Mchezo wa Kiduku Unavyowadhalilisha Wanaume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchezo wa Kiduku Unavyowadhalilisha Wanaume

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Boflo, Apr 23, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mchezo wa Kiduku Unavyowadhalilisha Wanaume
  [​IMG]
  Mtoto wa kiume akiwa amevaa kanga akikata mauno katika mashindano ya KIDUKU yaliyohudhuriwa na mamia ya watu Friday, April 23, 2010 12:14 AM
  Fainali ya mashindano ya kucheza mtindo wa taarabu unaoitwa KIDUKU ambao vijana wa kiume huvaa nguo za kike na kukata mauno kama wanawake itafanyika mwanzoni mwa mwezi ujao huku shutuma kali zikiwaendea waandaaji wa mashindano hayo kuwa wana malengo ya kuwaharibu watoto wa kiume. Mtindo wa KIDUKU uliobuniwa na mtangazaji mahiri aliyekuwa akitangaza
  katika kituo cha televisheni ya Afrika Mashariki EATV, Maimartha wa Jesse umekuwa gumuzo katika jiji la Dar es Salaam, kutokana na jinsi mchezo huo ulivyo wahusisha vijana wenye umri chini ya miaka 18.

  Wengi wa vijana huwa ni watoto wa shule za msingi na sekondari wengine wakitokea tu mitaani kushindana kucheza mchezo wa Kiduku.

  Hivi karibuni Maimartha aliandaa shindano la kumtafuta bingwa wa kiduku mwaka 2010 ambalo limewashirikisha vijana toka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

  Miongoni mwa vikundi vinavyoshiriki ni Vidoleki, Mazombi, Wanaume fasti, Wakali wa kitengo, Wakupoteza, Stavanga na Mazombi.

  Katika shindano hilo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya dola 250, mshindi wa pili atapata music system na watatu ataambulia feni. Fainali ya mashindano hayo itafanyika Mei 2 mwaka huu katika ukumbi wa Travertine uliopo magomeni.

  Hata hivyo shindano hilo wengi wamelibeza kutokana na kuonekana linawadhalilisha watoto wa kiume hasa hasa wanafunzi ambao huingia kushindana wakiwa wamevalia sare za shule.

  Kwa upande mwingine wapenzi wa muziki wa taarab wamekuwa na maoni tofauti kutokana na vijana hao kucheza huku wakiwa wamevalia nguo za akina dada jambo ambalo wengi wanalihisi kuwa linaweza likawa ni njia mojawapo ya kuwapotosha vijana hao kwa kujiingiza katika njia ya uasherati ikiwa ni pamoja na kuwa mashoga.

  Mmoja wa wazee aliyehudhuria katika mojawapo ya mashindano haya [Jina Kapuni] alisema kuwa wizara ya utamaduni, burudani na michezo inapaswa kuangalia na kupitia baadhi ya mashindano kama haya.

  "Mashindano haya yalipaswa yawahusishe wanawake na si watoto, lingine angalia ndugu mwandishi vijana wanakesha hapa na wanakuja na sare za shule zao inamaana wakitoka hapa wanaunganisha kwenda shule je watasoma nini huku wakiwa na usingizi?", aliuliza mzee huyo.

  Wadadisi wa mambo wameomba mchezo wa Kiduku usiwahusishe watoto wa kiume la sivyo vijana hao watakuwa mashoga kwani sehemu kama hizo huhudhuriwa na mashoga ambao wamekuwa wakiwarubuni vijana hao kwa vijisenti vidogo pia sehemu kama hizo ndizo zenya makuadi wa kutafuta vijana wanaotaka kwenda na wakati kwa kufanya mapenzi kinyume na maaumbile yao.

  Mei 2 mwaka huu ndio fainali ya kumpata bingwa wa kucheza KIDUKU.
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  :bump2::bump2:We hushiriki kwani ndo fani zenu
   
 3. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  nimeachana na hayo mambo........mimi ni janadume la haja
   
 4. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Im happy 4 u Bolfo:hug:
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kwani sheria za tanzania zinasemaje? mtoto wa chini ya miaka 20 si haruhusiwi kuingia club? (au huo umekuwa categorized kuwa ni ukumbi?)

  wanawake watu wazima walojaa ambao wako ready kufanya chochote unashindwa kuwahusisha na upuuzi huo unaenda kutafuta watoto? wanaume? umekusudia kuwafunza nini?
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kiduku
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sheria za Tanzania haziruhusu mtu akatazwe kufanya usanii ilimradi havunji sheria zilizopo. Huo ni usanii kuburudisha watu na kujiongezea kipato. Maimatha anastahili pongezi kwa ubunifu wake. Kila kitu kikitumiwa vibaya hudhalilisha, lakini kikitumiwa vema huleta heshima. Kuwowa sio kitu kibaya, lakini ukiwowa hadharani unajidhalilisha na unaidhalilisha jamii. Hao vijana walaa!
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kubinika ungefurahi mwanao wa kiume kwenda kucheza kiduku kwa kugombea dola 250?

  tanzania we have a long long way to go
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Jamii isiojali utu utaijua tuu..Ukiangalia larger picture utabaini tatizo lipo hasa kwenye jamii yenyewe kutaka mambo marahisi na shortcut ya kupata fedha za haraka haraka, in the process bila kujali kaa jamii inafaidika au la, na fmatendo yetu ya leo yata-affect vipi future yetu na vizazi vyetu. Na viongozi wetu ilimradi kitu hakiwagusi matumbo yao they will allow everthing else regardlessly..Hii ndio anarchy society.
   
 10. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mi sioni tatizo lolote wacha watu wabuni mbinu za kupata kipato,labda hao watoto wa shule wanatakiwa waondolewe ila kwa upande mwingine hakuna tatizo
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Mie picha sijaipenda hata kidogo naona ni dhahiri kweli mchezo sio mzuri
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  angalia avatar yako mkuu naamini umejiongelea na wete pia
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,449
  Likes Received: 22,367
  Trophy Points: 280
  jamani bwabwa a.k.a boflo aende huko akaonyeshe kipaji
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  guilty as charged..btw..kiduku ni usanii nd.msanii? sounds to me ni machezo ya mashoga.
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  ugumu wa maisha ndio unasababisha yote hayo.
   
 16. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  hehehehehe wanaume? eeeh!
   
 17. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Thumbs up....
  :A S thumbs_up:


  WTF is this? watu wameshidwa kutumia brain and show us some creativeness? This should be banned, ppl shouldnt entertain this..
   
 18. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  sherehe kubwa inafanyika mbinguni, malaika kwa furaha wanaimba wakisema 'aliyepotea tazama ameonekana,mwana mpotevu ameiona njia na kurudi nyumbani kwa baba yake'
  hureeeeee!
   
 19. bht

  bht JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  kupenda reeereeeee

  maisha yalikuwa na yataendelea kuwa magumu kwa hiyo tu-justfy tu upuuzi kwa kisingizio maisha magumu.

  kupenda mteremko ndo shida yetu (just like DECI n the like)

  Mai unachokifanya haipendezi wala kustahili sifa............ni vile tu huna uchungu na hao vijana...

  u are as selfish as most of us!!!
   
 20. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  haya mashindano hayakubaliki kabisaa!inasikitisha,wanatuharibia ndugu zetu,ndio nini hiyo eti watoto wakiume wavae mavazi ya kike wakate viuno,no way labda maimartha aseme mabasha wamemuomba awaandalie hili shindano!hayafai yanatakiwa yapingwe vikali!
   
Loading...