Mchumba wangu ameamua tuachane

Mchumba wangu ameamua tuachane

Dear If I was you ..as bitter as it is ningeshukuru Mungu for the everything .. Huyo hakuwa wako my Kaka subiri wako anakuja.. Just move on by taking a time off on dating for a while .. Take care of your child with all your heart .. Invest your time on Praying, your child and work.. Na God will heal you.. Dont worry huyo yakimmshindwa mbona atakukumbuka na kurudi kwa kasi kwako.. But never take her back because hakuthamini Upendo wako bali alithamini money , forget her dear , she is not worthy for your tears to come out ... Nakuhakikishia she will pay for your tears huko ataaishia kuchezewa na kupotezewa muda .. Why? For what she did to you.. Unajua ni bora MTU akucheat , au ku lie then can do that the way she did.. But you didnt ... Ni wivu tuu wa kummpenda ... Sasa wait the outcome yake ya ku reap for what she sowed .. Soon it will come .. Pole sana... Thanks..
I just like your advice.

I appreciate you Dear Loveissweet.
 
U gotta be naive to believe that we live in a perfect world,bad things happen to good people. And please don't get me wrong coz by no means do I support dead beat dads.
Halafu later on the child akija kukulaumu , for you not to be there , ndio nyie mnaanza kusema oooh her/ his mother taught the child to say that... Honestly men like that I do not have No respect toward them .. Because whatever happened between mother and Father has nothing to do with that child.. And for the Father not keep his duties going on , it shows how weaker he is and irresponsible parent... Thanks...
 
Pole sana... Kuna mdada anafanya kazi shirika moja la hifadhi ya jamii Dar makao makuu.. nae anakisa kama chako cha kuachwa kwa style hiyo...
 
Mkuu...
Ebu fanya utaratibu uwakutanishe.
I hope itakua boonge la couple
 
Pole sana ndugu yangu,hilo kwanza ni fundisho kwako,pili tumia hasira kutafuta yalishanikuta yeye alikuwa mtoto wa tajiri mimi nilikuwa machinga,lakini baada ya miaka kama kumi,tulikutana anatia huruma,baba yake alishakufa,bank wakataifisha mali,halafu mimi niko freshi na nimeowa,utakuja furahi tu siku moja chozi lako haliwezi kwenda bure
 
ameshapata muhasibu mwenzake. achana nae. ingawa mapenzi hayachagui, kwa elimu yako ya form four, kazi yako umachinga, ulikosea sana kuoa mke mwenye degree. kwa ufupi amekuona wewe ni mzigo maana mwanamke anataka kutunzwa na sio kutunza
 
Nimekufuatilia sana huu mkenge unawakuta wengi sana kuzaa sio tija , ELIMU yako na yake ni tofauti, UTEGEMEZI wako pia ni TATIZO , and FIMBO ya mbali mara nyingi haiui NYOKA .! fanya yako tu.
 
Pole kwa yaliyokukuta. Wewe siyo wa kwanza na hautakuwa wa mwisho kuachwa.

Kubali yaliyotokea japokuwa ni ngumu sana. Kwa sasa hivi kama vile upo kwenye hatua ya mwanzo kabisa ya kutokuamini yaliyotokea.

Hiyo ni kawaida kabisa hasa kama ulimpenda kwa dhati huyo mwanamke. Lakini baadae utaingia hatua ya kukubali yaliyotokea. Hapo utaumia sana tuu ila usikwepe au kujaribu kuyafukia hayo maumivu.

Kama wewe ni mtu wa kulia, basi lia sana. Hata siku moja usipingane na jinsi unavyojifeel. Let it out.

Ukishakubali yaliyotokea, then jiuguze na mwisho songa mbele. Hii ni ngumu sana lakini nakuhakikishia baada ya muda (inaweza kuwa miezi kadhaa au miaka miaka miwili) utakuja kuangalia nyuma na kujikuta unajiuliza, hivi nilikuwa nalia nini? Hivi nilimpendea nini yule mwanamke?

Kwa sasa usiwasiliane na huyo mwanamke tena isipokuwa kwa masuala ya mtoto tuu. Ukiwasiliana nae, ongea nae kwa kifupi sana juu ya mtoto tuu. Akitaka kukuongeleshea masuala mengine mwambie uko bize.

Pili usidate mwanamke mwingine kwa nia ya kuwa na mahusiano nae mpaka pale utakapokuwa umejiuguza na kusonga mbele. Muda huu zingatia zaidi kwenye biashara zako, kula vizuri, vaa fresh, tafuta marafiki zako wa zamani, nk. Huu ndo wakati wako wa kuwa wewe na kufanya mambo yako free bila kumhusisha yeye.

Usilewe pombe au kutumia madawa kuondoa mawazo. Pia usimchukie wala usimsumbue kwa msg au simu. Huwa wanasema njia pekee ya kumwonyesha unayempenda kuwa unampenda ni kumwacha aende anakotaka kwenda.

Tatizo letu kwa jamii yetu hasa kwa wanaume ni kuwa tunajua kuanzisha mahusiano lakini wengi wetu hatujui nini cha kufanya baada ya kutemwa. Tunaishia kucheza karata ya victim, wakati kwenye mahusiano, it takes two to tango.

Kwa hiyo, kubali kuwa kuna makosa ulifanya kwenye mahusiano na huyo mwanamke. Jifunze kutoka kwenye hayo makosa na mwisho utakuwa a better man.
 
Mkuu makosa yapi unavyoona nilifanya
 
Ndugu zangu mm ni kijana miaka 30,elimu yangu ni kidato cha 4. nina mchumba ambaye ukweli nnapenda sana, nimekuwa nae kwenye mahusiano, kuanzia 2014 alipo maliza tuu degree ya uhasibu pale tia, nilikutana nae mtaani tuu ndipo mahusiano yakaanza.

Tumebahatika kupata mtoto wa kike 19. 10 2015, mwenzagu kwa sababu anavyeti alikuwa amesha apply kazi sehemu tofauti tofauti na bahati nzuri 2015 alipata kazi selikarini. Alipo pangiwa sehemu ya kazi ikabidi tukubaliane mm nimfuate, ingawa kipindi hicho nilikuwa na umachinga wangu Dar, kweli baada ya miezi kadhaa mm niliamua kumfuata mpenzi wangu ili tuishi pamoja, maisha yamesonga ingawa mikwaruzano ya hapa na pale ni mingi tumeishi hivyo hivyo.

Mwezi wa kwanza walipewa maelekezo na tasisi waende kusoma, Short courses ya miezi 4, ameenda na mtoto baada ya wiki akamuachisha mtoto ziwa ili awe na muda mzuri wa kusoma mtoto akampeleka kwa bb yake huko huko dar. Kwa hili mm niliona ni sawa ili awe na muda mzuri wakujisomea maana mwisho wa siku wafanye tena mitihani.

Tulikuwa tunawasiliana vizuri tuu. Muda wowote ule, baada ya wiki tatu, ndipo matatizo yalipoanza, kuna siku nilimpigia simu zote mbili zikawa hazipatikani, sikujua shida ni nini kwa sababu tulikuwa tumeshazoeshana kujulisha kwa kila hali mm hiyo siku nilipaniki nilipiga simu usiku mzima simu zikajapatikana saa 3 asubuhi kumuuliza anasema ziliisha chaji, wakati huo huo, usiku niliingia WhatsApp niliona last seen yake ilikuwa saa8:43 usiku.

Nilishidwa kuelewa, nilimtukana sana kwasababu ya hasira ila yy akawa ananicheka, nilimuambia kuongea na mm lazma anipe sababu za kuridhisha sikumuamini kwa sababu ya kuonekana online usiku.

Sikumtafuta nikiamini kwamba lazima anitafute angalau aniombe msamaha, imepita miezi 2 bila mawasiliano, nimekuja kusitukia sasa mm nnahitaji mawasiliano nae tayari yupo kwenye uhusiano mwingine huko huko chuo eti ameshachoka kusubili hasira zangu ziishe, na ananitamkia wazi hataki tena kuishi na mm sababu sijamtafuta miezi 2, nimelia sana nmemuomba mm kama nilikosa anisamehe aachane na jamaa hataki anasema nimeshachelewa kusolve tatizo.

Nnapiga cmu anakata nnatuma sms hazijibiwi, na hadi fb ameandika ameingia kwenye uhusiano mpya. Ndugu zangu nnalia sijui cha kufanya, ukweli nnampenda sana.
Is this a real story or something similar to metaphore? Kama ni real story kusema kweli it's so sad, better u are crying but ingekua mimi ni mazishi. Mbaya sana.
 
Mkuu makosa yapi unavyoona nilifanya

Sikuwa kwenye hayo mahusiano kwa hiyo siwezi kujua ulifanya makosa gani.

Hata hivyo, huwezi kudai wewe ni perfect. Huwezi kudai hukufanya kosa lolote.

Vingenevyo, ukija kuanzisha mahusiano na mwanamke mwingine utashangaa anasepa tena bila kujua sababu.

Kaa chini tafakari tokea muanze mahusiano yapi ulifanya vizuri na yapi ulifanya vibaya na kwa nini? Then, fikiria hayo uliyofanya vibaya utayasahihisha kivipi kwenye mahusiano yajayo.

Lakini kama ukiendelea kuhoji umefanya makosa gani hutajifunza na hutabadilika kuwa mtu mzuri zaidi.

Kumbuka mwanamke akiamua kukuacha haamui leo na kukuacha kesho. Sisemi kuwa nae hana makosa lakini kama nilivyosema mwanzoni kwenye mahusiano, it takes two to tango.

Kuna sababu ambazo zimemfanya akuache lakini kama wawanake wengine hatakwambia hizo sababu.
 
Dah...mbona hiyo bahati mkuu amekupa chance ya kumprove wrong..Ur gentlement mkuu Mungu amekuepusha na balaa mbele
 
Ndugu zangu mm ni kijana miaka 30,elimu yangu ni kidato cha 4. nina mchumba ambaye ukweli nnapenda sana, nimekuwa nae kwenye mahusiano, kuanzia 2014 alipo maliza tuu degree ya uhasibu pale tia, nilikutana nae mtaani tuu ndipo mahusiano yakaanza.

Tumebahatika kupata mtoto wa kike 19. 10 2015, mwenzagu kwa sababu anavyeti alikuwa amesha apply kazi sehemu tofauti tofauti na bahati nzuri 2015 alipata kazi selikarini. Alipo pangiwa sehemu ya kazi ikabidi tukubaliane mm nimfuate, ingawa kipindi hicho nilikuwa na umachinga wangu Dar, kweli baada ya miezi kadhaa mm niliamua kumfuata mpenzi wangu ili tuishi pamoja, maisha yamesonga ingawa mikwaruzano ya hapa na pale ni mingi tumeishi hivyo hivyo.

Mwezi wa kwanza walipewa maelekezo na tasisi waende kusoma, Short courses ya miezi 4, ameenda na mtoto baada ya wiki akamuachisha mtoto ziwa ili awe na muda mzuri wa kusoma mtoto akampeleka kwa bb yake huko huko dar. Kwa hili mm niliona ni sawa ili awe na muda mzuri wakujisomea maana mwisho wa siku wafanye tena mitihani.

Tulikuwa tunawasiliana vizuri tuu. Muda wowote ule, baada ya wiki tatu, ndipo matatizo yalipoanza, kuna siku nilimpigia simu zote mbili zikawa hazipatikani, sikujua shida ni nini kwa sababu tulikuwa tumeshazoeshana kujulisha kwa kila hali mm hiyo siku nilipaniki nilipiga simu usiku mzima simu zikajapatikana saa 3 asubuhi kumuuliza anasema ziliisha chaji, wakati huo huo, usiku niliingia WhatsApp niliona last seen yake ilikuwa saa8:43 usiku.

Nilishidwa kuelewa, nilimtukana sana kwasababu ya hasira ila yy akawa ananicheka, nilimuambia kuongea na mm lazma anipe sababu za kuridhisha sikumuamini kwa sababu ya kuonekana online usiku.

Sikumtafuta nikiamini kwamba lazima anitafute angalau aniombe msamaha, imepita miezi 2 bila mawasiliano, nimekuja kusitukia sasa mm nnahitaji mawasiliano nae tayari yupo kwenye uhusiano mwingine huko huko chuo eti ameshachoka kusubili hasira zangu ziishe, na ananitamkia wazi hataki tena kuishi na mm sababu sijamtafuta miezi 2, nimelia sana nmemuomba mm kama nilikosa anisamehe aachane na jamaa hataki anasema nimeshachelewa kusolve tatizo.

Nnapiga cmu anakata nnatuma sms hazijibiwi, na hadi fb ameandika ameingia kwenye uhusiano mpya. Ndugu zangu nnalia sijui cha kufanya, ukweli nnampenda sana.
Elimu yako ndio tatizo alikuwa na stress tu ndio maana alikukubali hivi sasa ni stress free anajichagulia level zake Fanya maisha yako Huyo sio wako
 
we ndo star kwenye movie. Mkeo jambazii.. kwa maana hiyo usiifanye movie ikose mashiko au utamu ..movie imetumika kama maisha.. songa mbelee tafuta majambazi wengine ..

Maisha ni kama riadha katika mashindano ya mbio ndefu malathoni ukikata tamaa unakaa pembeni wengine wanaendelea ..usikate tamaa endelea kukimbia

Kiufupi huyo mama yetu mdogo hakufai hatakama ukifanikiwa kumbembeleza akarudi atajiona mwanaume utaendeshwa ..utageuzwa zoba

Over
 
Hahahah kwa kweli nimecheka baada yakusoma si kwa nia mbaya ika imenifurahisha....we jamaaa unalenda vibaya sana f unmoiga mkwara mtu ambaye anaona ye ana options zingine...pole sana tafuta chako acha kujipa presure tumi akili z Kiume huna chako hapo...
 
Sasa mkuu, huyo ameushikilia uhai wako? Au wanawake wameisha? Kama ameamua hivyo,si uendelee na yako? Tafuta anaekupenda ufanye mengine,huyo hakupendi,full stop!
 
Back
Top Bottom