Mchumba 'angu amemegwa halafu ka confess

Pole sana,kaka yangu.
Japo mimi ninamwelekeo mwingine kabisa wa ushauri.Na labda kwa hali ya kawaida unapaswa kutofautisha kati ya Mke ,mpenzi na Mchumba.Mpenzi na Mchumba inaruhusiwa kuachana katika aina mojawapo ya imani japo kuna tofauti ya imani.Lakini mke ukishaoana naye huruhusiwi kabisa kuachana naye.
Kweli tunapaswa kusameheana na kusahau sawasawa na moja ya imani.Lakini hata kama umeumizwa na kubaki na kovu bado kovu litakuwepo japo umepona.Ndivyo ilivyo kumsamehe mtu ni kweli sio rahisi kusahau kuwa mchumba wako ametembea na mwanaume mwingine.tena wawili tofauti na ambao hajatuambia afya zao zikoje.Je wote walipima????kwani siku hizi UKIMWI uko nje nje.Kweli hatupaswi kunyanyapaliana lakini tunapaswa kujikinga na maambukizi?Je wewe mwenzetu ulishatembeaa naye baada ya kurudi?je mmpepima kama ushauri unavyotuelekeza?NI MUHIMU.!!!!
baada ya hayo jambo lingine ni jinsi ya kushauriana na moyo wako.Je wewe huwezi kukosea?kama ndivyo je kama ingekuwa ni wewe je angefanyaje huyo mchumba wako?baada ya maswali hayo jaribu kujihoji mwenyewe endapo huyo anaweza kukufaa maishani wakati tayari ameshaonyesha kuwa sio mwaminifu.Je ikitokea tena utaweza kuwa bado na kifua?Kama laa bora kwa upendo kabisa mtafute huyo dada,kaaeni mjadiliane kisha toa maamuzi yako na maamuzi mazuri ni bora kuanza upya!!! yaani kumwomba Mungu akupe mke na sio mchumba.Mungu akikupa mke atakupa wa kufanana na yale unayoyatamani kwa mkeo na wewe pia Mungu atakubadilisha ili mkeo naye apate mume mwema wa kufanana naye.Hapo utakuwa na maisha ya ndoa yenye amani na uvumilivu wenye uaminifu.
 
Originally Posted by africa6666
Data: 50% ya wake za watu wanamegwa nje ndo maana 50% ya wana ndoa ni HIV ++ve

nadhani wanandoa wengi sio waaminifu.Na sio wanawake tu wanatembea nje ya ndoa naamini wanaume karibu 80%ndio wabaya kabisa na ndio wanasababisha migongano na wivu kwa wanawake wengi na kutokuaminiana na migogoro mingi yenye ugomvi mkubwa kwa ndoa nyingi kukosa uaminifu.Wanaume wengi wana nyumba ndogo ambazo zingine ni rasmi na zingine sio rasmi.Na ilivyo sasa hata wanawake hawahangaiki kuuliza kwani ni wanaume wachache sana ambao ni waaminifu katika ndoa zao pamoja na maradhi haya mengi yanayoendelea.
 
Muzeiya.huyo bwana ni tabia yake tu alikuwa anakuplay siku nyingi ila tu umembabatiza.Kama kakuput off,ushauri wa bure ni uchimbe for good.Usijali kama ulimtambulisha kwa wazazi au la.bora shari nusu kuliko shari kamili.atakuja kutembea mpaka na marafiki zako.take it from me
 
Jamani tusimdanganye ndugu yetu kuna adv na disad
mimi nimeoa na baada ya harusi nilikaa na mkewangu miezi 5 akaanza kumegwa
baya zaidi nilikaa nae uchmba miezi 24..baada ya kujua anamegwa nikanza kumega he akaamua kuwaplekea waliokuwa wanammega kule ireland..
Bada ya k urudi akasikia nampumulia rafiki yake wa karibu baadaye akujua aliekuwa akimpumulia nilisoma nae pale primary..ndipo mwanamke kikmwanza mara akasirike bilasababu mara anirushie maji ya moto...he

mwanawane nikaona isiwe tabu nkamuita nkauuliza unanidai hapana ndugu zako wananidai hapana hoo nilishukuru kwa majibu yale sikusita na kumwambia kila tulichochuma chako...akkaaa akakimbilia mahakamani

nikamshukuru mungu tena kwa mara ya pili kumbe alipata jibaab la ndoa yake inashake akamuahidi atamuoa..ajitahidi kupata talaka..nilimwambia mungu nikupe nini akajitahidi kuhonga na mahakimu ikatolewa ndani ya miezi 3..akaaendelea kupigwa na kuachika mpaka sasa anajaribu kuvuta nguvu ya kuja anashindwa.....ila alishangaa aliposikia kwamba niko na mwanamke wangu wa zamani ilibidi nikamlilie na tunaishi nae kama tunaelekea sayuni..jamani upendo na amani ni kitu kizuri katika mahusiano.

Wazo la kumshauri huyu ndugu ni kwamba kama amekuwa mbali kwa muda wa miezi 4-5 ana wawili jamani ni swalla la cross multiplication

miezi 5 bahasha 2

miezi 36(miaka 3) ???

Jibu utalipata....nakushauri ndugu usishindane na wanawake mwombe mungu akupe alietulia na wala usiangalie sana sura ya dhahabu mshukur mungu na zidi kuomba usikate tamaa kabisa...swala la kumwacha au la tunaomba uamue mwenye hakuna kitu kibaya siku ya siku ukaja na kichwa cha habari

walaaniwe wana jf wote na kutulist kisa walikushauri umwache...msaada wetu ni mmoja mwombe mungu akupe unaempenda usiongozwe na tamaa za mwili yaani just nampeda kweli jamani ,,,,utapenda majini ndugu

nami nitakuzidi kukuombea
salamu

'shaloom
 
Quote:
Originally Posted by africa6666
Data: 50% ya wake za watu wanamegwa nje ndo maana 50% ya wana ndoa ni HIV ++ve


..source of the data, please.



WEEEEEEEEEEEEEEEE USIOMBE UNAWEZA KUJUTA KWA NINI ULIULIZA NI NDEFU NDUG YANGU!!!
 
Pole mtu wangu, kama umesamehe sahau maisha yaendelee, kama huwezi kusamehe na kusahau lala mbele.... lakini jiulize na wewe je? vipi uaminifu wako kwake?
 
chichi demu wako kamegwa unataka nini tena? ACHANA NAE kumbuka hata ukimuoa lazima atamegwa tu............ACHANA na dala dala hilo 300 yako tu unapanda lingine.....
 
Sijui hata nianzie wapi..... Ni takribani mwaka wa pili sasa nipo nae, na ni mwezi wa pili mwaka huu nilimtambulisha kwa wazazi wangu na ndugu kadhaa kuwa huyu ni "mchumba wangu mpendwa niliyependezwa nae". Baada ya hapo maisha yakatuweka mbali takribani miezi mitano, lakini tulikuwa tukiwasiliana mara kwa mara... Chako ni chako tu, nilianza kuhisi mabadiliko kwenye mawaasiliano yetu na hiyo iliniumiza kichwa sana, Mungu si athumani siku isiyokuwa na jina nikapata kalikizo, nikaamua ku pay a suprise visit huko kwao...mengi yakatokea lakini la muhimu niligundua kuwa mwenzangu alianzisha mahusiano yasiyo rasmi kama mawili, akakiri kuwa ni kweli amemegwa na hao washkaji kwa muda tofauti... Iliniuma sana zaidi aliponiambia kuwa mmoja kati ya hao jamaa alikuwa anafahamu kuwa yeye ni mchumba wa mtu na wakala njama kuwa mimi nisijue, kumbe hata nilivyokuwa napiga simu au kutuma msg alikuwa na jamaa yake tena anaipumulia... Amejuta sana na anadai haelewi kwa nini ali kwenda astray, nimepima moyo wangu nimeamua kumsamehe kwani bado nampenda lakini nashidwa kuishi na fact kwamba jamaa kadhaa baada yangu wamepita... Na nikifikilia zile promises alizokuwa ananipa kuwa ananipenda na kamwe hawezi kuni hurt, zinanifanya nimuone Muongo kwa kila kitu.... Nisaidieni wajameni...

...Unauliza kama umechukia au la??? give me a break!
just move ahead with your life bila her.
 
kwa kweli kaka yangu kwanza pole sana kwa yaliyokukuta maana inaonyesha una moyo hadi umeamua akumsamehe, lakini umsamehe siyo suluhisho inaonyesha huyo mchumba wako hajatulia haiwezekani msichana ndani ya miezi mitano awe na wanaume wawili tofauti na ni mchumba wa mtu?, halafu wewe mwenyewe unasema inakuumiza sana huoni kwamba utaishi bila amani ya roho ? kuwa na amani na mpenzi wako ni kitu kizuri sana sidhani huko mbeleni kama atajirekebisha.
 
Jamani hivi inakuwaje usitulie tena kwa anaekupenda kala hasara huyo! Pole sana my dear! lakini wewe tambua kuwa mlamba asari harambi mara moja atarudia, kwa kuwa unampenda sana jitahidi kuongeanae kwa upole umueleweshe asicheze na maisha maana mwisho wa siku mtakuja kujuta wote! Anywy is a part of life lakini muambie asirudie tena msije angamia bure!
 
huko mbeleni ita ku cost ma bro, ni bora uanze moja! mwanaume yoyote kusamehe na kusahau ishu kama hii ni ngumu sana, kwenye ndoa angeachika huyo ijekuwa wewe uchumba? lakini na huyo mrembo nae miezi mi 5 tayari wanaume .
 
Wanawake wazuri wako wengi tu kwanini uhangaike na msaliti. kwanini uumize moyo wako bila sababu. Achana naye, tafuta wengine yeye aendelee na hao wanaommega, kwa sababu wameshakushinda uweze. Uking'ang'ania watamega hata akiwa mkeo
 
Wanawake wazuri wako wengi tu kwanini uhangaike na msaliti. kwanini uumize moyo wako bila sababu. Achana naye, tafuta wengine yeye aendelee na hao wanaommega, kwa sababu wameshakushinda uweze. Uking'ang'ania watamega hata akiwa mkeo

...Post of the Day
 
kaka mkubwa MPIGE CHINI huyo unamsamehe wakati roho inakuuma haina maana.......baaadaye roho si utakupasuka mjomba...........demu akitafunwa roho inauma sembuse mchumba.........kaka hata hivyo una roho kama KISIKI.
 
kwa kuwa umeshindwa kujiamulia ndo maana ukaja hapa, je ukiulezea umma kuwa ktk maamuzi yako uliamua nini?
kama vipi endelea naye halafu mufunge ndoa ila kwa sasa fanya booking taasisi ya Moyo waanze kukufanyia clinic therapy.
 
Back
Top Bottom