Mchungaji Msigwa Unatufurahisha sana Wananchi wa Iringa Municipal

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,235
4,949
Kwa miaka takribani 10 iliyopita nilikua sijawahi kusikia sauti ya mbunge wa jimbo langu ikisikika bungeni. Sijutii uamuzi wangu na gharama nilizozitumia kusafiri kutoka Kigoma hadi Iringa kwenda kumpigia kura Mchungaji Peter Msigwa. Wiki iliyopita nimeenda Iringa Municipal nimeshangaa kukuta barabara inayokuja mtaani kwetu ikiwekwa Lami na nilipofika mtaani hadi wale akina mama wa hali ya chini wakizinguliwa kidogo tu na maafisa watendaji wanaandamana kwenda kusemelea kwa mchungaji Msigwa ambaye ndiye mtetezi wao. Kuna wazee wengine maeneo ya Mkimbizi na Kihesa kilolo walidhulumiwa viwanja vyao wakaenda kumwambia mchungaji Msigwa nae amewapigania hadi ardhi yao na haki yao wameipata. Tupo pamoja Mchungaji Msigwa ukitoka bungeni usisahau kuja kuongea na wananchi utupe feedback ya huko mjengoni na usikilize kero zetu. Iringa kwa sasa ni wajanja wamekubali mabadiliko na hili liwe Funzo kwa majimbo mengine yaliyobaki katika mkoa wa Iringa
 
hakufurahishi bali anatetea kile kinachotakiwa kwa maslah ya wana Iringa na Tanzania nzima. Viva rev.Msigwa
 
hakufurahishi bali anatetea kile kinachotakiwa kwa maslah ya wana Iringa na Tanzania nzima. Viva rev.Msigwa

Anatufurahisha kwa jinsi alivyo imara kutetea maslahi ya wana iringa na Tanzania nzima
 
kabila01 amini usiamini hakuna kura ya CDM itakayokwenda bure utafurahia nauli yako uliyochoma kwenda kumpigia kura. no more than CDM in TZ
 
CHADEMA imeleta watu wenye thamani kubwa bungeni ccm imeleta vilaza na wadokozi hadi kwenye mahoteli
 
Kwani webunge wengine sio wajibu wao?? Bg up Msigwa, ni jembe sana, akiongea as if yupo kwenye maombi, magamba yote kimyaaaaaaa, wanamsikiliza!!
 
Big up Rev. Msigwa. Yule mama niniiiii alikuwa hana lolote, alichofanikiwa ni kudidimiza jimbo kwa miaka 10 - RIP Mama MM
 
Mmetumwa nyie. Wakati watu tunatafakari haya maumivu ya kumchagua Msigwa tutayavumilia hadi lini, nyie mnatuletea stori zisizoeleweka. Ni msanii tu hana jipya.
 
hakika iringa mmetuletea jembe bungeni

Njombe igeni mfano sio mmetuletea yule Anaeharibu mambo tu mle mjengoni. na Ndo maana akawaruhusu wananchi wake walime viazi kwenye uwanja wa Ndege
 
ninatamani hayo angefanya huyu jamaa mmoja anajiita Mh James Lembeli (MB) ccm kahama mjini maana kuna vumbi mpaka majengo yamepauka mbaya namshukuru mkapa kwa kuleta maji..
 
viva Chadema! big up sana wabunge wa CHADEMA kazi yenu tunaiona na kuikubari
 
Back
Top Bottom