TANZIA Mchungaji Owdencalm Mpayo afariki dunia

Heci

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
2,231
2,000
Screenshot_20210120-092912.png

Mchungaji Owdencalm Mpayo amefariki dunia alasiri ya leo katika hospital ya Rufaa Mbeya alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibu.

Wakati wa uhai wake, Mchungaji Owdencalm Mpayo aliwahi kuhudumu kwenye nafasi mbalimbali za uongozi wa kiroho.

Mchungaji Owdencalm Mpayo ameshawahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Kiroho la NEW LIFE MINISTRY ambapo walikuwa wakizunguka nchi mbalimbali kushudia, kufundia kanuni nne za kiroho na kuonuesha sinema za maisha ya Yesu.

Pia Mchungaji Owdencalm Mpayo amewahi kuwa Kiongozi Mkuu wa kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi.

Marehemu ameacha mke, watoto watatu na wajukuu saba.

Watoto wa Mchungaji Owdencalm Mpayo ni Elihuruma Mpayo wa Swissport, Isaac Mpayo wa ITV RADIO ONE, na Rebecca Mpayo.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa.
 

Mgiriki Jr VI

JF-Expert Member
Dec 20, 2019
2,015
2,000
Amevipiga vita vilivyo vizuri vya imani.

Mwendo ameumaliza, iman ameilinda

Apumzike kwa aman
 

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
2,148
2,000
Poleni sana wana Mbeya. Pole sana familia ya Moravian.

Mchungaji Mpayo hilo jina la kwanza alibadilisha ukubwani??? Kuna yule askofu mstaafu wa KKKT Iringa alipoenda Ujerumani akarudi na jina jipya la Owdenberg Mdegela.
 

CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
7,059
2,000
RIP Mch. Bila shaka umekwenda sababu ya zile changamoto lakini tufanyeje sasa?

Haya yote ni mapenzi ya Mungu, hata majirani wanajua.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom