Mchumba anasema atoe mimba

maimatha

Senior Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
129
Reaction score
162
Habari zenu

Ninarafiki yangu wa kike anamchumba wake ilikua wafunge ndoa mwezi wa nne wazazi wa bwana harusi wamesema wamekosa hela hivyo itabidi isogezwe mbele mpaka mwezi wa saba .

Tatizo sasa bint anamimba mwez 1 wamejaribu kila njia kuwashawishi wazazi angalau waafanye mwezi wa tano ikibidi wasifanye sherehe kubwa baba ni mchungaji kakataa anasema asubiri hata kama ni mwez wa tisa.

Mwanaume kakataa kuwaambia wazazi wake ukweli alichosema bint atoe mimba kama hataki waachane akisha zaa atampelekea mtoto bint hana kazi anashindwa ataishije na huyo mtoto analia tu mi nimeshindwa hata nimsaidiaje nimeamua hili swala nililete kwenu labda mnaweza mshauri.

SAMAHANINI KWA KUWACHOSHA
 
Binti akamwambie baba mkwe kuwa ana mimba, wanachohitaji ni ndoa, si sherehe ya harusi.

Huyo mume mtarajiwa naye kiazi, akchwale binti kala garasa la maana. Kwanza kakubli baba amfanyie maamuzi ya ndoa ifungwe lini, pili kumshawishi binti atoe mimba.

Between the line hii ndoa ipo matatani sana, sijui kama itatokea. Binti katoswa ki utu uzima hivyo.
 
^^
Yaani sijui mi nikoje, nisisikie nia ya mtu kutoa mimba.. Nachukia kuanzia miguu ya mtu mpaka masikio yake.
Nimeshindwa kuendelea
^^
 
Mtoto wa zinaa..

Mchungaji ataamua nini? Vs biblia inasemaje?

Swali la kiafya,

je mimba ikitolewa, binti atakuwa na hali gani!? Je, ikiwa ndio mwisho wa maisha yake ya kuzaa watoto itakuwaje?

Je akifa? Hali itakuwaje?

Hii hali ni tete!

Wazazi wa pande zote mbili inabidi wakae chini wajadili mustakabali wa maisha ya watoto wao kiujumla.

MWENYEZI MUNGU ASHIRIKISHWE KIUNDANI KABISA!
 
Tayar bint kamwambia jamaa kuwa anamwambia baba yake kwani nilimshauri hivyo... mwanaume kamjibu amwambie alafu waone kati ya yeye na mwanaume wazazi watamwamini nani
 

Wazazi wote hawajui kama bint anamimba ndo maana jamaa analazimisha mimba itolewe
 
People are so obsessed with sherehe...kwa nini?
Kuna njia nzuri sana hapo, fungeni ndoa, nendeni kanisani na mashahidi wenu, anzeni maisha, sherehe yaweza fanyika hata miaka kumi ijayo...no big deal..
Baada ya miaka kumi mnafanya sherehe nzuri. tena watoto watafaidi sana kumuona mama ndani ya shela...

Why are pips so obsessed with sherehe eeh!!!!!!!!
 
kama atamwacha sababu ya kutotoa mimba bac hampend so awe na msimamo ndoa hailazimishwi.
 
huyu mchungaji hajui maana ya ndoa kwanza..... binti na mwanaume wachukue hatua ya kufunga ndoa hata ya serikalini ili mradi tu ni ndoa..... hizi ndoa za masherehe makubwa hayana maana kabisa ndo maana yanavunjika mara kwa mara........ hizo hela wanazosubiria kupata wampe binti afanye biashara
 

because they want to impress their friends and relatives... this is stupidity thing in people mind
 
 
Nyumba za watumishi zimepigwa sana kupitia watoto wao... ivi kwa nini lakini?

Mtoto wa Mchungaji ndio anapiga Debe akauwe kiumbe kisicho na hatia ili aonekane mtu mwema, ili afiche aibu.... Hivi kweli unakusudia KUUA ili uonekane na waovu wenzako kama akina sie tu huku? Unafiki utatupelea pabaya sana... kila mtu anawajibika kwa matendo yake... HUWEZI KUWA MTU WA MAANA KWAKO NA KWA WENGINE KAMA HUTAKI KUWAJIBIKA KWA MATOKEO YA MATENDO YAKO MWENYEWE...

Sasa mshauri huyo binti aongee na huyo jamaa ili wakamwambie baba yao (Mch) binti akienda mwenyewe kabla hajamshirikisha huyo jamaa italeta shida kubwa zaidi na zaidi kati yake na huyo mumewe mtarajiwa. Kwa kuwa wakweli njia itapatikana.
 
because they want to impress their friends and relatives... this is stupidity thing in people mind
Kweli nashindwa kuelewa, watu wanataka makuu ilhali uwezo wao mdogo. Kwani ndoa lazima iwe na sherehe ya watu 500!!!
 
Mwambie wakafunge hata ya Serikali hafu wasifanye sherehe, yanini ugharimike wakati pesa huna?

 
Kweli nashindwa kuelewa, watu wanataka makuu ilhali uwezo wao mdogo. Kwani ndoa lazima iwe na sherehe ya watu 500!!!

baada ya hapo wanaanza kulipa madeni huu ni ulimbukeni tu....... kijana na binti mshahara laki 4, shererhe ya milion 15........ukichanganya mishahara yao kwa mwaka mzima ni million 9 na laki 6 .... huu si upumbavu hapo ukijakuona saving yao kwa mwaka incase wanajiatahidi wanasave 1/3 ya mishahara yao kila mwezi kwa mwaka watasave milion 3 na laki 2..... nyambafu kabisa huyu kijana..

hizo hela wawe wanawapa watoto wao kufanyia biashara wakishajichangisha
 
Hapo no way ukweli tu ndo utawaweka huru,kama kijana amemtishia asiogope na asifanye dhamb juu ya dhambi,awaeleze wazaz wake ukwel kisha waende wakamwambie wazaz wa mwanaume,asijaribu hata kdogo kutoa mimba na wala asikubal kufa nalo moyon,km mwanaume atamruka bas lkn atleast ukwel utamweka huru,na asisahau kuomba toba na rehema za Mungu.
 
 
Kwahiyo dada anatakiwa achague kati ya mimba(Mtoto) ndoa.

Mwambie aangalie kipi anadhani kitampa faraja baadae, huyo mwanaume anaemlazimisha kutoa mimba bila kujali utu na madhara yanayoweza kumpata huyo dada au katoto kasiko na hatia. Akae akijua hiyo ndoa haitompa furaha na huyo bwana hampendi kwahivyo unless yupo tayari kujitoa muhanga aangalie ustaarabu mwingine.

Kheri nusu shari kuliko shari kamili.
Awaeleze wazazi wake na wa kijana wamsaidie kulea mimba maisha yaendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…