Tayar bint kamwambia jamaa kuwa anamwambia baba yake kwani nilimshauri hivyo... mwanaume kamjibu amwambie alafu waone kati ya yeye na mwanaume wazazi watamwamini nani
habari zenu
ninarafiki yangu wa kike anamchumba wake ilikua wafunge ndoa mwezi wa nne wazazi wa bwana harusi wamesema wamekosa hela hivyo itabidi isogezwe mbele mpaka mwezi wa saba .
Tatizo sasa bint anamimba mwez 1 wamejaribu kila njia kuwashawishi wazazi angalau waafanye mwezi wa tano ikibidi wasifanye sherehe kubwa baba ni mchungaji kakataa anasema asubiri hata kama ni mwez wa tisa.
Mwanaume kakataa kuwaambia wazazi wake ukweli alichosema bint atoe mimba kama hataki waachane akisha zaa atampelekea mtoto bint hana kazi anashindwa ataishije na huyo mtoto analia tu mi nimeshindwa hata nimsaidiaje nimeamua hili swala nililete kwenu labda mnaweza mshauri.
Samahanini kwa kuwachosha
^^
Yaani sijui mi nikoje, nisisikie nia ya mtu kutoa mimba.. Nachukia kuanzia miguu ya mtu mpaka masikio yake.
Nimeshindwa kuendelea
^^
yaan upo kama mimi huwa natamani niwaambie walaaniwe kabisa
^^
Starehe zenu wenyewe, adhabu apewe mwingine!
You won't leave this world unpunished !!
^^
Kuna huu Uzi uliletwa hapa baadaye akaja mwingine akiitwa i jack 1 malalamiko yake yakielikea kwamba yeye ndie mhusika. Juzi juzi hapa kaleta thread nyingine ya kutaka kunywa sumu na watu wakatoa pole na ushauri mwingi. maimatha tunataka mrejesho ushauri wetu ulisaidia chochote kwa huyo rafiki yako?
Wanatuchezea akili cos jack 1 ndo alileta hii story juzi kasema anataka kunywa sumu...Dada Suzy na shangaziwe wakaenda guest hko wakaleta mrejesho ile Jana asubuh kuwa jack yupo salama hko arusha...