Wonderful
JF-Expert Member
- Apr 8, 2015
- 7,347
- 5,985
Mcheza kriketi maarufu wa West Indian amelambwa faini ya pauni 4,900 (zaidi ya Sh million 15) katakana na kitendo chake cha kuomba ‘mtoko’ kwa mtangazaji wa like wakati akihojiwa.
Chris Gayle amekumbana na faini hiyo, baada ya kumuambia mtangazaji wa runinga kwamba angependa watoke pamoja kwa ajili ya kupata kinywaji pamoja kama wangefanikiwa kushinda mechi hiyo.
Gayle pia alimueleza msichana huyo mwandishi Mel McLaughlin kuwa alikuwa akitafuta nafasi ya kuona macho yake. Baadaye akamsisitizia kwamba hakuwa na sababu ya kuona haya.
Lakini baadaye alilazimika kuomba radhi kutokana na kitendo hicho ambacho kimeelezwa kuwa si cha kiungwana na alisema jambo ambalo halikuhusiana na mahojiano.
Pia baadhi ya wanamichezo wamelaani kitendo hicho kwamba hakikuwa cha kiungwana kwa kuwa mhusika aliingiza mambo ya faragha kwenye hadhara.
05Jan2016