Mchungaji Anyeshewa Mvua ya Miaka SIta Jela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji Anyeshewa Mvua ya Miaka SIta Jela

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Lekanjobe Kubinika, Jun 7, 2011.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Source: Wapo FM - YALITYOTOKEA

  Mchungaji na pia Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Pomelini wilayani Kilolo kwa Wanyalukolo mkoani Iringa, amezawadiwa mvua hiyo na Hakimu moja mkoani humo jana baada ya kuridhika pasipo mawaa, na baada ya mtuhumiwa kukiri kusema "Ndisuka" takrima ya ngono na "kujaribu" kumbaka mwanafunzi wake wa kidato cha pili aliyekuwa akimfundisha shuleni hapo.

  Akisomewa hukumu hiyo, Mchungaji huyo wa KKKT aliambiwa kwamba August 28 2010 aliomba rushwa ya ngono kwa binti ambaye pia ni yatima ili amsaidie kumpa tuition ya nguvu yenye tija kwa maisha yake ya baadaye. Inadaiwa baada ya kulilia sana bidhaa hiyo, binti aliomba kibali kwa mjomba wake ambaye akamsaidia kwa kuweka mtego kama wa panya uliofanikiwa kumnasa kabla hajala karanga aliyotegeshewa. Mchungaji hakuwa na sababu ya kukataa mbele ya mahakama, lakini aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa sababu alikuwa na nia njema sana kwa kumsaidia binti huyo.


  Hakimu akimsomea mchungaji vifungu vya msahafu wa sheria za nchi, alimwambia mchungaji kwamba anamtia hatiani kwa makosa mawili kama ifuatavyo kulingana na kifungu Nambari 25 cha sheria ya mwaka 2007:
  1. Kuomba rushwa (sio lazima ya ngono, kuomba tu) - adhabu ni Laki Tano au kifungo miaka sita jela. mchungaji wala ndugu na marafiki zake hawakuwa na mahela hapo.
  2. Kutaka kubaka (sio tu mwanafunzi, dhamira tu) - adhabu Miaka 5 jela bila fine.
  Ndugu za Mchungaji badala ya kuchangishana pesa wao waliangua vilio kama vile wamefiwa, naye mchungaji akajikuta anabeba debe sita za miaka ya jela tangu jana hiyo hiyo.

  Sasa watu waligawanyika katika maoni yao, wengine wakisema mshahara wa dhambi ni mauti na apewe haki yake, na wengine wakimhurumia kwa vile yeye naye ni binadamu mwenye hisia na rijari kama mwanaume mwingine, kwamba ni vitu vya kawaida kutokea na isitoshe aliomba tu na kwa kuwa unyalukoloni kuna msemo wa "niangusage tu sambi ni sako mwenyewe" akadhani amekubaliwa naye akajaribu kuangusa kumbe kachomekewa na kunasa. Wachungaji wengine walituma sms redioni wakisema mchungaji amewavua nguo wachungaji wenzake. Lakini ilimradi kila mtu alisema anavyojisikia, mchungaji akawaacha kwenye mataa na kutinga zake jela kuanza kazi ya kupeleka huduma ya kichungaji kule jela kwa mbwembwe.

  My take: Huwezi kujua, huenda kule jela anapelekwa kufanya utumishi mzito kwa kuwapelekea injili wafungwa ambao bila njia hiyo ingekuwa vigumu kuwapata. Binadamu tunapenda sana kunyoosha kidole kwa wengine tukijisahau kwamba nasie twafanya hayo hayo. Ndio maana Msahafu unatuhabarisha kwamba Yesu Kristo aliwaambia wale wayahudi waliompelekea mwanamke (wakamficha mwanaume) aliyefumaniwa kwamba torati inawaagiza apigwe mawe hadi kufa. Naye akawaambia asiye na dhambi na awe wa kwanza kurusha jiwe. Huku akiandika chini dhambi ya kila mmoja wao mioyoni mwao akaingia mitini mmoja mmoja baada ya kuonyeshwa uovu wake hadi wote wakaisha. Naye Yesu akamuuliza mwanamke yule, wako wapi washitaki wako? Nenda zako na usitende dhambi tena.

  Mtu yeyote anaweza kutegeshewa. Mwanamke sio wa kubishana naye saaana, maana silaha ya ngono wanapenda sana kuitumia wakiamua ama kukukomolea au kufanikisha mambo yao. Ila tumefichwa kujua mambo yanayotufuata dakika ijayo, ndio maana tunamhitaji Mungu kwa sana katika maisha yetu.
   
 2. jockey emmanuel

  jockey emmanuel JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 330
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  surely,thnx kwa kunifungua macho...wat if through his presence in dat jail ppo are gonna b saved?
   
 3. SexaMicca

  SexaMicca Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  niliiona hii...
  mwache akutumikie makosa yake anastahili alichokipata
   
Loading...