Mchungaji Msigwa; the best risk decision maker ever! Tumpongeze

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,369
2,000
Wanabodi, Kuna usemi unasema"Your Boss is your Boss, Respect your Boss, Be on positive Side of your Boss. Kwa kiswahili na tafsiri isiyo rasmi ni kwamba "Muheshimi mkubwa wako wa kazi, ongelea mambo mazuri ya bosi wako tu, usimwongelee vibaya mkubwa wako wa kazi

Iringa ya leo hii tukiacha ushabiki na uzandiki imependeza sana hasa manispaa ya Iringa, Iringa mjini anayoongoza msigwa mbunge huwezi fananisha na mikoa mingi hapa Tanzania kwa huduma za msingi yaani Umeme, maji, Miundombinu iliyojengeka

Barabara imara zilizojengwa Mkoa wa Iringa hata katika majiji yetu hakuna, Majiji yetu Mbeya, Dar, Arusha na Mwanza zimejaa miundombimu iliyojengwa kwa kiwango cha chini Sana na mingi inabomoka, Kipindi cha mvua haya majiji yamegeuka uchafu na madimbwi ya kufugia minyoo

Mchungaji Msigwa asingeyaona hayo angekuwa hana heshima wala shukrani kwa Bosi wake, Mkoa wa Iringa umependelewa sana hasa kupelekewa fedha nyingi za Benki ya Dunia (World Bank) na zimetumika kurekebisha mji Sana Sana hilo aliefika kule juu mlimani kwenye mji analijua hilo

Tumpongeza Msigwa, Iringa itakuwepo hata Msigwa akiondoka madarakani, Kupendeza kwa Iringa yawezekana ilipangwa au imetokea kwa bahati mbaya, Kama ni kwa bahati mbaya basi Msigwa historia itamkumbuka sana kama mpigania maendeleo wa Iringa

Wananchi lazima tufahamu maendeleo hayapatikani kwa kumchukia mtu, Wanaomchukia Rais mnapoteza muda na mnajitakia magonjwa ya moyo na presha, Yeye yupo pale kama msimamizi tu na mamlaka kwa mujibu wa katiba

Katika Maisha ya sasa hakuna maamuzi ambayo yapo huru bila kuwa na Risk au tahadhari ndani yake, Tahadhari yaweza ikawa hasi au chanya, Shukrani ya Peter Msigwa kwa Raisi ni chanya kwa wana Iringa lakini ni hasi kwa wenye chuki na Raisi.

Mchungaji msigwa umetumia opportunity kuijenga Iringa iwe chanya ,Usiogope threats (vitisho) kwani opportunity for Iringa To success is greater than threats
 
GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,369
2,000
Tatizo lako hujafika Iringa ya sasa, Iringa hasa manispaa ya Msigwa huduma muhimu serikali imezifanya kwa 100 percent, kuanzia maji, umeme, Afya na barabara

Huwezi linganisha Iringa na mikoa mingi sana, Tuliofika mikoa mingi ina shida Sana ya umeme na maji lakini sio Iringa

Rubbish ni kuendekeza Uchadema na Uccm kwenye mambo ya msingi
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
27,952

Rubbish! Msingi usiokuwa na kujali maisha ya watu ni wendawaqzimu.....wakati Ben saanane amepotea, Azory, Mawazo, etc.....
 
stickvibration

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
3,228
2,000
Alishasema mkuu imebaki iringa tu,kwenda kutoa Dozi ya uhakika ili 2020 Msigwa asahau kurejea mjengoni dodoma
 
GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,369
2,000
Kampeni ya mwaka 2020 Iringa itakuwa watu wanaenda kupiga kura kutimiza wajibu tu, Lakini ishu za msingi walizohitaji Serikali imewapatia

Huwezi ongelea kwenye kampeni ishu za Social service
Msigwa ni hero kwa wana Iringa ila kwa wanaomchukia Rais wanaumia Sana, Raisi sio mkazi wa Iringa hata wabeba chuki hawaishi iringa
 
GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,369
2,000
Rubbish! Msingi usiokuwa na kujali maisha ya watu ni wendawaqzimu.....wakati Ben saanane amepotea, Azory, Mawazo, etc.....
Kupotea kwa hao yaweza ikawa ni chuki na wapenzi wao, Umefanya utafiti ukajua chanzo cha hao Kupotea?

Kuna mambo mengi nyuma ya hii dunia mkuu, Hakuna anayejua maisha ya hao waliopotea yawezekana walidhulumiana kwenye biashara zao na rafiki?
 
Nyanya mbichi

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
3,692
2,000
Rubbish! Msingi usiokuwa na kujali maisha ya watu ni wendawaqzimu.....wakati Ben saanane amepotea, Azory, Mawazo, etc.....

Mkuu sometimes tunawaonea bure hawa wanasiasa wanapigana sana wanapata mateso sana
sisi kazi yetu kuwalaumu tu kwa makosa madogo
utasikia "wanasiasa wa upinzani wa sasa wabadili aina ya Siasa wanazozifanya" walipigwa ndani pasaka yote wakati mwingine hawalali makwao kuhofia usalama wao.
Lissu alitoa tahadhari kuna watu wananifuatilia tukakaa kimyaa,kuna wengine hata michango hafujamchangia

Mange kahamasisha maandamano watu wamembeza
oooh wewe uko nje huko mara hivi njoo bongo tuandamane ukae wewe mbele.
Mdada wa watu amevunjika Moyo sana

watu wakakaa majumbani kimyaaa
siku ya maandamano imepita comments kibao wanataka "ubuyu" nani kamuua Masogange
upuuz upuuzi tu
Mbowe yuko kwenye hardtime watu wanachukulia poa tu
natamani siku moja hawa wanaotupigania walioko nje ya Ccm wangekaa kimya wakafanya shughuli zao nyingine hata kwa miaka 3 tu akili ingetukaa sawa
 
713

Senior Member
Apr 1, 2018
126
250
Siasa ni mchezo wa faida siasa ni ajira ila upinzani wa kweli bado sana naona makanjanja tu wafia tumbo tu ikifika 2020 Wa Tanzania wataelewa vzuri
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
27,952
2,000
Mkuu sometimes tunawaonea bure hawa wanasiasa wanapigana sana wanapata mateso sana
sisi kazi yetu kuwalaumu tu kwa makosa madogo
utasikia "wanasiasa wa upinzani wa sasa wabadili aina ya Siasa wanazozifanya" walipigwa ndani pasaka yote wakati mwingine hawalali makwao kuhofia usalama wao.
Lissu alitoa tahadhari kuna watu wananifuatilia tukakaa kimyaa,kuna wengine hata michango hafujamchangia

Mange kahamasisha maandamano watu wamembeza
oooh wewe uko nje huko mara hivi njoo bongo tuandamane ukae wewe mbele.
Mdada wa watu amevunjika Moyo sana

watu wakakaa majumbani kimyaaa
siku ya maandamano imepita comments kibao wanataka "ubuyu" nani kamuua Masogange
upuuz upuuzi tu
Mbowe yuko kwenye hardtime watu wanachukulia poa tu
natamani siku moja hawa wanaotupigania walioko nje ya Ccm wangekaa kimya wakafanya shughuli zao nyingine hata kwa miaka 3 tu akili ingetukaa sawa
Nakubaliana na wewe sana. Wanatupigania/wanapigania haki sana. Hili kateleza na kuna mahali nimesema kuwa mimi namuamini sana tena sana Msigwa, kwa hili kateleza kidog. Hatuwezi kumhukumu kwa hili dogo, ila kusema ni lazima lisirudiwe tena!
 
ofisa

JF-Expert Member
May 15, 2011
2,840
2,000
Nilijua atakuwa mpole maana JPM anajua pesa ya jimbo mil 50 zimeshatolewa kwa wabunge na angeweza kumchallenge kama alivyofanya kwa yule wa kilolo.wapo Karibu na chanzo cha maji halafu JPM akakadiria sh 5 mil zingetosha kufunga water pump na kuyaleta kijijini.
Kwa kifupi ,Nae msigwa ameogopa ku challengiwa na JPM kuhusu pesa ya jimbo.Pesa ambazo kwa wabunge wao ni siri sana ila JPM huwaumbua kama wamepewa na wananchi wajue kuwa pesa ya maendeleo ya jimbo anayo mbunge wao.
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,920
2,000
Mchungaji Msigwa kaongea kiujanja sana . But he hasn’t conceded anything. BAHATI mbaya wengi hawakumuelewa

Yeye Mwenyewe kakiri Kwa ku tweet kuwa kakosea Kwa falsafa ya Chadema kutosifia Serikal Halafu Wewe unaleta Nahau zako
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom