katiba ya sasa, Rais
anakuwa kila kitu. Ndiyo maana maswali kama utafanyaje kuhusu hili na
lile yanajitokeza kwa wingi. Lakini KATIBA MPYA mambo hayatakuwa hivyo.
Kila jambo litashughulikiwa na wizara husika na wanataaluma husika.

Swali la uraia litashughulikiwa idara ya uhamiaji. Katiba mpya
itawatengenezea mazingara mazuri ya kufanya kazi yao bila kuingiliwa
kisiasa. Kwanza kutakuwa hakuna chama cha kisiasa madarakani.

Maswali mengi niliyatarajia, na bado nayatarajia. Wengi wamezoea sana
utawala wa CCM wala hawajui itakuwaje bila CCM. Mimi naiona Tanzania
mpya bila CCM. Picha hiyo iko akilini mwangu. Niko tayari kuendelea
kuwafafanulia zaidi picha ya Tanzania mpya. Naiona iko nami. Mungu
ameiweka maishani mwangu. Hakuna kitakachonitenga na Tanzania mpya iliyo
maishani mwangu, labda maisha yenyewe ndiyo yanaweza kunitenga na
Tanzania mpya na katiba mpya, halafu MAISHA MAPYA YA WATANZANIA. Mungu
bariki watanzania. Waonyeshe Tanzania mpya bila CCM.

Jiandikishe Hapa
Hata kuishi Amerika ni haki yako
 
Ikiwa CCM hawataibadili Katiba iruhusu
wagombea binafsi, basi tutaiasi katiba tuandike yetu. Wakichaguana nasi
tutachaguana. Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa KATIBA ya Injili na
serikali ya Injili, Rais wa Injili na Bunge la kiinjili. Hapo ndipo
tunapoelekea. Siyo ajabu kwani tayari tuna nyimbo za GOSPEL kilichokuwa
kimebaki ni KATIBA ya Gospel Itakayounda tume ya Gospel ya uchaguzi
utakaomchagua Rais wa Gospel atakayeunda Serikali ya Gospel akitumia
wabunge wa Gospel.
Waislamu wakiona vyema wajiunge na Gospel
tutawakaribisha. Wakiona waunde yao ya SHARIA, ni sawa. Pia kwa mara ya
kwanza Tanzania itakuwa nchi ya serikali zaidi ya kumi. nayote hayo
yatafanyika kwa amani.

Mkorogo mtupu!

Lakini hata Mkapa kiingereza
chake ni cha kubabaisha
pamoja na kwamba alisomea lugha ya kiingereza
kama somo ili aweze kuwa mhariri wa DAILY NEWS. Kwa mtaji wa lugha tena
ya kiingereza hapa wamefika. Watafute jingine. Ikulu nitaingia tu. Nia
na sababu ninazo. Kama walifikiria kwamba uwezo ni kiingereza, basi hata
uwezo ninao.

Kazi kweli kweli....
 
Lakini baada ya Mkapa Mkristo
kuwaua Waislamu Zanzibar, Watanzania wamejua kumbe serikali na CCM zina
dini.

Haya ni mawazo ya mtu binafsi na si ya watanzania. Kuna kazi kubwa sana kuwaelimisha watu wenye mawazo kama haya.

Watanzania tuwe makini na watu wanaoibua hisia za udini na kubaguana.

Mkapa, Kikwete, na Paparazi muwazi wanaweza kujadiliwa kama wao na nafasi zao katika Taifa kama watanzania na si kwa dini zao.

Inatupasa tukue kifikra!
 
Mie Munishi nilishamfuata kwenye YOUTUBE na kumpa maneno yake.

Alijitahidi kunijibu na nilitumia maneno ya kwenye BIBLIA, na tena maneno ya Yesu kuwa "Ya Kaisaria mpeni Kaisaria na ya Mungu Mpeni Mungu - Akalala mbele.
 
Back
Top Bottom