Mchina wa miaka 16 avunja record London.

USA ndo wameshika bango sana eti apimwe. Bad losers!

Wamarekani bwana, kushinda washinde wao, akishinda mwingine kanywa dawa! Yule Phelps (not sure na spellings) walikuwa wanachekelea, wakicheka wengine wanapiga kelele!
 
Muda wa maandalizi siye tunapiga ulojo, wakati wa mavuno tunabaki kushabikia kama hivi!! hatuna mipangp mizuri kazi kulia tu mitaji ya kufanya project kubwa hatuna, mara Oooh nchi yetu haijulikani sana ndiyo maana watalii hawaji!! Utangaza vipi nchi kama hujitumi kwenye inshu kama hizi? Utajulikana vipi duniani kama huna cha kuonyesha au huna unachoweza kufanya? Nani atapoteza hela kuja kukuona wewe wakati hakujui unachoweza nini? Ni full usanii tu mwanzo mwisho, kuanzia ikulu hadi kwa m/kiti wa mtaa au balozi wa nyuma kumi (ccm).

Mafanikio ya michezo kimataifa kwa nchi nyingi zinazoongoza kwa medali ni michezo mashuleni ndio chimbuko. Miaka iliyopita enzi za akina Filbet Bay ni matunda ya michezo iliyoanzia mashuleni kisha kuendelezwa majeshini. Leo hii shule zetu wanafunzi legelege hata msamiati wa mchakamchaka hawajui maana yake nini sembuse gwaride ya kuendeshwa kwa band master mwenye kuwakoga watu kwa umahiri wa kuringa na stick? Tunachomoa wacheza chandimu ati waende olimpic kushindana na hawa ambao tangu utotoni wamefanya makubwa?
 
Wenzetu wapo kikazi zaidi sio sisi tunapeleka timu kwenda kushangaa watu na mafataki':..matokeo yake hatutarudi na medali hata moja labda kama zipo za medali za mchanga!

Wakianzisha Olympic za mikataba mibovu hakuna atakaye tuweza
 
Mafanikio ya michezo kimataifa kwa nchi nyingi zinazoongoza kwa medali ni michezo mashuleni ndio chimbuko. Miaka iliyopita enzi za akina Filbet Bay ni matunda ya michezo iliyoanzia mashuleni kisha kuendelezwa majeshini. Leo hii shule zetu wanafunzi legelege hata msamiati wa mchakamchaka hawajui maana yake nini sembuse gwaride ya kuendeshwa kwa band master mwenye kuwakoga watu kwa umahiri wa kuringa na stick? Tunachomoa wacheza chandimu ati waende olimpic kushindana na hawa ambao tangu utotoni wamefanya makubwa?
This is a critical issue kwakweli!! Tunakosea mno kuanzia kuteua mgombea urais, ubunge, waziri ndo kabisaaa! Mtu atakuwa vipi na uelewa kama hajafikia hali za walio wengi na kuwa na fikra za kimapinduzi ambapo moja ya eneo la kukuza mitaji ya ndani na kuitangaza nchi ni hii ya dezo dezo inayotegemea nguvu na bidii ya mshiriki. Tungekuwa na vichwa kama Candid Scope kwenye hizo nafasi nyeti naimani tungekuwa tumesharudisha uzalendo ndani ya hii nchi. Watu wangekuwa wako tayari kufa kwa ajili ya nchi yao kwa jambo dogo tu!! Sasa ni mpaka tumtoe nyoka chumbani, tujipange upya, tuweke mzalendo wa kweli anayeweza kuwa na hisia za watanzania wanaohitaji kupewa muongozo wa nini kifanyika kutoka A - Z.
 
Back
Top Bottom