Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Wanabodi,

Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?, Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji Gwajima Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!. Akiwa katika mimbari, madhabahuni, badala ya kuhubiri neno la Mungu lenye kujenga upendo, yeye anahubiri siasa za chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "kiumbe".

Isikilize Clip hii Akisema Uongo Madhabauni, tena mchana kweupe. Mara baada ya Mashekh wa Mkoa wa Dar es Salaam, kumuombea dua, Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mchungaji Gwajima, amemuonea vivu kuwa dua zile zitazidi kumnyooshea mambo yake, hivyo ili kumbomoa, Mchungaji Gwajima, mwenye utajiri wa ajabu (Hammer, Helcopter, na kanisa kubwa), akaamua kuhubiri mahubiri ya kusingizia, kwa kumsingizia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kuwa ni mhalifu wa kosa la jina la kuiba jina la mtu mwingine, na kosa la kughushi kwa vyeti, kwa kudai kuwa eti jina halisi la Paul Makonda, sii jina lake, ni jina la mtu mwingine, Makonda jina lake halisi ni Daudi Albert Bashite!, na hakuishia hapo, amedai Yeye nini Zaidi ya Rais, kugombea urais ni demotion!. Hivi kwa mtumishi wa Mungu wa kweli, anaweza kusema maneno kama haya madhabahuni kwa Mungu, au Mchungaji huyu, ni wale Manabii wa Uongo, Bwana wetu Yesu Kristu aliotuhusia?.

Msikiliza Mchungaji Gwajima.


Nimeisikiliza hii clip hii ya Mchungaji Gwajima, akimzungumzia Daudi Albert Bashite, A.K.A Paul Christian Makonda, akidai kuwa kilichomponza yeye Mchungaji Gwajima hadi kusingiziwa madawa ya kulevya, ni dhana kuwa anataka kugombea ubunge jimbo la Misungwi, kufuatia kutua kijiji Kolomije kwa Chopa, (Helcopter), hivyo Daudi Bashite, A.K.A Paul Manajipanga kugombea jimbo hilo mwaka 2020!. Mchungaji Gwajima akajitapa Ubunge, Uwaziri hadi Urais kwa Mtumishi wa Mungu aliye hai ni demotion!. "Mtumishi wa Mungu ni zaidi ya Rais wa nchi!". Jee hii ni kweli?.

Akielezea kuhusu Daudi Albert Bashite, na yeye Mchungaji Gwajima, ni watu wa kabila moja na wametokea kijiji kimoja cha Kolomije. Daudi Bashite alisoma Shule Msingi ya Kolomije hadi darasa la tano, akahamia Shule ya Msingi ya Nyanza hadi akamaliza Darasa la 7, hakuchaguliwa. Akajiunga na Shule ya Sekondari Pamba, akiwa anakaa kwa mama Kamese (Gwajima ana simu yake) ambako alipata Divisheni 0, ndipo dada mmoja wa Kihaya kwa jina la Christina (Gwajima ana simu yake) akamuunganishia Daudi Albert Bashite, kwa mdogo wake, Paul Christian, hivyo Daudi Bashite akaanza kutumia cheti cha kaka yake Paul Christian ndipo akajiunga Nyegezi kusomea certificate ya uvuvi kwa jina la Paul Christian Makonda, kisha akajiunga Chuo cha Mbegani Bagamoyo kuchukua diploma ya uvuvi na kumalizia Chuo cha Ushirika kuchukua degree kwa majina ya kughushi ya Paul Christian.

Katika kumuelezea Daudi Bashite, Mchungaji Gwajima amemuita "kiumbe huyu", hili sio neno zuri kwa kiongozi wa dini ya Mungu kweli, kumuita binadamu mwenzako kiumbe!.

Ila pia Mchungaji Gwajima amedai, anavyo vyeti vyote ofisini kwake tangu cha Daudi Albert Bashite alichopata Divisheni 0. hadi cheti cha Paul Christian alichounganishiwa na Christina!, na kudai kuwa ana mshitaki Makonda kwa Ndalichako na kwa Magufuli, na asipochukuliwa hatua zozote, yeye atashangaa sana na atavitoa vyeti hivyo hadharani, umma uvione.

Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Huyu ni mchungaji wa Mungu au mungu. Hili la kudai anavyo vyeti vya Daudi Bashite na Paul Christian, Jee hii inaweza kuwa kweli?!. Nijuavyo mimi, mtu ulikuwa ukipata Div. 0 hupewi cheti chochote na NECTA zaidi ya Leaving Certificate, sasa hicho cheti cha Daudi Bashite alichonacho Mchungaji Gwajima, kimetoka wapi?. Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo madhabahuni, jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu, au ndio hawa wachungaji wanaomtumikia mungu?!.

Jumatatu Njema.
Paskali

siku hizi mayala una hoja nyepesi sana.
vip unaonaje ukipumzika ili uweze kujifunza biblia.
HIVI YESU AKIKAA NDANI YAKO NA WEWE NDANI YAKE .
Kwahiyo unakuwa mkubwa kuliko raisi au mdogo????
KATIKA ULIMWENGU WA ROHO SISI NI WAFALME PAMOJA NA YESU.
NA YESU NDIYE ALPHA NA OMEGA .
UFUNUO 1:1-10
 
Mtumishi wa Mungu ni yule anayeona uovu na kuukemea si kupaka mafuta ya uongo.. Kemea uovu watu wapate kupona...

Elewa pia panapotoa moshi sana jua pana jambo. Kwa hiyo wenye mamlaka waliangalie hili nalo likae sawa isijeonekana kuna double standard katikavuongozi
 
Kumtumikia mungu ni jambo kubwa kuliko kitu chochote. Maandiko yanasema mtu akinitumikia Baba yangu atamuheshimu. Sasa kama unafikiri kuheshimiwa na Mungu ni jambo dogo jaribu ujinga.
 
Gwajima angejiekeleza kuhuburi injili kuliko kuingia vita binafsi na wanasiasa.

Kiburi cha pesa kinazidi kumjaa gwajima...
 
Hajasema ana matokeo, amesema ana vyeti mezani kwake, hivi kweli kuna cheti cha divisheni 0 ya miaka hiyo?.

Paskali
Mayalla, rais gani unaweza kumfananisha na mfalme suleman,rais gani unamfananisha na daud,petro,yohana,abel? Aliposema ni demotion hakukosea angalia petro alikuwa nani,daud alikuwa nani. Kutumia neno kiumbe hakukosea au sababu ni jamaa yako. Wanadamu wote ni viumbe. Mbona mnapenda kujitukuza sana?
 
Mtumishi wa Mungu ni yule anayeona uovu na kuukemea si kupaka mafuta ya uongo.. Kemea uovu watu wapate kupona...

Elewa pia panapotoa moshi sana jua pana jambo. Kwa hiyo wenye mamlaka waliangalie hili nalo likae sawa isijeonekana kuna double standard katikavuongozi
Bwana Yesu mwenyewe alizibinua meza za wachuuzi hekaluni. Hakucheka na waovu...aliwaita majina mabaya....kizazi cha nyoka, wapumbavu n.k. Leo hii eti mtu anajiita mtumishi wa Mungu halafu anakuwa mnafiki kisa kuwapendeza watawala!
 
Hivi hili suala linautofauti gani na lile la mkurugenzi wa Itigi/Singida ndugu Luhende Pius George?! Mbona serikali ilikanusha nakumbuka hadi siku ya kuapishwa mkuu alisema waandishi wapige picha cheti cha huyu jamaa!

Hili suala mwisho wake ni mdogo sana! Kama unajiamini uko sawa na una vyeti sahii haijalishi umepata ngapi maana wote hatuwezi kuwa sawa darasani jitokeze na sema ukweli!

Kosa si ulipata daraja gani darasani kosa ni kama kwel unatumia cheti cha mtu! RC au mamlaka husiku wajitokeze kutolea ufafanuzi kama suala la mkurugenzi wa Itigi lilivyotolewa ufafanuzi maana na lenyewe lilianzia huku huku kwenye mitandao!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom