Mchezo wa kibaba baba na kimama mama hatarini kupotea

Poker

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
5,304
14,176
Nina siku ya 4 hapa A-town almaarufu Arachuga ila katika zunguka zunguka yangu mitaani sioni watoto wakicheza michezo hiyo zaidi ya playstation. Jamani wazazi nitoe wito au rai kwenu huu mchezo ni muhimu sana kwa jamii yetu, acheni uzungu wa kuwapa watoto michezo ya playstation na kwenye simu.

Maana sisi ndio imetukuza na jana nimemuona mzazi akimchapa mwanawe kisa ameenda kucheza ukuti ukuti wa nani wa nani, kagongwa na gari, tumpeleke mnazi mmoja...

Leo nitaandaa mchezo wa kula mbakishie baba wale wa Arusha mkuje tuungane kuucheza ili michezo yetu ya kiafrika isipotee jamani! Na pia msiwafungie huko geti kali mnawaaribu kisaikolojia.
 
Huenda hawachezi hiyo nao wana michezo yao mipya.

Ila kina junya wao ni simu na playstation na huwez wabadilisha dad na Mom eti wamruhusu junya akacheze nje si rahisi.
Huoni ule uafrika wetu unapotea kwa kasi sana?
 
Nina siku ya 4 hapa A-town almaarufu arachuga ila katika zunguka zunguka yangu mitaani sioni watoto wakicheza michezo hiyo zaidi ya playstation...
Bila hii michezo inatutengenezea vijana wa jamhuri ya vizazi vya hovyo mkuu hii michezo ilitufanya tusiishi kizembezembe km watoto wa sa hv
 
Daa kombolela nakumbuka nilienda jificha na binti mmoja sa hivi ni mama wa watoto watatu ... Hatukuonekana Hadi kesho yake ilifika muda ni too late Kila mtu akaenda tu kwao
 
Nina siku ya 4 hapa A-town almaarufu arachuga ila katika zunguka zunguka yangu mitaani sioni watoto wakicheza michezo hiyo zaidi ya playstation. Jamani wazazi nitoe wito au rai kwenu huu mchezo ni muhimu sana kwa jamii yetu, acheni uzungu wa kuwapa watoto michezo ya playstation na kwenye simu.

Maana sisi ndio imetukuza na jana nimemuona mzazi akimchapa mwanawe kisa ameenda kucheza ukuti ukuti wa nani wa nani, kagongwa na gari, tumpeleke mnazi mmoja...

Leo nitaandaa mchezo wa kula mbakishie baba wale wa Arusha mkuje tuungane kuucheza ili michezo yetu ya kiafrika isipotee jamani! Na pia msiwafungie huko geti kali mnawaaribu kisaikolojia.
Acha ipoteetu wengine ndy michezo iliyo tufunza uhuni
 
Back
Top Bottom