Yiyu Sheping
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 1,720
- 850
Hivi unafahamu kuwa katika muda huu kuna majaji wanne, wapo kazini, huku wawili wakikabiliwa na tuhuma za kuwasaidia wauza unga na wawili wakiwa miongoni mwa waliopokea mgao wa Tegeta Escrow? Ukidhafahamu hilo huenda ukaanza kuwekeza nguvu zako katika masuala ya maendeleo yako binafsi kuliko kujipa matumaini hewa kuhusu "kutumbuliwa kwa Makonda."
Watanzania ni viumbe wa ajabu sana. Wamesahau kabisa kuwa mtu mmoja aitwaye Masauni, alilazimika kung'oka huko UVCCM kwa tuhuma za forgery/udanganyifu. Guess leo ni nani serikalini?
Prof Muhongo ni miongoni wa watu waliohusishwa na kunufaika na skandali ya Escrow. Leo ni nani?
Wale jamaa wa GSM, sote twajua walioyafanya na hatimaye "kujifilisi" only to come back with another name. Ungejua Home Shopping Centre "ilifilisika" huku inadaiwa kiasi gani, yet ni "wadau muhimu wa maendeleo kwa Awamu ya Tano" basi huenda usingepoteza muda wako kutarajia kuona "Makonda akitumbuliwa."
Tunawalipa IPTL sh milioni 400+ KILA KUKICHA ilhali sote twafahamu kuhusu hali ya Tanesco na kushamiri kwa mgao wa umeme. Talking about mgao, umeshadumu kwa miaka mingapi, na nani kawajibishwa so far "solely kwa kuchangia kudumu uwepo wa mgao wa umeme"?
Endeleeni kutarajia miujiza. Ni haki yenu kikatiba anyway!
.....Itakuwa kweli mbona yupo kimya, silent means yes
Swali lilipaswa kuwa tangu "sakata la Kihiyo 1996" hadi leo, ni wangapi waliokwishatumbuliwa kuhusu kufoji elimu?Wee jamaa mfatiliaji mzuri wa masuala na mtunzaji kumbukumbu mzuri!!! Katika kumbukumbu zako yule Kihiyo yuko wapi? Tafadhali.
Na washawasha!
Swali lilipaswa kuwa tangu "sakata la Kihiyo 1996" hadi leo, ni wangapi waliokwishatumbuliwa kuhusu kufoji elimu?
Na pengine swali la msingi zaidi ni "kwanini Kihiyo na sio kina 'Dokta' Nchimbi?"
Wanaofahamu undani wa sakata la Kihiyo watakufahamisha kuwa huyo ubunge wake haukutumbuliwa kwa sababu za kufoji elimu bali "mengineyo." Naliona suala la Makonda likimalizika kwa staili hiyo: kama ni kutumbuliwa sio kwa vile ni Bashite bali "endapo atamtibua mkulu."
.....Mchungaji Dr.Josephat Gwajima, leo kanisani kwake mbele ya umati wa waumini akiwaita wanafamilia wake, ametoa maelezo yakinifu juu ya tuhuma zinazomkabili ndg. Paul Makonda na katika clip inayosambaa kwa kasi mitandaoni.
Askofu Gwajima amedai anaoushahidi wa kutosha kua ndg. Makonda alitumia vyeti visivyo vyake.
Katika clip hiyo mchungaji Gwajima amesema ana vyeti vinavyotoa ushahidi kua Makonda alitumia vyeti vya mtu mwingine.
Swali: Je, Rais atamwacha Makonda na kulifumbia macho hilo suala?
=======
PAUL MAKONDA:
1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.
2. Majina yake halisi ni Daudi Albert Bashite
3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije akitumia majina ya Daudi Albert Bashite. Mwaka 1991 alifeli darasa la 4, akarudia.
4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).
5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.
6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Pamba.
7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero).
8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002.
9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005.
10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg. Benjamin Sitta (mtoto wa Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Meya wa Kinondoni kwa sasa). Wakawa marafiki.
11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yake ya uvuvi, aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada lakini akakosa nafasi.
12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta). Kwakuwa alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha elimu ya juu.
13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani).
14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management & Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati ya Course 8 alizokuwa akisoma (akawa discontinued).
15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission upya. Akamaliza first year akiwa na carries 3 ambazo alienda nazo 2nd year. Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya course 8 alizokua akisoma. Akawa na mzigo wa carry over na supplementary. Akaamua kuacha chuo.
16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.
17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya. Akaachana na CMA akachagua Community & Economic Development (CED).
18. Mwaka 20012 akahitimu shahada ya kwanza ya Community & Economic Development kwa jina la Paul C Makonda badala ya majina yake halisi ya Daudi Albert Bashite
19. Jina Makonda analitumia baada ya kula kiapo mahakamani kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka Paul C Muyenge lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C Makonda baada ya kuapa mahakamani.
20. Ndugu Daudi Albert Bashite ameoa (tangu mwaka 2009) lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa.
Swali lilipaswa kuwa tangu "sakata la Kihiyo 1996" hadi leo, ni wangapi waliokwishatumbuliwa kuhusu kufoji elimu?
Na pengine swali la msingi zaidi ni "kwanini Kihiyo na sio kina 'Dokta' Nchimbi?"
Wanaofahamu undani wa sakata la Kihiyo watakufahamisha kuwa huyo ubunge wake haukutumbuliwa kwa sababu za kufoji elimu bali "mengineyo." Naliona suala la Makonda likimalizika kwa staili hiyo: kama ni kutumbuliwa sio kwa vile ni Bashite bali "endapo atamtibua mkulu."
Ndio hapo mnapokosea: kudhani hisia/hasira zenu ndizo alizonazo aliyemteua.Hivi kumtibua ni mpaka afanye nini hasa? Maana kama hizi tuhuma ni za kweli tayari kesha muabisha na kumfedhehesha kwa anao watawala. Na hii kwa awamu ya nne na ya tano. Hili jambo kwa sasa laweza kupuuzwa lakini upande ule wa pili watakapo anza kupanda majukwaani ndio madhara ya hili yatakapo jidhihirisha.
Na washawasha!
hivi kwa kawaida maadhimisho kama hayo mgeni rasmi huwa anatangazwa na taasisi gani?Ya kwamba mchezo ulipangwa aende sandton Jo burg halafu kesho ashindwe kutokea kama mgeni rasmi kwenye siku ya wanawake duniani iwe imepatikana sababu ya kumtumbua
isije ikaonekana alitolewa sababu ya forgery...tusubiri kesho then tutatona
unahaha kama ngolo kante,kila nyuzi ya bashite wa kolomije unaingia kuijambia...kolooomije kollloooooomije,nawaona nawaona mnakula tu ubuyu...fa fa fa fa afa fa afafafafafafafafaaaaaaa laaaaaaaaaUmekaa umemuwazaaaaaa, usingizi umekata huyoooo unataka tu kumuandika. Vipeeee ufuasi wa waliowavuta imekuwaje bado mnadanganyika?
Teeh teeh.Hivi walio mualika nao wako na matatizo gani!!?
Maana jamaa hana credibility hata ya kuhudhuria sherehe za kumaloza shule ya msingi kwa sasa