Elections 2010 Mchungaji Pentekoste atangaza kugombea urais

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Na Elizabeth Suleyman

uraismchungaji.jpg

MCHUNGAJI wa Kanisa la Tanzania Assembles of God (Tag) Macmilan Lyimo


MCHUNGAJI wa Kanisa la Tanzania Assembles of God (Tag), lililoko eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam Macmilan Lyimo, jana alitangaza nia yake ya kumvaa Rais Jakaya Kikwete, katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Alisema lengo lake ni kutaka kupata uongozi na kuasisi taifa jipya la Tanzania na kwamba kizazi cha walioleta uhuru yaani Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeshamaliza muda wake, na ni vyema kikaondolewa kutokana na kushindwa kuleta maendeleo hapa nchini.


Lyimo ambaye alisema atagombea nafasi ya urais kupitia tiketi ya Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kinachoongozwa na Mwenyekiti Augustine Mrema, aliliambia gazeti la Mwananchi jana katika mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisini kwake kwamba, nia ya kugombea ni kuasisi taifa jipya la Tanzania litakalokuwa na misingi inayokubalika na lenye mueleleko wa kisasa.

“Ukiangalia siasa ya sasa hivi imeshaingia doa, kutokana na wanaoshikilia nafasi hizo kuivuruga na matokeo yake, Tanzania inakuwa na siasa chafu ya watu kulala makaburini, kwenda kwa waganga, na kufanya mambo ya kishirikina, lengo ni kutaka tu! kupata nafasi ambazo zina maslahi yao binafsi”, alisema Lyimo.

Alisema cha kushangaza viongozi waliotokana na mfumo wa kuleta uhuru zaidi ya miaka 50 iliyopita, bado wanaendelea kutembeza mabakuli na hakuna jitihada zozote ambazo wamezifanya, badala yake nchi inaishia kuingia katika dimbwi la ufisadi.


Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Nisawa lakini anania ya kweli? na ukitupatia CV yake itapendeza sana.
ni sawa mkuu kujua wasifu wake, lakini wasifu unatusaidia nini?
mimi labda ni mtazamo wangu tu, wasifu si uongozi, mbona hata jk ana wasifu mzururi lakini haujatusaidia kitu? zaidi ya pumba tu?
 
I don't know if it's just me but I'm usually very skeptical of religious leaders getting into politics. For some reason I think religious practices contradict political practices. But anyway it is his constitutional right.
 
Absolutely right MWANAFALSAFA 1. Moreover, some of those who declare their intentions are out to gain publicity while they know that they do not have what it takes to put up a serious fight. In any case I doubt if Mrema will his name to get to the ballot paper.

Only time will tell.
 
Back
Top Bottom