Mchumba 'angu amemegwa halafu ka confess

Chichi cut your losses now and leave that woman.Ukishaoa na ukapata safari ya mwaka utasafiri kwa amani kweli?She told you only when you found out.You deserve better MAN!
 
Mzozoooooooooooooooooo!!! Unataka mashine mpya??? Then iweje?? we ukipata utakayoridhika nayo songa mbele siku hizi cha peke yako hakuna kaka wala hizo mpya nazo utasaidiwa tu wadau hawana uvumilivu sana....

Hahaha mimi sijasema nataka mpya...

nilisema tu kwamba mpya zipo nyingi tu hapa mjini. Mimi mda wa kuanza kutafuta mpya ulishapita ndugu yangu.

Afterall Tanzania ni nchi ya mitumba mitumba tu kwa hiyo hata hizo ambazo ni refubrished mbona kwema tu... as long as ni ridhiko la moyo.

Ila suala la kumegewa ndio gumuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!
 
Huyu binti kugawa uroda kwa wanaume 2 tofauti na wanajua kuwa jamaa amechumbia ni dalili za kuwa huyu binti atakuwa mama huruma aka jamvi la wageni au chakula cha wote au dada powa na mengine mnayo yajua.Hafai
 
Mama na mama mdogo wako wapi? nimekuwa nikisubiri ushauri wao lakini hamna, huenda hata hawapitii thread hii, i'm shouting mama and mama mdogo say something please!
 
Kwanza pole sana ndugu yangu,kama walivyosema wengine ndo ukubwa.Unakumbuka uwa tunaongea suala la kufanya maamuzi magumu kuwa ni moja ya sifa ya kiongozi imara,basi hapa ndo mahala pake.Ninavyofahamu mimi ndoa inahitaji sana uvumilivu lakini ni kosa kubwa sana kama utakubali kuanza kuvumilia tangu kipindi cha uchumba hasa katika suala zima la kukosa uaminifu.Jaribu kukubaliana na hali halisi,kitendo chako cha kujifanya huzioni halama za nyakati kitakukosti hapo baadae.Suala hili litakukosesha amani siku zote maishani mwako,HASA KAMA WEWE NI MWAMINIFU.
BELIEVE ME THERE ARE ALOT OF FISHING GROUNDS,GO ON FISHING.ALICHOKIUNGANISHA MUNGU MWANADAMU HAWEZI KUKITENGANISHA LAKINI KWA UZINZI UTENGANISHWA.

Ndoa si lelemama,inahitaji mtu unaemkubali na unamwamini,HAPO PALISHAINGIA LUBA NDUGU YANGU,HATA WE MWENYEWE UNAJUA HILO.ANGALIA USIJE UKAWA MJUKUU WA MAJUTO
 
wanasema "isiyokuwasha hujailamba"
sasa wewe chichi imeshakuwasha na wewe ndo umejua utamu au uuchungu wake, so maamuzi ya mwisho mi naona unayo wewe na sisi ni watazamaji coz bado haijatuwasha..wakati unamtongoza hukutushirikisha.

so mi naona mjadala ufungwe.
 
taratibu Mwana Mama... Wanikumbusha Kipindi Niko Kwa Mze Wa Shamba Pugu...

Huyo mzee alikuwa kiboko ya njia...mihogo kwenda mbele..usisahau mkwara wake kwamba anaweza loga mtu instantly......nakuenzi PUGU yetu...asante MTM kwa kumbukumbu hizi.

Chichi,

Hujammwaga tu huyo mchumba kiburudisho?
 
wanasema "isiyokuwasha hujailamba"
sasa wewe chichi imeshakuwasha na wewe ndo umejua utamu au uuchungu wake, so maamuzi ya mwisho mi naona unayo wewe na sisi ni watazamaji coz bado haijatuwasha..wakati unamtongoza hukutushirikisha.

so mi naona mjadala ufungwe.

Ni kweli Isiyokuwasha hujailamba..., lakini Mngojea masika shamba hata lilima!!! mimi nachohitaji si kuzungumzia nini kilichotokea na nini yule binti amefanya, nachohitaji kwa sasa ni kupata maoni, ushauri, wosia, nasaha,tambuzi,uzoefu,na hata tiba ya Ku OVERCOME THE FACT ndio maana nikaja hapa Barazani...... Ni hayo tu.
 
Sijui hata nianzie wapi..... Ni takribani mwaka wa pili sasa nipo nae, na ni mwezi wa pili mwaka huu nilimtambulisha kwa wazazi wangu na ndugu kadhaa kuwa huyu ni "mchumba wangu mpendwa niliyependezwa nae". Baada ya hapo maisha yakatuweka mbali takribani miezi mitano, lakini tulikuwa tukiwasiliana mara kwa mara... Chako ni chako tu, nilianza kuhisi mabadiliko kwenye mawaasiliano yetu na hiyo iliniumiza kichwa sana, Mungu si athumani siku isiyokuwa na jina nikapata kalikizo, nikaamua ku pay a suprise visit huko kwao...mengi yakatokea lakini la muhimu niligundua kuwa mwenzangu alianzisha mahusiano yasiyo rasmi kama mawili, akakiri kuwa ni kweli amemegwa na hao washkaji kwa muda tofauti... Iliniuma sana zaidi aliponiambia kuwa mmoja kati ya hao jamaa alikuwa anafahamu kuwa yeye ni mchumba wa mtu na wakala njama kuwa mimi nisijue, kumbe hata nilivyokuwa napiga simu au kutuma msg alikuwa na jamaa yake tena anaipumulia... Amejuta sana na anadai haelewi kwa nini ali kwenda astray, nimepima moyo wangu nimeamua kumsamehe kwani bado nampenda lakini nashidwa kuishi na fact kwamba jamaa kadhaa baada yangu wamepita... Na nikifikilia zile promises alizokuwa ananipa kuwa ananipenda na kamwe hawezi kuni hurt, zinanifanya nimuone Muongo kwa kila kitu.... Nisaidieni wajameni...

Daaaaang it... Pole sana faza.
Hili suala ni gumu sana..na ni wewe pekee mwenye kuweza kulitatua.
Ila kwa upeo nilionao kuhusu haya masuala......kuna msemo unaosema "Once a cheater,always a cheater". Itakuwa ngumu sana kuweza kumuamini tena,na kama hamna Imani au hutaweza kumuamini....kwa nini ujiumize kichwa kaka.
Maana hata akiwa kwenye simu na kaka yake uta panic.

Kwenye suala la kumpa mtu mwingine penzi(kumwegwa/kumega) hamna second chance hapo......kwa kuwa kila utakapokuwa sehemu na mpenzi wako na ikatokea na hao jamaa waliommega wapo hapo......hautaweza kuwa na amani.

The best thing is to MOVE ON. Kuwa kama alimegwa nje....ina maana basi haridhiki na mapenzi yenu,ndio maana akatafuta dudu nje.
Wanawake wako wengi tu ndugu yangu.....ni ngumu lakini inawezekana......endelea na maisha yako. Kupenda unaweza kupenda ukiupa moyo wako nafasi.
GoodLuck.
 
Ni kweli Isiyokuwasha hujailamba..., lakini Mngojea masika shamba hata lilima!!! mimi nachohitaji si kuzungumzia nini kilichotokea na nini yule binti amefanya, nachohitaji kwa sasa ni kupata maoni, ushauri, wosia, nasaha,tambuzi,uzoefu,na hata tiba ya Ku OVERCOME THE FACT ndio maana nikaja hapa Barazani...... Ni hayo tu.

dogo nakushauri tena nenda kapime ukimwi.
kama unao "u decide to hang ur gloves" na utuachie game wakongwe.
la kama huna nakushauri kwa sasa uachane na maswala hayo na ukazanie maswala yako ya maisha.
kama mwenyezi mungu akipenda baadae atakupa mke mzuri na mtazaa watoto wazuri wa damu yako na mtajenga familia iliyo bora na yenye furaha.

narudia tena achana na mademu wataakuumiza kichwa.
 
dogo nakushauri tena nenda kapime ukimwi.
kama unao "u decide to hang ur gloves" na utuachie game wakongwe.
la kama huna nakushauri kwa sasa uachane na maswala hayo na ukazanie maswala yako ya maisha.
kama mwenyezi mungu akipenda baadae atakupa mke mzuri na mtazaa watoto wazuri wa damu yako na mtajenga familia iliyo bora na yenye furaha.

narudia tena achana na mademu wataakuumiza kichwa.
Pole sana kijana kwa yaliyokukuta,jambo la kwanza nakushauri ukapime ukimwi na la pili achana na huyu binti kama si hivyo raha ya siku moja itakupa majuto ya daima
 
Ukiwa mkweli itakusaidia. honestly wakati wote ambao hamkuwa pamoja wewe umemega mara ngapi?
 
Izo kesi ni za kawaida now days,bse unaweza ata ulipokutana nae mara ya kwanza hata haukuwa bikira na mbona hukujiuliza if so.
Kuwa mpole take you time,mweke kwa probation ya mwaka mzima ukiangalia mwenendo wake baada ya hapo ndo ufanye uamuzi.
Otherwise kwa kuwa ameconfess kama ana akili timamu hatarudia tena.
Pole kwa yaliyokupata!
 
Ndugu yangu, kwanza kabisa mshukuru Mungu kwa kukufunulia hayo.
Kwa uamuzi wa kumsamehe umefanya vyema sbb Mungu ametufundisha kusamehe 7x70 hapo sawa lakini si kuwa uendelee nae mimi binafsi sikushauri hivyo hata kama unampenda kiasi gani.

Binafsi yaliwahi kunitokea na muhusika akaomba nimsamehe nikamwambia
sawa nimekusamehe, lakini bado akawa anaendelea kuomba msamaha. Aah nikashangaa nikamwambia mbona nilishakusamehe akasema sio hivyo yaani unisamehe na tuendelee na uhusiano wetu hahaha ukweli nilimpenda sana lakini nikampa BIG NO sbb kurudiana nae ni sawa na kuona shimo kubwa kwenye njia unayoiendea halafu unasema aah ntaruka tu wakati huwezi.
Matokeo yake ni kutumbukia na kujeruhiwa kama si kuangamia.
So my bro futa hiyo anza kwa upya! hakuzaliwa kwa ajili yako huyo waachie wenyewe.
Thanks.
 
Njowepo,
Umemshauri ampe probation ya mwaka mzima akimtazama mwenendo wake,
hivi unadhani atakuwa na kazi hiyo tu ya kumfuatilia mtu mzima na akili zake?
Pia kumbuka sisi wanawake ni wajanja sana, anaweza akamfuatilia nyendo zake na huyo bibie akaendelea na watu wake na huyo bwana asigundue lolote.
 
Ya kale hayo si kitu, kinachozungumziwa hapa nilichokielewa mimi ni kuwa na uhusiano tena uchumba halafu mmoja anakuwa cheater na si mambo ya zamani sbb hayo yalishapita. Na kama ni suala la kuangalia bikira basi tungeziuliza na zenu wanaume tuwatambueje kuwa nyie hmjawahi fanya hayo mambo (ngono)??????
Kama bikira zingepewa kipaumbele ndoa zisingekuwepo.
Ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya.
Ciao
 
MUACHE BRO,ONE MISTAKE ONE GOAL.
kumbuka.
Atakapo kuachia umeme atajuta pia na pia atakwambia hajui kwanini alienda astray na wewe pia itabidi umsamehe kwa kuwa utaupima moyo na kwa sababu bado unampenda lakini pia utashindwa kuishi na fact kuwa umeambukizwa na utakuwa ukifiria zile promise alizokuwa anakupa kwamba kamwe hawezi kukuhurt hutamouna muongo ila utajilaumu kwanini na wewe pia ulimpenda kwa kuwa yeye pia alikupenda.

that's always the price to pay for loving somebody too much.
 
Back
Top Bottom