Mchumba wangu ameamua tuachane

Mchumba wangu ameamua tuachane

Cha msingi kaka fikiria kutafuta ela tu mapenzi siku hizi hayana mjuzi wala formula, ila mtoto husiache kumlea ata ukipata kumi we mtumie tu maana hasije kumuambia ata mtoto kuwa baba yako ndio alitukimbia hawachelewi hawa.
Ukimtumia hela si ndo watakula wote na baba mwingine? Subiri amlishe afike miaka 7 nawe uchukue jukumu la kumtunza. Mpaka akue... Mnagawana miaka tu ya kulea.. Matunzo ni jukumu la baba na mama..
 
Kuna wizara mpya imeanzishwa na raisi mwenye kasi ya ajabu nayo ni wizara ya Mapenzi, Uchumba, Kuoana na taraka.

Waziri mwenye dhamana Siku ya kwanza tu alipoteuliwa alilia sana maana alikuwa na uchungu na watu wanavyopigana chini.

Ameahidi kufuta mitandao ya kijamii na kuondoa bundles (mb's) ili watu wasiwe na access na mitandao.

Amesema kuwa kwasasa hata ukiwa na smartphone haitakuwa na kazi zaidi ya kupiga picha.

Amewataka wanaonunua simu za gharama kuacha maramoja maana ndio chanzo cha migogoro kwenye mahusiano. Amesema ni bora MTU akanunua simu za promosheni au tecno, huawei na itel ambazo hata ukitaifishwa na mamlaka haitakuuma sana.

Pia amesema kuanzia sasa hakutakuwa na taraka maana kama watu walikubaliana na kufunga ndoa wenyewe kwanini waachane. Alisema kama wanandoa hawa walitongozana, wakakubaliana, wakachunguzana, wakapelekana gest na maghetoni wakaonjana baadhi yao na baadae wakataarifu wazazi kuwa wanataka kuoana iweje Leo watake talaka? Hayo ni matuminizi mabaya ya rasilimali ubongo.

Ni huko nchi za nje!
Nimecheka sana hope ingekuja kwetu hiyo
 
Aisee! Hivi kumbe na wanaume huwa mnalia mkiachwa??? Duh! Kijana! Katafute pesa acha uboya! Mwenzako keshakuona we fala yaani mzigo hamlingani ! Na unavyotoa michozi ndo kabisaaa anakuona duanzi!khaa! Skia,usimtafute ,tafuta pesa!tena uondoke huko nyumbani kwake! Mpotezee akishavurugwa huko atarudi na magoti juu! Eboh!
 
We as men think differently, mwanamke akikuzingua unampotezea yeye na mtoto wake ingawaje na we ni mtoto wako.
Na mwanamke ukimfeel unamtake care ye na mtoto wake hata kama mtoto sio wako.
Still you didn't answer my question what the child has to do na mistake ya Huyo Dada? I think the baby has to be left out of this crazy mess na jamaa has to take care of that baby since the child is his .. Thanks..
 
Ukimtumia hela si ndo watakula wote na baba mwingine? Subiri amlishe afike miaka 7 nawe uchukue jukumu la kumtunza. Mpaka akue... Mnagawana miaka tu ya kulea.. Matunzo ni jukumu la baba na mama..
Si lazima ela ata mavazi yanatosha, ela ya matumizi kwa mtoto unaweza kutuma kiasi kidogo. Yeye hasiangalie anakula na nani hiyo Pesa.
 
Kama hayajawahi kukukuta unaweza kutoa kebehi na dharau za aina yoyote lakini kwa tunaojua nini mapenzi tunaumia sana tunapoona yanamtokea mtu,mapnz yana nguvu sana jamani,but no way out ishatokea jamaa,piga moyo konde kwa sasa,angalia kitu unachopenda uwe nacho bize ili kuondoa stress,after the time utasahau kila kitu na maisha yatasonga,huwezi jua MUNGU mkuu kakuepusha na nini,using'ang'anie.
 
kwanza sali mpe Mungu shida zako nae atakutatutllia matatizo yako. halaf malipo nibhapa hapa duniani kupunguza mawazo najuabulimpenda sana ila usiwaze Mungu atakupatia mwingine tena wakukujali kabisa mwambie akupe mtoto umleee kwani ndio faraja yako akikataa nenda kadai haki yako mahakamani. pia jichanganye upoteze mawazo kula mziki na burudani bro ucjali utampata mdada atakufufa machozy tuu. sa nyingine wanawake ni kama mapepo pia kwa level yako huoni kakuacha sna mbali so anataka wa levo zake wala usilie ni kawaida ukiona umekaa nae sana. jua ana kipaji chamsingi we mbato rafi then songa mbele hawa nibwakutuliwaza usimtegemee mtu mtegemee Mungu tuu. damn this bichez are so complicated.
 
Amekwambia form 4 harafu we unaandika kiswanglish... Utakuwa unamsaidia kweli?
english yake simple sana hii mimi mwenye STD 7 lkn namsoma fresh ila sionagi sababu ya kingereza wakati thread imeandikwa kwa kiswahili.
 
Dear If I was you ..as bitter as it is ningeshukuru Mungu for the everything .. Huyo hakuwa wako my Kaka subiri wako anakuja.. Just move on by taking a time off on dating for a while .. Take care of your child with all your heart .. Invest your time on Praying, your child and work.. Na God will heal you.. Dont worry huyo yakimmshindwa mbona atakukumbuka na kurudi kwa kasi kwako.. But never take her back because hakuthamini Upendo wako bali alithamini money , forget her dear , she is not worthy for your tears to come out ... Nakuhakikishia she will pay for your tears huko ataaishia kuchezewa na kupotezewa muda .. Why? For what she did to you.. Unajua ni bora MTU akucheat , au ku lie then can do that the way she did.. But you didnt ... Ni wivu tuu wa kummpenda ... Sasa wait the outcome yake ya ku reap for what she sowed .. Soon it will come .. Pole sana... Thanks..
Nimeupenda sana ushauri wako.,
 
Ila jamani mapenzi yanauma mno mno kuliko ambavyo mtu unaweza kufikiria ila jipe muda utasahau tu na utaendelea na maisha yako,jipende,jitunze na jithamini wewe kwanza.
 
I think tunatofautiana as human being from different backgrounds... Some women ni ulimbukeni unawasumbua tuu.... That's all I can say .. Kuna some women I know wamekwenda shule zaidi ya waume zao walioolewa nao na huwezi juwa if their husbands wako chini in education . they just let Love lead .. So it depends . Malezi pia na maisha ya kuiga yanachangia kwa hili.. Thanks
Elimu ndogo kwa mwanaume na mkwanja hakuna, uhusiano hauwezekani.
 
Sasa keshakumwaga bado unang'ang'ania nini? Wewe ni bure kwake ndo maana pamoja na kugombana kwenu hakuwa na muda na wewe. Mambo ya kufanya ni mengi, pengine waweza kuwa unalia sababu uliwah kuwa moja ya nguzo yake kipindi yupo chuo. Ndugu "Mara nyingine huwa tunatumika kama madaraja kuwafanya tuwapendao au tuliowasaidia kufika pahala na kukutana na waliokusudiwa ingawa huwa tunaishia katika uchungu na majuto mengi." Angalia upande mwingine wa maisha, na ikibidi mchukue mtoto mkapime DNA ili uwe na uhakika kuwa ni wako.
 
Ndugu zangu mm ni kijana miaka 30,elimu yangu ni kidato cha 4. nina mchumba ambaye ukweli nnapenda sana, nimekuwa nae kwenye mahusiano, kuanzia 2014 alipo maliza tuu degree ya uhasibu pale tia, nilikutana nae mtaani tuu ndipo mahusiano yakaanza.

Tumebahatika kupata mtoto wa kike 19. 10 2015, mwenzagu kwa sababu anavyeti alikuwa amesha apply kazi sehemu tofauti tofauti na bahati nzuri 2015 alipata kazi selikarini. Alipo pangiwa sehemu ya kazi ikabidi tukubaliane mm nimfuate, ingawa kipindi hicho nilikuwa na umachinga wangu Dar, kweli baada ya miezi kadhaa mm niliamua kumfuata mpenzi wangu ili tuishi pamoja, maisha yamesonga ingawa mikwaruzano ya hapa na pale ni mingi tumeishi hivyo hivyo.

Mwezi wa kwanza walipewa maelekezo na tasisi waende kusoma, Short courses ya miezi 4, ameenda na mtoto baada ya wiki akamuachisha mtoto ziwa ili awe na muda mzuri wa kusoma mtoto akampeleka kwa bb yake huko huko dar. Kwa hili mm niliona ni sawa ili awe na muda mzuri wakujisomea maana mwisho wa siku wafanye tena mitihani.

Tulikuwa tunawasiliana vizuri tuu. Muda wowote ule, baada ya wiki tatu, ndipo matatizo yalipoanza, kuna siku nilimpigia simu zote mbili zikawa hazipatikani, sikujua shida ni nini kwa sababu tulikuwa tumeshazoeshana kujulisha kwa kila hali mm hiyo siku nilipaniki nilipiga simu usiku mzima simu zikajapatikana saa 3 asubuhi kumuuliza anasema ziliisha chaji, wakati huo huo, usiku niliingia WhatsApp niliona last seen yake ilikuwa saa8:43 usiku.

Nilishidwa kuelewa, nilimtukana sana kwasababu ya hasira ila yy akawa ananicheka, nilimuambia kuongea na mm lazma anipe sababu za kuridhisha sikumuamini kwa sababu ya kuonekana online usiku.

Sikumtafuta nikiamini kwamba lazima anitafute angalau aniombe msamaha, imepita miezi 2 bila mawasiliano, nimekuja kusitukia sasa mm nnahitaji mawasiliano nae tayari yupo kwenye uhusiano mwingine huko huko chuo eti ameshachoka kusubili hasira zangu ziishe, na ananitamkia wazi hataki tena kuishi na mm sababu sijamtafuta miezi 2, nimelia sana nmemuomba mm kama nilikosa anisamehe aachane na jamaa hataki anasema nimeshachelewa kusolve tatizo.

Nnapiga cmu anakata nnatuma sms hazijibiwi, na hadi fb ameandika ameingia kwenye uhusiano mpya. Ndugu zangu nnalia sijui cha kufanya, ukweli nnampenda sana.
Me wallaa ckujibu
 
Tumia kichwa kikubwa mkuu, ndo ushaachwa hivyo anza kusaka hela kwa kutumia hasira hizo ukizipata tu utaona nyota yako inavyowaka
 
Tatizo la ilimu duni linawatesa sana vijana wengi katika mahusiano, lakini dokta mwaka ni suluhisho... Kama vp mpotezee. Tafuta unayelingana naye kielimu huenda mkaenda sawa... Pole sana mwana. Yote hayo ni mapito ya dunia hii...
 
Back
Top Bottom