Mchungaji Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' awaombea kifo waandishi wa habari

"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. "
Bado waamini wake wataenda kusikiliza mahubiri yake huyu mchungaji uchwara?
 
Baba Mchungaji ikiwa kweli alikunywa na akawatukana jirani zake, atubu kwa Mungu atamsamehe na yeye atajirekebisha badala ya kuwajibu watu kwa jinsi hiyo ya kuwalaani na kuwatakia kifo. Maandiko yanasema bariki wanaokuudhi usiwalaani.
Hujaona video mkuu?
 
hahaaa hakuwa na hangover wakati anatoa hii kauli?
Hapa ndo huwa naona jamii ya kiafrika uelewa wetu ni mdogo sana. Ona huyu msanii anayoyaongea lakini utaona watu wanaendelea kumwamini na kutoa pesa zao. Mimi nasema sisi waafrika bado hatujafikia level ya ubinadamu bado ni wanyama ni a bit advanced tu. Hainiingii akilini mtu kama huyu bado anaendelea kuaminiwa. ni shida
 
2 kings 2:23-24 vijana walimdhiaki Elisha ,Elisha akawalaani dubu wawili wakajitokeza wakawararua na kufa .Niwakati muafaka wa kupima kama Lusekelo ana mtangaza Mungu alie hai kwa vifo vya wadhiaki wake .Hiki ni kipimo tosha kama Elia na manabii wa baali
 
2 kings 2:23-24 vijana waliomdhiaki Elisha ,akawalaani dubu wawili wakajitokeza wakawararua na kufa .Niwakati muafaka wa kupima kama Lusekelo ana mtangaza Mungu alie hai kwa vifo vya wadhiaki wake .hiki ni kipimo tosha kama Elia na manabii wa baali
Sasa tuna agano jipya Jesus mwenyewe alisema samehe saba mara sabini siyo kuwaombea watu wafe! Angekuwa kaandikwa kwa uzushi hapo sawa lakini alilewa watu wasiseme sasa!!!!
 
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako jana amesema waandishi wote wa habari wanaoandika habari za kumchafua, watakufa kabla ya kufika Machi 2017.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa.

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya, ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mko humu mmekuja na mnasikiliza tu,”alisema.

“Akisema Mungu uishi wewe basi, nakuwa sina namna, lakini sijawahi kumtumikia Mungu ambaye ananyamaza. Nilishakubaliana mimi na Mungu, mpango wa Mungu ndiyo mpango wangu, sasa wajiandae, mimi siyo Sheikh Yahaya, mmeingia choo cha kike, nasema ‘Mama yangu mzazi’ nitaacha kuhubiri, nitaacha kuhubiri ….mimi nina nguvu saaana,”alisema.

Hata hivyo baadaye mchungaji huo alishuka na kusema anamuachia Mungu wake ambaye atawahukumu kwa wakati wake.

“Lakini Mungu anasema tusihukumu, namuachia Mungu atawahukumu kwa wakati wake, haleluya, haleluya, Mungu awabariki sana."

Novemba 24, mitandao ya kijamii ilikuwa na picha zinazomuonyesha Mzee wa Upako akirushiana maneno makali na jirani huyo ambaye anasikika sauti.

Taarifa za kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kiroho zilisambaa baada ya mwandishi wa habari, Happiness Katabazi aliyeshuhudia tukio hilo, kuandika kwa urefu kisa hicho na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Novemba 26, Mzee wa Upako kwa mara ya kwanza alisita kuzungumzia sakata hilo na badala yake akasema wanaomtuhumu waendelee kusema: “Sisemi, lakini siogopi kwenda jela mimi na kwa taarifa yao watashindana sana, lakini hawatashinda. Hii ni kama kumpiga chura teke.”

Novemba 28, pia Mchungaji huyo akajibu akisema maneno aliyotumia ambayo ni mshenzi, mpumbavu na mjinga siyo matusi kwani yameandikwa kwenye biblia na kwamba watu hao ndiyo walianza kumtukana yeye baada ya kuwauliza wanatafuta nini eneo la getini kwake.

Jana, mchungaji huyo aliwahakikishia waumini wake akisema waandishi walioandika kwa lengo la kumchafua watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.

Katika mahubiri yake yaliyojengwa na msingi wa Biblia kutoka kitabu cha Samweli wa kwanza, sura ya 16, mstari wa saba, Mzee wa Upako aliyekaribishwa kwa nyimbo kadhaa ikiwamo ‘kusanya kusanya’ alisema yeye siyo mchungaji anayejikweza, lakini baadhi ya wachungaji wakubwa kutoka nje wamekuwa wakienda kuomba upako.

Pia, alisema hata Rais John Magufuli hakumuita yeye bali aliona kitu ndani yake na kubarikiwa kabla ya kumtembelea.

Chanzo: Malunde1
 
Attachments

  • 15349747_10154817041594339_2659213238415870321_n.jpg
    15349747_10154817041594339_2659213238415870321_n.jpg
    19.4 KB · Views: 39
Imani ni hatari!

Halafu waumini kama kawaida wakamwaga haleluya za kutosha!
 
We have been there. Watu wanaoombea wenzao kufa wao ndiyo hutangulia kwanza. Mchungaji achunge kauli zake!
 
huyu nae akamatwe kwa kutishia kuua,maono na mafundisho ya namna hii havipaswi kufumbiwa macho vinaweza kuchochea watu kuuana kwa kisingizio cha maono toka kwa Mungu,hata Manabii na Mitume wa M/Mungu hawakuota ndoto za kipuuzi kama hizi wanazoota watu siku hizi
 
Anatumia biblia gani kuhubiri.. Biblia inasema;

"..msilaani, barikini.."

"..barikini wanaowachukia, waombeeni wanaowaudhi.."

"..mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie na la kushoto.."

"..Nijaponena kwa lugha za wanadamu na malaika, kama sina upendo ni sawa na upepo uvumao! tena nijapokuwa na kipawa cha unabii na imani ya kuhamisha milima, kama sina upendo mimi si kitu. Tena nikitoa mali zangu zote kulisha masikini, au nitoe mwili wangu niungue kama sina upendo hainifaidii kitu ......... Upendo huvumilia, upendo hauna majivuno, upendo hauna kiburi, upendo haukasiriki, upendo hauhesabu mabaya........ Upendo huvumilia yote....... Upendo hustahimili yote.."
Awwwwww...leo ndio nimejua siri ya busara zako.
Oh my God,I'm the luckiest girl ever
#TheBoldIsMine#
 
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu Mzee wa Upako amesema waandishi wote wanaoandika habari za kumchafua watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.

Kauli hiyo aliitoa jana ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yaliyoandikwa kwenye vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa.

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mpo humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema.

=======

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako jana amesema waandishi wote wa habari wanaoandika habari za kumchafua, watakufa kabla ya kufika Machi 2017.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa.

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya, ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mko humu mmekuja na mnasikiliza tu,”alisema.

“Akisema Mungu uishi wewe basi, nakuwa sina namna, lakini sijawahi kumtumikia Mungu ambaye ananyamaza. Nilishakubaliana mimi na Mungu, mpango wa Mungu ndiyo mpango wangu, sasa wajiandae, mimi siyo Sheikh Yahaya, mmeingia choo cha kike, nasema ‘Mama yangu mzazi’ nitaacha kuhubiri, nitaacha kuhubiri ….mimi nina nguvu saaana,”alisema.

Hata hivyo baadaye mchungaji huo alishuka na kusema anamuachia Mungu wake ambaye atawahukumu kwa wakati wake.

“Lakini Mungu anasema tusihukumu, namuachia Mungu atawahukumu kwa wakati wake, haleluya, haleluya, Mungu awabariki sana."

Novemba 24, mitandao ya kijamii ilikuwa na picha zinazomuonyesha Mzee wa Upako akirushiana maneno makali na jirani huyo ambaye anasikika sauti.

Taarifa za kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kiroho zilisambaa baada ya mwandishi wa habari, Happiness Katabazi aliyeshuhudia tukio hilo, kuandika kwa urefu kisa hicho na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Novemba 26, Mzee wa Upako kwa mara ya kwanza alisita kuzungumzia sakata hilo na badala yake akasema wanaomtuhumu waendelee kusema: “Sisemi, lakini siogopi kwenda jela mimi na kwa taarifa yao watashindana sana, lakini hawatashinda. Hii ni kama kumpiga chura teke.”

Novemba 28, pia Mchungaji huyo akajibu akisema maneno aliyotumia ambayo ni mshenzi, mpumbavu na mjinga siyo matusi kwani yameandikwa kwenye biblia na kwamba watu hao ndiyo walianza kumtukana yeye baada ya kuwauliza wanatafuta nini eneo la getini kwake.

Jana, mchungaji huyo aliwahakikishia waumini wake akisema waandishi walioandika kwa lengo la kumchafua watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.

Katika mahubiri yake yaliyojengwa na msingi wa Biblia kutoka kitabu cha Samweli wa kwanza, sura ya 16, mstari wa saba, Mzee wa Upako aliyekaribishwa kwa nyimbo kadhaa ikiwamo ‘kusanya kusanya’ alisema yeye siyo mchungaji anayejikweza, lakini baadhi ya wachungaji wakubwa kutoka nje wamekuwa wakienda kuomba upako.

Pia, alisema hata Rais John Magufuli hakumuita yeye bali aliona kitu ndani yake na kubarikiwa kabla ya kumtembelea.
he looks like an engel, talk like an engel, but a devil in disguise - American singer
 
Hapa mzee wangu umechemka!!! Unazidi kuharibu. Kuna siku utatoa tamko juu ya wasomaji wa hayo magazeti!!
 
Mzee wa upako sasa amekuwa poyoyo mpayukaji; kwanini anatarajia afanye maola kisha watu wasiongee, wasiandike kwani yeye ni kitu gani?! Kasemwa na kuandikwa sana Yesu Kristu sembuse yeye?! Uhayawani huo, watu wazima hawatishiwi nyau bhana, akae kimya aendelee kupiga "dini dili", kwani muda umebaki mfupi sana watamshtukia!
 
Back
Top Bottom