Mchumba ninayekaribia kumuoa mjamzito

Tigga,
Duh inaonyesha wewe sio mvumilivu hata kidogo, nakusihi ujitafakari upya kama maisha unayoyaenda utayamudu. Kuna changamoto nyingi sana, sembuse hili. Mimi nilikuwa na case kama yako- kabla ya ndoa mchumba akapata mimba. I was extra extra extra happy. Baada ya wiki 2 sasa zile effect zikaanza- full kutapika, kichwa , kizunguzungu. Ila in all that i was happy. Alikuwa mama anatapika hadi anaishiwa maji na analazwa, mzee mzima nachukua off kumhudumia. alikuwa hapendi wageni, hapendi kelele, (tunanongonezana) etc. Ila nilimchukulia taratibuuuuuu. Akitapika nazoa , akitaka chakula ntatafuta, tena anaweza omba kuku-ukahangaika kumtafuta na ukimleta tu anasema sio kuku tena ni mbuzi !!! . Ukaribu wangu ulijenga sana mahusiano yetu , alipokuwa miezi 5 preg tukafunga ndoa.

Kwa hiyo kama unaona kutapika ni kujifanyisha ,bado kuna mengi. Maana akijifungua lazima usaidie kubadili nepi/pampers. Utabeba mtoto akilia, utamfulia hadi nguo za ndani akiwa bado mzazi.
Be responsible bwana.
 
Sikujua kama wewe ni mwanaume,why umejiita Tigga?BACK TO TOPIC:msome Kongosho ametoa ushauri mzuri!
 
Last edited by a moderator:
Duh vijana siku hizi mnatunguana kweki kweli. ....Hapo jiandae na majukumu mzeee....Anza kutega mitego ya pesa yanakuja mazito zaidi....
 
Mwambie bana, hiyo ndiyo faida ya ile raha ya dakika mbili za siku ileee.... ..
Hahahahaaaaa hiyo raha hata dakika moja haifiki ni vijisekunde tu ingefika dk 2 tungekuwa tunazimia kama siyo kufa kabisa maana ni tamu ile kitu balaaaaa.......
 
Tigga,
Duh inaonyesha wewe sio mvumilivu hata kidogo, nakusihi ujitafakari upya kama maisha unayoyaenda utayamudu. Kuna changamoto nyingi sana, sembuse hili. Mimi nilikuwa na case kama yako- kabla ya ndoa mchumba akapata mimba. I was extra extra extra happy. Baada ya wiki 2 sasa zile effect zikaanza- full kutapika, kichwa , kizunguzungu. Ila in all that i was happy. Alikuwa mama anatapika hadi anaishiwa maji na analazwa, mzee mzima nachukua off kumhudumia. alikuwa hapendi wageni, hapendi kelele, (tunanongonezana) etc. Ila nilimchukulia taratibuuuuuu. Akitapika nazoa , akitaka chakula ntatafuta, tena anaweza omba kuku-ukahangaika kumtafuta na ukimleta tu anasema sio kuku tena ni mbuzi !!! . Ukaribu wangu ulijenga sana mahusiano yetu , alipokuwa miezi 5 preg tukafunga ndoa.

Kwa hiyo kama unaona kutapika ni kujifanyisha ,bado kuna mengi. Maana akijifungua lazima usaidie kubadili nepi/pampers. Utabeba mtoto akilia, utamfulia hadi nguo za ndani akiwa bado mzazi.
Be responsible bwana.

Thank you very much. Sababu nampenda basi nafunga mshipi na kukaza uzi. Nitakuwa beneti zaidi na zaidi.
 
Sikujua kama wewe ni mwanaume,why umejiita Tigga?BACK TO TOPIC:msome Kongosho ametoa ushauri mzuri!

Tigga Mumba ni jina la kufikirika la starring kwenye hadithi inayoitwa MKIMBIZI. Mimi nilipenda ile character yake(plus hadithi yenyewe ilivyo-Thanks to Hussein Hassan Tuwa), ndio maana nikapenda nitumie jina hili.
 
Sina hakika kama unayetaka kumuoa kama ni mchumba tena, pia neno kutaka kuoa sina hakika kama lina nafasi tena hapa. Baada ya kuona title nilifikiri umegundua kwamba mchumba unayetaka kumuoa ana ujauzito ambao hujui mwenyewe....!

Kumbe ni wa kwako kwa mujibu wa uzi wako, hivyo huyo si mchumba tena ni mke na tayari umeshaoa unachojiandaa kufanya ni retrospective approval tu... (Yaani kuhalalisha yale uliyoyafanya kinyume cha utaratibu) na hili wengi tumepita hapa ila haipendezi. Kwa wale ambao hamjaharibu basi epukeni kabisa hili..

Kuhusu hali ya kutapika na kulegea-legea ni sawa hasa anapokuwepo mtu wa kumwonea huruma ambaye ndiye aliyesababisha hali hiyo ambaye ni wewe. Ila baada ya muda ikifika miezi 3 na kuendelea ata-stabilise tu labda anaweza kubaki na kutembea na kikopo au vitaulo kwa ajili ya kutemea mate tu.
 
ewaaaaaaah!
marhabaaah!
na huo ndo uanamume!
MWANAUME KIFUA KAKA!MWANAUME MAJUKUMU
MWANAUME KUJIREKEBISHA FASTA akihisi hayuko sawa mahala fulani!
uliza kaka na baba zako wadogo walivopata shida na vimimba vichanga vya wake zao Dark City hebu kuja kipande hii The Boss a bit of ue uzoefu iz needed here SnowBall hebu mueleze kijana wetu ile habari inakuwaje fabinyo we una uzoefu very recently hebu msaidie kijana Mtambuzi mzee mzima hebu waambie jinsi mama ngina alivokuwa anakutuma udongo ukileta anakwambia nilikutuma ubuyu alivokuwa na mimba ya King'asti C6 mwambie inakuwaje kulea kijacho wenu na charming lady
wakimaliza hawa utakuwa poa kabisa!

hahahaaa!!!wangu alikaa hosp miezi minne ya mwanzo,baada ya hapo akaingia kitaa ukimuona huwezi amini!!!ful kula mahindi ya kuchoma,kunusa viatu...acha tu!kwa ufupi hiyo ni kawaida sanaaaaaaaaaa,baadae atakuwa poa tu kijana!!ni PM ntakupa mauzoefu
 
ivi wewe unafikiri kubeba mimba ni kazi rahisi?hebu chukua jukumu la kumsaidia mwenzio,au uhamishiwe wewe uone kimbembe chake?hajifanyishi
 
Tigga Mumba ni jina la kufikirika la starring kwenye hadithi inayoitwa MKIMBIZI. Mimi nilipenda ile character yake(plus hadithi yenyewe ilivyo-Thanks to Hussein Hassan Tuwa), ndio maana nikapenda nitumie jina hili.

Wrong reason,usidhani Tigga sio jina halisi,ni sawa na angetumia Aisha au Halima,hilo ni jina halisi kabisa,usidhani kuwepo kwenye hadithi kunalifanya kuwa la kufikirika. . . . .Why don't u call yourself John Vata?
 
Nisingependa kuendelea kudiscuss hili maana mantiki ya thread hii ni kuomba ushauri kwa niliyoyasema. Jina nalitumia kama nilivyokujibu. Kama lipo kweli sawa, silitumii kama jinsia yake ila natumia kama character yake. Jaribu kusoma kitabu cha Mkimbizi na uone ambavyo usingedhani wala kufikiria jinsia ya huyo Tigga Mumba.
 
Nilikua nakuchallenge tu,hadithi hiyo nimeisoma hata mdunguaji pia na kitabu ninacho.Nafikiri unamkumbuka Kemirembe "the bastard" Wairema,Koku,baa ya Urno trabanjo,Kachiki,The rickshow n.k,but still hukutakiwa kutumia jina hilo!
 
Nawasalimia...
Mchumba ninayekaribia kumuoa(early next year) ni mjamzito wa miezi michache ya kwanza.

Mahari ilikwishatolewa, sasa tuko kwenye vikao vya harusi/sendoff.

Tatizo sasa;
dakika moja katapika.... Yani nahisi anajifanyisha..... Analegea akisimama kidogo eti amechoka.....

Hivi ni kweli ujauzito mdogo wa ki embryo unakuwa hivi? Sasa miezi 9 si balaa....

Hakukaliki!! Nahisi anazidisha kudeka.....

Wenye experience nisaidieni pls

kijana Tigga Mumba,kwanza hongera kwa kum-Togga Mimba mwenzako!swali lako ungeweza kupata jibu sahihi kwa mtu yeyote wa kwanza ambaye ungemuuliza huko kwenu,hapa umekuja kujaza server tu na kujichoresha kuwa una utoto ndani yako ilhali umekwisha anza kufanya mambo ya kikubwa!

niwe muungwana sasa nikupe jibu la swali lako,unapotia ujauzito jiandae na mambo mageni toka kwa mwenza wako ktk kipindi chote cha miezi tisa,iwe baada ya siku moja toka utie mimba au hata siku 2 kabla ya kujifungua!iite miezi tisa ya mpito na jiandae kwa lolote,na uwe pamoja na mwenzako ktk hali yoyote!mimba ni ya kwenu sio ya kwake peke yake,cheza nafasi yako vema!all the best
 
Asante kwa ushauri mtu mzima
 
Nawasalimia...
Mchumba ninayekaribia kumuoa(early next year) ni mjamzito wa miezi michache ya kwanza.

Mahari ilikwishatolewa, sasa tuko kwenye vikao vya harusi/sendoff.

Tatizo sasa;
dakika moja katapika.... Yani nahisi anajifanyisha..... Analegea akisimama kidogo eti amechoka.....

Hivi ni kweli ujauzito mdogo wa ki embryo unakuwa hivi? Sasa miezi 9 si balaa....

Hakukaliki!! Nahisi anazidisha kudeka.....

Wenye experience nisaidieni pls

kawaida sana, just love her more the way she is............
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom