Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Lazima heshima iwepo kwa viongozi wa serikali vipi kuhusu viongozi wa dini wao hawastahili heshima


Dini ya kishetani ya Gwajima? He is fake pastor, and he earns monies thru uchawi tu, jizi sana hili, this time on, lazima ajute mhuni huyu, kavunja ndoa ya Emanuel Mbasha na Flora Mbasha, sbb alikuwa mchungaji feki huyu ana fanya ngono, huyu akajidai atamfufua Amina Chifupa, jizi sana hili...

Ni kumfungia kanisa feki akome kabisa.. aaaarrghh
 
Salaam humu, nina hasira sana na Gwajima...

Laiti, mm ningekuwa RC Makonda, saa hizi Gwajima angekuwa maabusu and behind unknown bars..

Serikali, kamateni huyu mchungaji feki, mmemlea sana, kaota mapembe, akijua yuko juu ya state.. Iweje Gwajima, anamchafua Mkuu wa Mkoa, Makonda kwa kiwango hiki, na asikamatwe? With immediate action, kamateni mhuni mchungaji feki, iwe funzo la milele..

HATUWEZI kuwa na mchungaji mhuni mhuni kuchafua viongozi wa serikali kutumia kanisa lake . I wish ningekuwa RC Makonda, sitanii, Gwajima ungejuta, kamata huyu mhuni haraka.. Aaaaarrghh

Haiwezekaniki mchungaji feki huyo kumchafua RC kiasi hiki, no way, no how, not acceptable, lazima lazima heshima iwepo kwa viongozi wa serikali ikibidi kwa lazima, Who is Gwajima? Mandate ya kuchafua kiongozi wa serikali anapata wapi? I was offline for 2 weeks, namuona Gwajima anaachiwa kucheza hovyo, piga ndani huyu mhuni mkubwa, ww Gwajima ww, jua wazi hauko juu ya serikali, na serikali inakujua ww kuliko unavyojijua, acha ujinga mara moja.. Aaaarrghh
Sawa mama Bashite tumekusikia
 
Njaaa zako zitakuuuaa...bashite alete vyeti hicho tu... Akuanzae mmalize tulifundishwa hivyo..bashite alisema mwenzie anauza dawa...mwenzie kajibu bashite kanunua vyeti....bashite kasepa no vyeti no nn..
Big up askofu
Huyo siyo askofu bro trust me. Alipewa na nani kwani. Alijipachika mwenyewe kama ambavyo na wewe unaweza kujiita askofu kuanzia leo
 
Huyu mchungaji ni mnafiki na mchonganishi hatofanikiwa ila kwa wajinga wenzie tu hana maana katika jamii kiongozi unakua na element za umbea umbea
 
Kumuweka ndani sio wazo zuri, ni kuonyesha uoga.

Njia nzuri na ya KIUME kumjibu mtu anayekuita mchovu, umefulia, omba omba n.k ni siku moja unapaki JAGUAR LAND ROVER mpya miguuni kwake, unashusha kioo, unamsalimia, unampatia kopi ya kadi ya gari, unapandisha kioo unaondoka.

Akiendelea kupayuka basi unaachana naye tu kwani sasa utakuwa unashindana na Mgonjwa.
 
Mkuu acha hasira za kipumbavu,huwezi kuongoza watu huku ukiwa na hasira na Watu unaowaongoza,Gwajima anataka kuthibitisha kuwa mkuu wa mkoa amefoji vyeti kwa kuonyesha ushahidi wa wazi,Na makonda athibitishe kuwa Gwajima anatumia au anauza Madawa kwa wazi,Tuache siasa za maji taka.
 
Ukweli ni kwamba Gwajima anaweza kuwa sawa kwenye vidato vya chini. Makonda amesoma vyuo vyote mpaka chuo kikuu kwani unaweza kusema makonda hana elimu? Hata kama cheti cha fomu four si chake but jamaa kajitahidi kuparangana. Hii inaonyesha kuwa jamaa alikuwa na maono na malengo na maisha yake. Kwanza anahitaji kupongezwa kwa juhudi sake za kujiendeleza. Big up makonda.
Naomba mbadilishe kauli mseme hivi kwa mujibu wa Gwajima,, MAKONDA ANA JINA FEKI LAKINI SIYO ELIMU FEKI NA VYETI FEKI. ASANTENI
 
Nenda UDSM kaulizie; Hii ya Gwajima ni fake from the fake fakes! Kibaya zaidi ni mtu wa Mungu kuendelea kujiita DR. Wakati Taasisi iliyompa hiyo " Honorary PHD" Haitambuliki popote! Mamlaka zote za Afrika Kusini Haziitambui hiyo Taasisi Feki.


Mwambie Daudi Bashite aonyeshe cheti chake cha kuzaliwa na cha form four. Mnapishana sana viunga vya Lumumba hutopata shida kumpata.

Tuhuma hujibiwa sio kukaa kimya au kuanza kumsingizia Mungu... Mwambie Kabisa hatuna shida na dv ziro yake tunachotaka ni akanushe tuhuma za kujiendeleza kielimu kwa kutumia cheti cha mtu tena kwa evidence.

Haya haya ya sijui PhD feki ya Gwajima wala hayana mashiko ile ni PhD ya hesima tu.
 
Mukitenda kwa haki haya yote yasingejitokeza,mkiacha haki mkafanya ya kwenu mambo yenu yote machafu yatawekwa hadharani.
 
Gwajima mpuuzi sana, naamini serikali imesikia, na itambana mapvmbv jinga hili
 
Umechambua hoja vizuri sana bwana mayalla ila najiuliza kwann utafiti wako umeegemea upandw mmoja?
Hoja ya upande mmoja imeeleweka kwa kueleza baadhi ya sababu lakini kwann upande wa pili umeleta hoja isiyokuwa na maelezo ya kutosha kama ilivyo iyo nyingine.??
Napata ukakasi hapo....
Unafanya hivyo kwa maslahi yapi Mayalla??
Lete ushahidi ya hiyo hoja yako sio kusisitiza na kutoa general information bila kuleta ufafanuzi wake..
 
Pascal Mayala haeleweki, ila nae atuambie alikopitia elimu yake mpaka anapata digrii. Make mimi Mayala nimeanza kumsikia anaandika habari wakati hana digrii.......sasa atuambie alikuwa mwandishi vipi wakati hana digrii......na ameipataje digrii yake hapo baadae. Hizi elimu za kuunga zina shida sana.
Nadhani atajibu hii asikute naye alibashite, Pasco njoo huku ujibu hizi tuhuma
 
Wanabodi,
Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.

Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.

Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa, ndivyo Bwana Yesu alivyofundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kushoto mgeuzie na la kuume. Adui mpende. Samehe saba mara sabini. Vipi kuhusu Baba Mchungaji Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo? .

Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Mchungaji Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.

Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma unga kwa Mchungaji hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.
Paskali
Jumatatu Njema.
Paskali
Imani na sheria ni vitu viwili tofauti sana. Kama yeye kwenye Imani yake anaamini ni cheo kikubwa zaidi ya urais why wewe uone kasema uongo? Mind you hajasema kikatiba yeye ni zaidi ya rais, but he meant is at peace with what is doing
 
Kuhusu mchungaji Gwajima kuwa au kutokuwa mtumishi wa Mungu kwangu Sina comment ila kuhusu mchungaji kuwa mkubwa kuliko raisi hilo lipo wazi na kwa sababu umetumia neno la Mungu kusimamia hoja yako kadhalika name nitakujibu kwa kutumia neno la Mungu, inategemea mtazamo wako mfano raisi huwekwa na wanadamu (huchaguliwa na watu)uchungaji ni wito (huitwa/huwekwa) Na MUNGU sasa hapa tukiangalia kwa mtazamo huo mchungaji ni mkubwa kuliko rais kutokana na mamlaka ilomuweka.Kuhusu kusamehe ni kweli imeandikwa samehe saba Mara sabini ila biblia inatupa wajibu wa kuonyana inapolazimu kulingana na mazingira Bwana wetu Yesu alipowakuta wafanyabiashara hekaluni aliwafukuza na kuwachapa na hata meza za biashara aliimwaga. Hapo Bwana Yesu angewasamehe na kuwaacha wangeendelea na biashara pale kitu ambacho hakikutakiwa. Hivyo mara zote tuelewe muktadha wa maandiko badala ya kuyatumia kujihesabia haki/au kujudge we go wengine.
 
Back
Top Bottom