Mchumba wangu ameamua tuachane

Apr 6, 2016
33
5
Ndugu zangu mm ni kijana miaka 30,elimu yangu ni kidato cha 4. nina mchumba ambaye ukweli nnapenda sana, nimekuwa nae kwenye mahusiano, kuanzia 2014 alipo maliza tuu degree ya uhasibu pale tia, nilikutana nae mtaani tuu ndipo mahusiano yakaanza.

Tumebahatika kupata mtoto wa kike 19. 10 2015, mwenzagu kwa sababu anavyeti alikuwa amesha apply kazi sehemu tofauti tofauti na bahati nzuri 2015 alipata kazi selikarini. Alipo pangiwa sehemu ya kazi ikabidi tukubaliane mm nimfuate, ingawa kipindi hicho nilikuwa na umachinga wangu Dar, kweli baada ya miezi kadhaa mm niliamua kumfuata mpenzi wangu ili tuishi pamoja, maisha yamesonga ingawa mikwaruzano ya hapa na pale ni mingi tumeishi hivyo hivyo.

Mwezi wa kwanza walipewa maelekezo na tasisi waende kusoma, Short courses ya miezi 4, ameenda na mtoto baada ya wiki akamuachisha mtoto ziwa ili awe na muda mzuri wa kusoma mtoto akampeleka kwa bb yake huko huko dar. Kwa hili mm niliona ni sawa ili awe na muda mzuri wakujisomea maana mwisho wa siku wafanye tena mitihani.

Tulikuwa tunawasiliana vizuri tuu. Muda wowote ule, baada ya wiki tatu, ndipo matatizo yalipoanza, kuna siku nilimpigia simu zote mbili zikawa hazipatikani, sikujua shida ni nini kwa sababu tulikuwa tumeshazoeshana kujulisha kwa kila hali mm hiyo siku nilipaniki nilipiga simu usiku mzima simu zikajapatikana saa 3 asubuhi kumuuliza anasema ziliisha chaji, wakati huo huo, usiku niliingia WhatsApp niliona last seen yake ilikuwa saa8:43 usiku.

Nilishidwa kuelewa, nilimtukana sana kwasababu ya hasira ila yy akawa ananicheka, nilimuambia kuongea na mm lazma anipe sababu za kuridhisha sikumuamini kwa sababu ya kuonekana online usiku.

Sikumtafuta nikiamini kwamba lazima anitafute angalau aniombe msamaha, imepita miezi 2 bila mawasiliano, nimekuja kusitukia sasa mm nnahitaji mawasiliano nae tayari yupo kwenye uhusiano mwingine huko huko chuo eti ameshachoka kusubili hasira zangu ziishe, na ananitamkia wazi hataki tena kuishi na mm sababu sijamtafuta miezi 2, nimelia sana nmemuomba mm kama nilikosa anisamehe aachane na jamaa hataki anasema nimeshachelewa kusolve tatizo.

Nnapiga cmu anakata nnatuma sms hazijibiwi, na hadi fb ameandika ameingia kwenye uhusiano mpya. Ndugu zangu nnalia sijui cha kufanya, ukweli nnampenda sana.
 
Anza maisha yako mapya kamanda kama akifa Leo maisha yako yataendelea hayawez kuishia kwa kuwa yeye amekufa, anza upya jenga maisha yako mshitikishe Mungu na pigana kiume umlee mwanano huyo mwanamke hakufai tayar ana maisha yake mapya atakuumiza zaidi ukiendelea kumng'ang'ania
 
Pole sana ndugu ,hapo tatizo ni pesa yy tayari amesha ona maisha mengn inshort hakupendi, ndomana na encourage wanaume mujitahidi kutafuta wa level yk. Form four oa form four au std 7 hawa wanawake walio fika mbali kukuzidi utakufa kaka angu,tafuta pesa oa mke mzr, maisha yakisha mpiga atarudi kwa magoti.pole sn
 
Ndugu zangu mm ni kijana miaka 30,elimu yangu ni kidato cha 4. nina mchumba ambaye ukweli nnapenda sana, nimekuwa nae kwenye mahusiano, kuanzia 2014 alipo maliza tuu degree ya uhasibu pale tia, nilikutana nae mtaani tuu ndipo mahusiano yakaanza.

Tumebahatika kupata mtoto wa kike 19. 10 2015, mwenzagu kwa sababu anavyeti alikuwa amesha apply kazi sehemu tofauti tofauti na bahati nzuri 2015 alipata kazi selikarini. Alipo pangiwa sehemu ya kazi ikabidi tukubaliane mm nimfuate, ingawa kipindi hicho nilikuwa na umachinga wangu Dar, kweli baada ya miezi kadhaa mm niliamua kumfuata mpenzi wangu ili tuishi pamoja, maisha yamesonga ingawa mikwaruzano ya hapa na pale ni mingi tumeishi hivyo hivyo.

Mwezi wa kwanza walipewa maelekezo na tasisi waende kusoma, Short courses ya miezi 4, ameenda na mtoto baada ya wiki akamuachisha mtoto ziwa ili awe na muda mzuri wa kusoma mtoto akampeleka kwa bb yake huko huko dar. Kwa hili mm niliona ni sawa ili awe na muda mzuri wakujisomea maana mwisho wa siku wafanye tena mitihani.

Tulikuwa tunawasiliana vizuri tuu. Muda wowote ule, baada ya wiki tatu, ndipo matatizo yalipoanza, kuna siku nilimpigia simu zote mbili zikawa hazipatikani, sikujua shida ni nini kwa sababu tulikuwa tumeshazoeshana kujulisha kwa kila hali mm hiyo siku nilipaniki nilipiga simu usiku mzima simu zikajapatikana saa 3 asubuhi kumuuliza anasema ziliisha chaji, wakati huo huo, usiku niliingia WhatsApp niliona last seen yake ilikuwa saa8:43 usiku.

Nilishidwa kuelewa, nilimtukana sana kwasababu ya hasira ila yy akawa ananicheka, nilimuambia kuongea na mm lazma anipe sababu za kuridhisha sikumuamini kwa sababu ya kuonekana online usiku.

Sikumtafuta nikiamini kwamba lazima anitafute angalau aniombe msamaha, imepita miezi 2 bila mawasiliano, nimekuja kusitukia sasa mm nnahitaji mawasiliano nae tayari yupo kwenye uhusiano mwingine huko huko chuo eti ameshachoka kusubili hasira zangu ziishe, na ananitamkia wazi hataki tena kuishi na mm sababu sijamtafuta miezi 2, nimelia sana nmemuomba mm kama nilikosa anisamehe aachane na jamaa hataki anasema nimeshachelewa kusolve tatizo.

Nnapiga cmu anakata nnatuma sms hazijibiwi, na hadi fb ameandika ameingia kwenye uhusiano mpya. Ndugu zangu nnalia sijui cha kufanya, ukweli nnampenda sana.
Dear If I was you ..as bitter as it is ningeshukuru Mungu for the everything .. Huyo hakuwa wako my Kaka subiri wako anakuja.. Just move on by taking a time off on dating for a while .. Take care of your child with all your heart .. Invest your time on Praying, your child and work.. Na God will heal you.. Dont worry huyo yakimmshindwa mbona atakukumbuka na kurudi kwa kasi kwako.. But never take her back because hakuthamini Upendo wako bali alithamini money , forget her dear , she is not worthy for your tears to come out ... Nakuhakikishia she will pay for your tears huko ataaishia kuchezewa na kupotezewa muda .. Why? For what she did to you.. Unajua ni bora MTU akucheat , au ku lie then can do that the way she did.. But you didnt ... Ni wivu tuu wa kummpenda ... Sasa wait the outcome yake ya ku reap for what she sowed .. Soon it will come .. Pole sana... Thanks..
 
Kuna wizara mpya imeanzishwa na raisi mwenye kasi ya ajabu nayo ni wizara ya Mapenzi, Uchumba, Kuoana na taraka.

Waziri mwenye dhamana Siku ya kwanza tu alipoteuliwa alilia sana maana alikuwa na uchungu na watu wanavyopigana chini.

Ameahidi kufuta mitandao ya kijamii na kuondoa bundles (mb's) ili watu wasiwe na access na mitandao.

Amesema kuwa kwasasa hata ukiwa na smartphone haitakuwa na kazi zaidi ya kupiga picha.

Amewataka wanaonunua simu za gharama kuacha maramoja maana ndio chanzo cha migogoro kwenye mahusiano. Amesema ni bora MTU akanunua simu za promosheni au tecno, huawei na itel ambazo hata ukitaifishwa na mamlaka haitakuuma sana.

Pia amesema kuanzia sasa hakutakuwa na taraka maana kama watu walikubaliana na kufunga ndoa wenyewe kwanini waachane. Alisema kama wanandoa hawa walitongozana, wakakubaliana, wakachunguzana, wakapelekana gest na maghetoni wakaonjana baadhi yao na baadae wakataarifu wazazi kuwa wanataka kuoana iweje Leo watake talaka? Hayo ni matuminizi mabaya ya rasilimali ubongo.

Ni huko nchi za nje!
 
Why wewe hata elimu yako sio kihivyo ukaingia kwa huyo ambaye ni degree kabisa. Mwanamke anakuwa na ego Fulani ambayo hawezi kujizuia km akikuzidi elimu that's y huko chuo kakuta wa level yake kielimu ndio maana kasepa. Tafuta STD 7 ndugu yangu wala hutasikia maumivu tena
 
hawa watu ni wa kuwatafutia hela tu. hiyo hasira ikuongezee nguvu ya kusaka hela ili ufanikiwe zaidi. atarudi mwenyewe tu
 
Yaani mwanaume wa leo bado unalilia mwanamke?...inbox nikugawie dada yangu.
 
Sjui kwanini haya mambo skuizi misipendi kuyaongelea kabisa aiseee...... sababu mapenzi yamekua na maumivu makubwa zaidi ya misiba, na watu tumejikuta tuna haribikiwa kabisa kwasababu ya mapenzi.
Agghhhh... ngoja nisiendelee tu
 
Mtoto wa kiume acha kulia lia wanawake wote mjini humu.!!! Kama hakutaki msusie na mtoto pia. Yakimfika shingoni atakutafuta tu.
 
It sounds like umeachwa na sio kuachana
Sitaki kukupa pole kwa kuachwa kwa sababu ni maamuzi ambayo mwenzako amefikia.
Labda nikuulize
1. Baada ya kulia, umepata ahueni ya maumivu ya kuachwa?
2. Hivi mwanamke ameshakwambia ana mahusiano mengine ( ana mwanaume mwingine anayeshiriki naye tendo la ngono) unalazimisha arudiane nawe ili iweje?!
3. Angalia mustakabali wa mtoto wako, kwa miaka yako 30 jipange uoe mke mwingine na acha maisha yaendelee. Utamuwaza huyo mwanamke mpaka lini? Itakusaidiaje ?
4. Mapenzi hufikia mwisho, au hujui? Sahau hizi Habari za kupendana Sana ; katika ulimwengu halisi hayo ni mambo ya kufikirika.

Note: Nothing is permanent; hautaishi milele hapa. Ukikaa na kulialia katika ulimwengu huu utalia sana.
 
Mtoto wa kiume acha kulia lia wanawake wote mjini humu.!!! Kama hakutaki msusie na mtoto pia. Yakimfika shingoni atakutafuta tu.
Dear What the kid has to do na break up yao? I call it irresponsible parent to any Father does that.. Thanks..
 
Back
Top Bottom