Mchumba 'angu amemegwa halafu ka confess

chichi

Member
Aug 15, 2007
27
7
Sijui hata nianzie wapi..... Ni takribani mwaka wa pili sasa nipo nae, na ni mwezi wa pili mwaka huu nilimtambulisha kwa wazazi wangu na ndugu kadhaa kuwa huyu ni "mchumba wangu mpendwa niliyependezwa nae".

Baada ya hapo maisha yakatuweka mbali takribani miezi mitano, lakini tulikuwa tukiwasiliana mara kwa mara... Chako ni chako tu, nilianza kuhisi mabadiliko kwenye mawaasiliano yetu na hiyo iliniumiza kichwa sana, Mungu si athumani siku isiyokuwa na jina nikapata kalikizo, nikaamua ku pay a suprise visit huko kwao...mengi yakatokea lakini la muhimu niligundua kuwa mwenzangu alianzisha mahusiano yasiyo rasmi kama mawili, akakiri kuwa ni kweli amemegwa na hao washkaji kwa muda tofauti...

Iliniuma sana zaidi aliponiambia kuwa mmoja kati ya hao jamaa alikuwa anafahamu kuwa yeye ni mchumba wa mtu na wakala njama kuwa mimi nisijue, kumbe hata nilivyokuwa napiga simu au kutuma msg alikuwa na jamaa yake tena anaipumulia...

Amejuta sana na anadai haelewi kwa nini ali kwenda astray, nimepima moyo wangu nimeamua kumsamehe kwani bado nampenda lakini nashidwa kuishi na fact kwamba jamaa kadhaa baada yangu wamepita... Na nikifikilia zile promises alizokuwa ananipa kuwa ananipenda na kamwe hawezi kuni hurt, zinanifanya nimuone Muongo kwa kila kitu....

Nisaidieni wajameni...

UPDATE ON THE 27th of June, 2012:
Nilisamehe kwa moyo wote, na tofauti na mwanzo nikajipa muda mwingi wa kukaa nae na kumshauri jinsi ulimwengu ulivyo na namna ya kuvishinda vishawishi, it seemed to have worked! A lot passed, uphills and down the valleys then we were blessed with a child mwaka jana na tukaanza maandalizi ya ndoa, literally ilibidi iwe October mwaka huu, lakini kilichotokea najuuuuta kumfahamu! all along she was playing at the background the very same old game. Na from nowhere akanipiga kibuti cha fukuza mwizi bila kosa lolote na bila kujali kuwa mimi ni baba wa mtoto wake and the little empire that we have created! it broke me to dust aisee, only knowing later kuwa she is pregnant with a man she was cheating with na njia pekee ilikuwa ni kutoka nduki, Maumivu niliyonayo can only be experienced not expressed, Inauma sana aisee, Inauma kuliko ilivyotokea mwanzo. I am done with Believing in Love. I AM DONE! THE GAME IS OVER.
 
Last edited by a moderator:
Wahenga walisema fimbo ya mbali haiuwi nyoka. Amua kusuka au kunyoa, lakini consider this a blesing in disguise, umefichuliwa mtu alivyo, kama unaamua kuendelea au kutua ngoma ni juu yako.
 
Sijui hata nianzie wapi..... Ni takribani mwaka wa pili sasa nipo nae, na ni mwezi wa pili mwaka huu nilimtambulisha kwa wazazi wangu na ndugu kadhaa kuwa huyu ni "mchumba wangu mpendwa niliyependezwa nae". Baada ya hapo maisha yakatuweka mbali takribani miezi mitano, lakini tulikuwa tukiwasiliana mara kwa mara... Chako ni chako tu, nilianza kuhisi mabadiliko kwenye mawaasiliano yetu na hiyo iliniumiza kichwa sana, Mungu si athumani siku isiyokuwa na jina nikapata kalikizo, nikaamua ku pay a suprise visit huko kwao...mengi yakatokea lakini la muhimu niligundua kuwa mwenzangu alianzisha mahusiano yasiyo rasmi kama mawili, akakiri kuwa ni kweli amemegwa na hao washkaji kwa muda tofauti... Iliniuma sana zaidi aliponiambia kuwa mmoja kati ya hao jamaa alikuwa anafahamu kuwa yeye ni mchumba wa mtu na wakala njama kuwa mimi nisijue, kumbe hata nilivyokuwa napiga simu au kutuma msg alikuwa na jamaa yake tena anaipumulia... Amejuta sana na anadai haelewi kwa nini ali kwenda astray, nimepima moyo wangu nimeamua kumsamehe kwani bado nampenda lakini nashidwa kuishi na fact kwamba jamaa kadhaa baada yangu wamepita... Na nikifikilia zile promises alizokuwa ananipa kuwa ananipenda na kamwe hawezi kuni hurt, zinanifanya nimuone Muongo kwa kila kitu.... Nisaidieni wajameni...


Toka umegundua hilo ni muda gani mpaka ulipofikia uamuzi wa kumsamehe?
Jipe muda na uzitafakari zaidi sababu zilizopelekea wewe kumsamehe.




.
 
Ndugu yangu kumbuka huyo ni mchumba si mke na hata kama umempenda mno na kuhisi huwezi kuishi bila yeye, kitendo cha kuingia kwenye ndoa huku tayari humuamini bado ita ku-cost sana kwenye ndoa yako na hutamuamini kamwe ingawa unampenda.

Ni busara kuachana na mchumba lakini si mke, kama ameweza kumegwa na hao jamaa sasa hivi wakati wa mapenzi ya uchumba je, mkiingia kwenye ndoa na kuishi miaka 5 ambapo penzi hushuka na kupanda?

Mimi nakushauri chukua kikombe cha chai au kahawa then kaa sehemu tumia akili yako yote, uwezo wako wote kupiga hesabu je bila yeye unaweza kuishi na kupata mwingine? kwani mchumba si mke. Historia hujirudia na wakati mwingine unaweza kujikuta umechelewa. Ila mwamuzi ni wewe.
 
Chakufanya nikukaa chini nakujiuliza mwenyewe maswali bila kujidanganya; Je, Bado unamwamini?? Kama umemsamehe lakini haumwamini achana naye utajitesa bure na utamtesa na yeye bure, utakaa bila amani kwakuwaza kuwa hiko kitendo kitajirudia, kama umemsamhehe na bado unamwamini basi sio mbaya uendelee naye lakini vile vile kua makini....
 
...tatizo ni kwamba, katika hiki kizazi kipya, 'wachumba' wengi wa sasa hasa mijini ndivyo walivyo!
 
Inategemea una "kifua' kiasi gani...maana utakutana nayo sana hapo mbeleni. Ingekuwa mimi ningemshukuru Mungu kwa ufunuo huo.....halafu mitini.....
 
Kaka anza......Hiyo ni tabia yake ndugu yangu,Wenzio tumeona hayo,na kama utamsamehe anaweza kujenga tabia ya kuondoa "uwezo wako wa kujiamini",na kila wakati ukajikuta mnyonge na hata lile utakaloona kwa macho ukadhani ni ndoto....Mapenzi ya sasa inabidi uwe muangalifu mno.Katika ktk hali hiyo,Zungumza nae na kila mtu ashike lake,Vinginevyo kila siku maisha yako yatakuwa ya wasiwasi.
 
...Kulingana na jinsi ulivyo elezea, anza moja Chichi.
...By the way, pole sana.

SteveD.
 
Unampenda na umeshaamua kumsamehe sasa sijui msaada unaoutaka ni upi hapa. Nahisi bado unaumia sana moyoni mwako kwa yaliyojiri kisogoni mwako na unatamani ungekuwa na courage ya kumuacha, zigo la maumivu limekuelemea ndio ukaamua kuja kulitua hapa barazani.

Nikuambie ndugu yangu, dawa ya hili suala ni ndogo sana- Na wewe nenda ukageme, tena ikiwezeka wewe kageme mara mbili ya idadi yake, you will be so suprised the difference it makes, you will regain urijali wako back and it will make you feel good about yourself na utajikuta umemsamehe jumla na kuzidi kumpenda mwandani wako zaidi, ila tu usisahau daluga mwanangu kwenye revenge mission yako, goodluck!

KKN
Senior Sexpert.
 
Mkuu Chichi pole sana... naona mafisadi wameingia mpaka kwenye 18 ya ndoa yako. If the best is possible good is not enough! Unayo nafasi ya ku-msend off mchumba wako kwa amani. Hiyo meli sidhani kama itafika salama ukiilazimisha kukatiza maji. .

Kwani Chichi ni kitu gani kinakufanya uhisi AMEJUTA SANA wakati ma-best wako TOFAUTI (sijui wangapi) wamekuwakilisha kumkoboa mara kadhaa... Hayo machozi ya demu yasikuchanganyanye wala nini.. hiyo ni sanaa na ni kipaji tu, what if usingegundua kuwa ana hako kamchezo!?.

Mtoe out, pateni dinner fresh, candle light na kamziki.. buy her a good gift na likadi likubwa la GOOD BYE, na wewe ukiweza hiyo fani hapo jitahidi TOA MATONE KADHAA ya machozi (au mguno wa huzuni) kuonyesha kuwa inakulazimu kuchukua hatua ya kuachana nae japo inakuumiza. Then mwache aende zake. Utafute mwingine.
 
Unampenda na umeshaamua kumsamehe sasa sijui msaada unaoutaka ni upi hapa. Nahisi bado unaumia sana moyoni mwako kwa yaliyojiri kisogoni mwako na unatamani ungekuwa na courage ya kumuacha, zigo la maumivu limekuelemea ndio ukaamua kuja kulitua hapa barazani.
Nikuambie ndugu yangu, dawa ya hili suala ni ndogo sana- Na wewe nenda ukageme, tena ikiwezeka wewe kageme mara mbili ya idadi yake, you will be so suprised the difference it makes, you will regain urijali wako back and it will make you feel good about yourself na utajikuta umemsamehe jumla na kuzidi kumpenda mwandani wako zaidi, ila tu usisahau daluga mwanangu kwenye revenge mission yako, goodluck!

KKN
Senior Sexpert.



Beh... hii ni jino kwa jino au dawa ya moto ni moto.... ! Kazi kwako Chichi, nakutakia mission accomplished salama.
 
Tafuta wawili ambao ni wazuri kuliko yeye na wewe wamege, halafu confess. Akikusamehe nawe msamehe ila ujue muendako ukimwi unaweza kuwa source ya kukatisha hayo maisha yenu ya ndoa.

Pole sana chichi.....
 
aliye msafi na akatize.
sina hoja juu ya malipo ya madhambi ni mauti na akutendae mtende, ila mwisho wa safari hiyo ni wapi. na jee Mungu tumemuweka wapi na kwa nini iliumbwa kusameheana.
kama ametenda kosa na ameomba msamaha ni jambo kubwa kusamehe, wewe utakuwa imara sana na mtawala mzuri wa familia yak o kamautasamehe, walioshauri naweutamtende dhambi ,jihadhari mana jino kwa jino angalia vyema kama alikugonga jino la kulia nawe ugonge hilo hilo na kwa mgongo ule ule nikiwa na maana ya impact.
bro langu nakuomba uwe msamehevu, hakuna mkamilifu na kama huo ni mtindo wake hata acha, usiharakife kufunga ndoa lakini usitende dhambi kwa kuwa yeye katenda. mpe muda na angalia mwenendo wake. maamuzi utafanya baadae mana wanasema kila muonja asali.
 
Chichi,

katika miezi mitano kamegwa na jamaa wawili tofauti kisha anaomba msamaha. Yaani alikosa ya kwanza, kisha akajumuisha na kosa la pili ndipo akaamua omba msamaha baada ya wewe kurudi kwa mda..!

si kwamba inasikitisha bali inauma...jaribu kumuuliza ni nini haswa alichofata kwa hao jamaa wengine, yaani mpaka kufikia hatua ya kuwaambia wewe upo lakini usijue... hakufai huyo!

mtapokuwa pamoja tena utawa na uhakika gani kwamba hayatatokea tena na yeye atakuwa anajua wazi kwamba anaweza samehewa.?

pima mazuri na mabaya, mapungufu yenu na kama unaweza ishi nayo kaza buti...ila dah wawili miezi mitano, ndoa itawaje? angalia usije ishia kujinyonga!
 
Tafuta wawili ambao ni wazuri kuliko yeye na wewe wamege, halafu confess. Akikusamehe nawe msamehe ila ujue muendako ukimwi unaweza kuwa source ya kukatisha hayo maisha yenu ya ndoa.

Pole sana chichi.....

Chichi,

hapa hata ukatafuta wanawake mia, wazuri kama malaika ukawamega haitapunguza maumivu ulionayo juu yake...labda kama mngekuwa mlikosana wewe ukatoka na hasira nae akaenda kumegwa!

I have been in that situation, maumivu zaidi ni pale mnapokuwa pamoja na unawaza mtu mengine alikuwa anapewa kama hivi...pengine zaidi! huchelewi kuta mwenzako kafikia hata Kutifua!!!

if you have a big heart brother stay but kama moyo mwepesi fanya mbio...imekata kwako sana tu!
 
Chichi,

Wewe katika hii miezi mitano umekuwa mwaminifu kiasi gani? kwa sababu wakati mwingine tunakuwa rahisi kunyoosha kidole wakati sisi pia tunapaswa kunyooshewa kidole. Just be honest with yourself na kama hujafanya lolote la ku-betray mapenzi yako kwake, then follow your heart. Kama ulitembea na mtu na yeye hajui unafikiri akijua utataka akuache au akusamehe? I think what you need to do no matter what the circumstance, follow your heart! Jinsi moyo wako utakavyokwambia ili wewe uwe na furaha then itabidi uufuate huo moyo unavyotaka. Ila kumbuka, Do unto others what you would have them do to you!!!!!
 
Ni kiasi gani cha muda mtu anahitaji kusahau... Tatizo lipo hapo natamani ningeweza kuchukua uamuzi tofauti, kwani tangu nilipojua nimekosa amani, the Body is willing but the Spirit is too weak, kifupi nampenda sana huyu binti, itz just i cant live with the fact kuwa kuna wageni walimtembelea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom