TANZIA Mchungaji Owdencalm Mpayo afariki dunia

Hilo jina alipewa na wazazi wake na hajawahi kulibadilisha.
Poleni sana wana Mbeya. Pole sana familia ya Moravian.

Mchungaji Mpayo hilo jina la kwanza alibadilisha ukubwani??? Kuna yule askofu mstaafu wa KKKT Iringa alipoenda Ujerumani akarudi na jina jipya la Owdenberg Mdegela.
 
Pumzika kwa amani mtumishi wa Mungu!! Tumefurahia sana sinema tulipokuwa watoto!! Poleni wana familia na kanisa kwa ujumla
 
Pole sana pumzika kwa amani
Bwana atamvika
IMG-20210120-WA0040~2.jpg
 
Kifo ni funzo kwa walio hai ajabu mtu anatesa wenzake,anauwa watu kwa ajili ya tumbo Hali you marehemu mtarajiwa
 
Poleni sana wana Mbeya. Pole sana familia ya Moravian.

Mchungaji Mpayo hilo jina la kwanza alibadilisha ukubwani??? Kuna yule askofu mstaafu wa KKKT Iringa alipoenda Ujerumani akarudi na jina jipya la Owdenberg Mdegela.
Mwanzoni aliitwa nani?
 

Mchungaji Owdencalm Mpayo amefariki dunia alasiri ya leo katika hospital ya Rufaa Mbeya alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibu.

Wakati wa uhai wake, Mchungaji Owdencalm Mpayo aliwahi kuhudumu kwenye nafasi mbalimbali za uongozi wa kiroho.

Mchungaji Owdencalm Mpayo ameshawahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Kiroho la NEW LIFE MINISTRY ambapo walikuwa wakizunguka nchi mbalimbali kushudia, kufundia kanuni nne za kiroho na kuonuesha sinema za maisha ya Yesu.

Pia Mchungaji Owdencalm Mpayo amewahi kuwa Kiongozi Mkuu wa kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi.

Marehemu ameacha mke, watoto watatu na wajukuu saba.

Watoto wa Mchungaji Owdencalm Mpayo ni Elihuruma Mpayo wa Swissport, Isaac Mpayo wa ITV RADIO ONE, na Rebecca Mpayo.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa.
Poleni sana wafiwa. Mungu awape faraja
 
Back
Top Bottom