Mchezo wa mia kwa mia (100/100)

Mchezo wa mia kwa mia (100/100)

Mr. BK

Member
Joined
Aug 6, 2014
Posts
99
Reaction score
35
Wana jamvi kuna kamchezo kadogo tukikacheza kwa pamoja kanaweza kuwa kazuri.

Pamoja na kuwa ID zetu hazitutambulishi kuwa ni Me au Ke lakini mchezo huu huchezwa kwa kufuata jinsia,
Sheria zake ni nyepesi mno kama ifuatavyo
Kama wewe ni mwanaume ( Me) utatumia alama kujumlisha (+)
Kama we ni mwanamke (Ke) utatumia alama kutoa (-)
Mchezo utachezwa kama ifuatavyo.
Naweka namba ya kuanzia ambayo ni 100.
Mwanaume atakuwa akipost namba kwa kujumlisha moja kwenye namba utakayokuta imepostiwa tayari.
Mwanamke atakuwa akipost namba kwa kutoa 1 kwenye namba aliyokuta imeishapostiwa tayari
Mfano: 100
Me: 101
Me: 102
Ke: 101
Ke: 100
...................
Angalizo
Haitakiwi kuposti post zako mwenyewe zikafuatana:
Mfno: Ksf (mtu) 105
Ksf (mtu) 106
.................................
Mchezo utachezwa kwa interval ya 100 steps ahead to each direction. Wanaume wakiipandisha hiyo digit (100)
Ikafika 200 watahesabika washindi kadhalika wanawake wakiishusha hiyo digit (100) ikafika 0 watahesabika washindi.

Lengo la mchezo huu ni kuleta ushindani tu wa kimchezo kwa jinsia, na pia kujiburudisha wenyewe.
Karibuni wote
 
Back
Top Bottom