Mchina ampiga Ofisa Uhamiaji, kazimia

Mchina ampiga Ofisa Uhamiaji, kazimia

Halisi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2007
Posts
2,802
Reaction score
617
Mchina mmoja YUXIAN WENG hati ya ukazi RPA O31266 ISSUED DSM 28.7.2O1O amempiga afisa Uhamiaji cpl Mussa Mkubwa Abdallah wa Ilala hadi umepoteza fahamu hadi sasa. Amepelekwa Muhimbili Hospital na hajapata fahamu. Taarifa zinasema POLISI mmoja amekua akiwalinda Wachina hao anaitwa W.KABEMBERA ASST. INSP.
 
Huyo Mussa Mkubwa Abdallah ana umri gani? Manake kama ni kijana (chini ya miaka 60) nitamlaumu kwa nini hakupigana na huyo Mchina.

Mimi siwezi nikapigwa na mtu. Tutapigana. Hata kama ukinishinda lakini lazima nikutoe damu sehemu.
 
Hilo jina la huyo Afisa linaashiria ni "mla urojo", huenda alikuwa "unfit" wakati wa pambano au "aliviziwa".
 
Na huyo Mchina kampigia wapi huyo jamaa?

Kwa kweli bado haiingii akilini mwangu. Mtu utapigwaje bana? Kwa nini usipigane?
 
ya wezekana alitaka kumchakachua mchina akaona haiwezekani,au katika inshu za uraia waliaidiana kupeana rushwa mchina kashutuka kamchenjia
do! ange mgonga mtu kama jairo
 
police case. ndugu wanaweza kufuatilia kabla mchina hajatoweka hasa kuhakikisha yuko ndani kutokana na hali ya mgonjwa.
 
taarifa iko wazi mno kiasi kwamba inaonekana jamaa alimwacha mchina kumpiga hadi kupoteza fahamu ni muhimu tukapata ufafanuzi ili taarifa isimame vizuri na kuonekana ina ukweli.
 
Mchina mmoja YUXIAN WENG hati ya ukazi RPA O31266 ISSUED DSM 28.7.2O1O amempiga afisa Uhamiaji cpl Mussa Mkubwa Abdallah wa Ilala hadi umepoteza fahamu hadi sasa. Amepelekwa Muhimbili Hospital na hajapata fahamu. Taarifa zinasema POLISI mmoja amekua akiwalinda Wachina hao anaitwa W.KABEMBERA ASST. INSP.

Wachina wana tudharau sana kwa sababu wanajua tunahongeka kwa fedha ndogo tu.
Arusha alipigwa OCD vibao, wachina wakahonga yakaisha.
Watatupiga na hawatachukuliwa hatua yoyote.
 
hata watanzania kwa watanzania wanaweza kupigana hadi mmoja akapoteza fahamu. kwanza tuondoe shaka ya ubaguzi na tujue alimpiga kwa sababu ya uafrika wake au kuna kitu hakikuenda sawa hadi wakaingia katika ugomvi ambao ukaisha kwa mswahili kupigwa.
 
waache wapigwe hao watu wa uhamiaji maana mtz ukienda hapo wanakuangalia tu lakini wakiona ngozi nyeupe wanaipa huduma haraka
 
tukitanguliza hoja ya ubaguzi hatutapata ukweli mbona kuna watanzania wamewahi kupigana hadi mmoja kumuua mwenzake?
 
Aliyepigwa hadi kupoteza fahamu inawezekana ni wale jamaa zetu wa CUF toka Pemba.
 
kila binadamu ana mwisho wa subira, ni busara tukajua kwa nini mchina aliishiwa na subira na kufanya jambo ambalo halina utu wa binadamu
 
Na huyo Mchina kampigia wapi huyo jamaa?

Kwa kweli bado haiingii akilini mwangu. Mtu utapigwaje bana? Kwa nini usipigane?

wabongo wanadhana kwamba kila mchina anacheza kong fu! .. kumbe wala sio kweli.. hata mimi jamaa namuona mpuuzi apigwe hadi apoteze fahamu!

mwanaume unapigana ukizidiwa unakimbia ...

Na huyo Mchina kampigia wapi huyo jamaa?

Kwa kweli bado haiingii akilini mwangu. Mtu utapigwaje bana? Kwa nini usipigane?
Hiyo ndio serikali lege lege ya JK watendaji wake wote ni lege lege,hata ukimsukuma tu anazimia je ukimtwanga ngumi si anakufa kabisa.
 
wabongo wanadhana kwamba kila mchina anacheza kong fu! .. kumbe wala sio kweli.. hata mimi jamaa namuona mpuuzi apigwe hadi apoteze fahamu!

mwanaume unapigana ukizidiwa unakimbia ...

Kung fu za kwenye sinema haziko applicable katika street fighting. Kwenye street fighting hakuna cha babake kung-fu wala mamake karate.

Kwenye street fighting anything goes...vitofa, vyupa, vipisi vya mbao, kung'ata, kubinya kende, kurusha viti, na hata kukimbia kumo. Sielewi kabisa hii dhana ya huyo afisa uhamiaji kupigwa hadi apoteze fahamu.

Ina maana hakuwa na wenzake hapo alipopigiwa? Kama wenzake walikuwepo kwa nini hawakumchangia huyo Mchina? Au achana hata na kumchangia, kwa nini hawakuamulia mapema?

Miafrika bana....daaaah.
 
Back
Top Bottom