Mchumba wangu kabadilika sana simuelewi

Mchumba wangu kabadilika sana simuelewi

Habari wana jukwaa la MMU,

Mimi nina mpenzi nimedumu nae kwa takribani mwaka mmoja sasa, ila siku za hivi karibuni mwenzangu kabadilika sana kupita kawaida.

Majuzi nimeenda kwake lakini hakuonyesha kujali uwepo wangu na ukizingatia ni miezi miwili ilipita hatujaonana. lakini pia ndani amani hakuna unachomsemesha ndo anachojibu.

Anaweza akakaa kimya siku nzima mpaka uanze wewe kuongea, yeye yuko busy na laptop na simu basi kiukweli nakosa amani ya moyo na nikimuuliza " what's wrong mbona umebadirika hivyo?" anajibu," Nothing".

Mwanzoni tulikuwa tukishikiana simu lakini yeye ya kwake ametia password kila kona.yaani mpaka najiuliza nitakaa maisha haya mpaka lini nakosa amani ya moyo kabisa.

Naombeni ushauri wenu

Asanteni

1. huo uchumba wenu ni halisia, yaani, wazazi wenu, ndugu zenu, marafiki na jamaa zenu wanautambua rasmi?
2. kishika uchumba na mahali vimekwishalipwa?
3. je, mpango wenu wa kufunga ndoa ilikuwa iwe lini?
4. kwa nini kwa kipindi cha mwaka huo mmoja hamjafunga ndoa? je, kulikuwa na vikwazo au conditions zozote zile?
5. muda huo wa miezi miwili ambao hamkuwa pamoja ni sababu gani ziliwafanya msiwe pamoja?
6. je, hapo mwanzo mlipokuwa mkishikiana simu ulikuwa unaikagua simu yake?
7. je, hakuna wabaya wenu ambao mnafikiri ni marafiki kumbe sio ambao yawezekana wametia sumu hapo kwenye relationship yenu? (usiende kwa mganga wa jadi kutafuta hili, tafadhali)

Cha kufanya ni kumweleza kwa utaratibu juu ya malengo yenu ya mwanzo, halafu uzoefu wa mambo ya uchumba na ndoa za watu wengine kuwa uchumba waweza kuvunjika na mahali kurudishwa, halafu ondoka hapo kwake kwa kumuuaga na kwenda kutulia kwako na kuendelea na maisha yako; ukipata mchumba mwingine uwe muazi juu ya tukio hili au siku akirudi kwako mpokee ila kabla ya yote lazima atoe maelezo ya kina juu ya tukio hili na kuhakikisha afya yake ni njema.

Wakati mwingine mtu anaepushwa na jambo baya ambalo laweza kutokea hapo baadae katika mazingira ambayo hayatamfurahisha mapaka hapo baadae ambapo atakuwa na furaha badala ya huzuni.
 
Pole sana my dear...mungu angetupa uwezo wa kuona moyo wa mtu jinsi unavyo waza haya yote yasingekuwepo, usivujike moyo katika mahusiano yenu hizo ni changamoto tu za mahusiano kaa chin zungumza nae kwa upole na unyenyekevu tena kwa sauti ile inayomtoa nyoka pangoni.
 
Mkuu ye ndo Wa kwanza ila mpaka hapa nishachoka na simuhitaji tena kwakweli maana mambo anayoyafanya hapaswi kufanyiwa mtu na moenzi wake, toka Jana sijawasiliana nae na nahis roho yangu ina amani kabisa

Thats my girl! akufukuzae hakwambii toka, najua its not easy lakini kama unaempenda hakupendi sioni sababu ya kupenda usiko pendwa,vuta subra usimtafute ningekua wewe hata number ya ningefuta kwenye cm na sijui kumchungulia kwenye DP kaweka nini yani delete him in yoyr life, unaweza kua umemshikilia yeye unajinyima bahati yako kwa wengine,utampata mwengine ujute kwa yule ulifata nini?
 
1. huo uchumba wenu ni halisia, yaani, wazazi wenu, ndugu zenu, marafiki na jamaa zenu wanautambua rasmi?
2. kishika uchumba na mahali vimekwishalipwa?
3. je, mpango wenu wa kufunga ndoa ilikuwa iwe lini?
4. kwa nini kwa kipindi cha mwaka huo mmoja hamjafunga ndoa? je, kulikuwa na vikwazo au conditions zozote zile?
5. muda huo wa miezi miwili ambao hamkuwa pamoja ni sababu gani ziliwafanya msiwe pamoja?
6. je, hapo mwanzo mlipokuwa mkishikiana simu ulikuwa unaikagua simu yake?
7. je, hakuna wabaya wenu ambao mnafikiri ni marafiki kumbe sio ambao yawezekana wametia sumu hapo kwenye relationship yenu? (usiende kwa mganga wa jadi kutafuta hili, tafadhali)

Cha kufanya ni kumweleza kwa utaratibu juu ya malengo yenu ya mwanzo, halafu uzoefu wa mambo ya uchumba na ndoa za watu wengine kuwa uchumba waweza kuvunjika na mahali kurudishwa, halafu ondoka hapo kwake kwa kumuuaga na kwenda kutulia kwako na kuendelea na maisha yako; ukipata mchumba mwingine uwe muazi juu ya tukio hili au siku akirudi kwako mpokee ila kabla ya yote lazima atoe maelezo ya kina juu ya tukio hili na kuhakikisha afya yake ni njema.

Wakati mwingine mtu anaepushwa na jambo baya ambalo laweza kutokea hapo baadae katika mazingira ambayo hayatamfurahisha mapaka hapo baadae ambapo atakuwa na furaha badala ya huzuni.

Nashukuru sana Mkuu nimeamua kumove on na hata akirudi sitoweza kumsamehe coz kanidharau sana na mm hakuna kitu nachukia kama kudharauliwa
 
Pole sana my dear...mungu angetupa uwezo wa kuona moyo wa mtu jinsi unavyo waza haya yote yasingekuwepo, usivujike moyo katika mahusiano yenu hizo ni changamoto tu za mahusiano kaa chin zungumza nae kwa upole na unyenyekevu tena kwa sauti ile inayomtoa nyoka pangoni.

yaan my dear nimejitahid sana kuutumia uanamke wangu kumueka sawa lakn mwanaume mwenyewe hip hop yaan anavopenda hizo nyimbo za kina weusi sijui fid Q ndo moyo wake ulivo.. he's not romantic at all hata uige sauti ya Celine Dion bado mambo ni yaleyale.. m tired!!
 
Si kwamba wanaume ndo hamna mapenzi ya kweli pia si wanawake,bali ni mtu mwenyewe..it depend na tabia ya mtu sio jinsia sababu wanawake pia tunaumiza pia tunaumizwa same to wanaume wanaumiza na wanaumizwa.

my dia wanaume wanaongoza bhana
 
Thats my girl! akufukuzae hakwambii toka, najua its not easy lakini kama unaempenda hakupendi sioni sababu ya kupenda usiko pendwa,vuta subra usimtafute ningekua wewe hata number ya ningefuta kwenye cm na sijui kumchungulia kwenye DP kaweka nini yani delete him in yoyr life, unaweza kua umemshikilia yeye unajinyima bahati yako kwa wengine,utampata mwengine ujute kwa yule ulifata nini?

Asante Darling ngoja nianze mchakato Wa kumdelete na mapicha mapicha yake
 
Mwanaume Anayekupenda Hawezi kukuumiza Wala Kukufanya Uhuzunike Bali Atahakikisha Kuirudisha na Kuithamini Furaha Yako.. Futa Vumbi, Simama na Uianze Safari.... Wapo Walioumizwa na Wanao Endelea Kuteswa Zaidi Yako. Kuendelea Kulia nikujipa Stress Zisizo na Faida...
 
nyinyi viumbe Hamna huruma wala upendo mna tamaa za mwili tu basi

Sio wote tupo ivyo mbona mi nmetulia...unajua iko ivi ukitaka usiumie sana usiwe mwepes kuutuoa mwili wako kwa mwanaume( usiwe mwepes kutoa penz) hata akikuacha utaumia ila siyo kivile sababu thamani ya mwili wako inakuwa palepale kinachowaumiza ni pale unapogundua tayar umempa thamani na kakujua vilivy,,,,hii izingatie ukimpata mpya itakusaidia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom