Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

KOSA LAKO KUBWA NI UONGO....
-Kwann ulidanganya at the firstplace?
-Chakufanya kwasasa mjulishe MKEO, mwambie hali halisi ili naye umsikie ANASEMAJE
-Next time ukirudi tena nchi za watu kwa MASTERS au PHD nadhani hutarudia tena Kosa..
 
MwanaDiaspora, pole kwa unayopitia. You have crossed the line, you are just facing the consequences.
Swali kwamba ufanyaje sio sahihi kwa sasa, kwa waliowahi kukosea kwa namna hii wanajua kuwa ni swala la muda tu Kabla dunia haijakujua vizuri.
Mkeo atajua vile ulivyo, hata watoto wako pia.
Haya ni aina ya makosa ambayo ukijaribu kuzuia matokeo yake basi inazidisha damage.
Unaweza kufanya yafuatayo.
1. Mweleze binti wa Kikorea kuwa una mke na watoto ( haitamshangaza maana Waafrika hatuaminiki Sana)
2. Kwa mkeo subiri kidogo, huna haja ya kukwambia chochote kwa sasa mpaka utakapopata response ya Mkorea ambaye she will likely opt for abortion.
3. Don't feel guilty..haisaidii you are guilt already
4. Sio wakati wa kutangazia ulimwengu kuwa unampenda sana mkeo kilichofanyika ni kinyume kabisa na maneno hayo labda Kama una maana nyingine ya Upendo.

Acha tusubiri.
 
Mkuu kwa hili jambo, ukweli ndio utakaokuweka huru ata kama ni mchungu, Nakushauri maliza kwanza mitihani then mwambie mkorea ukweli kuhusu marital status yako, kisha yeye atatafakari. Ukirudi nyumbani mueleze mkeo, cha muhimu usitelekeze damu yako yaani mtoto atakayezaliwa na mkorea, ukitelekeza ni mbaya sana hata kwa Mungu.
 
Mkuu wazo ni zuri sana ila nafikiri nikikosa wazo mbadala lililozuri nitalifanya aidha airport ya huku Seoul tukiwa tumeshacheck in au Doha ili akachachamaa nampotezea.
Do not do that! Kwanza tuliza mawazo ili ujipange vizuri. Je, uwezekano wa wewe kukaa na kutafuta shillingi huko upo vipi?
 
Ushauri wako nitauzingatia. Huyu binti tulipokuwa marafiki hakuwahi niuliza habari za mimi kama nimeoa wala mimi sikuona sababu ya kumwambia kuwa nimeoa. Tukiwa marafiki hakutaka kuona mimi nazungumzia habari za wanawake wengine anatabia fulani ya wivu.

Taratibu tukajikuta tumevuka mipaka, mimi sikuona sababu ya kuweka wazi kwa sababu nilijua ni mahusiano ya muda mfupi na hatuna mpango wa kuoana, bahati mbaya zaidi mwenzangu akanogewa moyo huruma ukawa unaingia ili nisimuumize.

Mimi technique yangu ilikuwa ni kwamba nikisharudi bongo ndio nivunje mahusiano kumbe yeye yuko mbele yangu 300 km. Huo ujauzito kashika makusudi mana siku zote alikuwa makini sana.
 
Usicheze na mwanafunzi wa mapenzi, anaweza kukuondoa hivi hivi. Jipange kijana ndiyo uanaume huo
 
Mwambie mkeo kuwa unae mchepuko wa kikorea na anakuzingua.
 
Sikiliza wewe kakate tiketi yako kwa pesa yako siku nyingine na ndege nyingine halafu mtoroke ila akikisha unamwandikia mail yenye ukweli wote kisha ama hapo ulipo nenda kapige shopping kwa ajili ya familia kisha unasepa kimya kimya. Hqkijua ukweli hawezi kukutafuta tena maana roho itamwingia nyongo na kama akikutafuta au akija Bongo ujue huyo kaja kukuua
 
Pole sana, pia ufikirie mtoto wako huyo mkorea ni damu yako hiyo, unaiacha vipi? Pia umwambie ukweli mkeo kuwa unatarajia mtoto na mkorea umpe story nzima. Hakuna kitu nakithamini kama damu yangu. Ukimkimbia huyo mkorea baadae utakuja kuwaza kuhusu mtoto wako, na unaweza kujutia maamuzi yako. Ulishindwa kusema ukweli mwanzo, useme wote sasa Lubebenamawe
 
Huyo
Ndio Shetani mkuu,ameshamaliza kazi yake na sasa kakuachia msala hana msaada wowote zaidi ya kukucheka ujinga.HAKUNA DHAMBI NZURI,ndio maana Mungu alituonya tukae nayo mbali.
 
Hivi hawa wakorea si ndio kina JUMONG? na kina IRIS? Mkuu hilo unalo. Cha kufanya muandae rafiki yako wa Tz akuandalie nyumba mbali na kwako. Mwambie wife umeahirisha safari utamwambia ukiwa tayari, acha kuwasiliana na wife kwa muda. Njoo Tz ukifika jipange maisha mapya na mkorea. Baada ya Muda mpange sasa ili ajue A-Z.
 

Wanawake tukipenda kwenye uhusiano tunafikiria kinachotokea next, unafarijika pale mtu anapokuuliza maswali kama, uko tayari kuishi Afrika?, Ungependa kuzaa watoto wangapi, majina ya watoto, ukiona hivi vyote hakuna unaanza kusoma namba 'I'm here just for a ride'.
Either unaanza kupotezea, kuna wanaopenda kupita hao ndio wanawaza mbinu mbadala.
 
Asante sana umenifunua hilo mana anaweza zusha nimemuibia, mpaka sasa anataka kiasi cha fedha alichonacho anataka ahamishie kwenye akaunti yangu kwa madai ya kwamba benki alimohifadhia hizo fedha sio international. Mimi nimweleza kuwa kiasi hicho cha fedha kikiingia kwenye account yangu ninaweza kuhisiwa kuwa natakatisha fedha hivyo nikamshauri afungue kwenye benki ambayo ni international hilo amenielewa. Lengo langu ni kupunguza kufungamana naye.
 
Mkuu sina mpango wa kumuacha mke wangu natafuta namna ya kumueleza huyo mkorea ili anielewe na tuachane kwa amani.
 
Njoo nae TZ ila mfikie hotel, then mkifika muambie ukweli tu na kwamba mtaishi wote ila mkeo wa ndoa hutamuambia. Itabidi umtafutie nyumba ili awe mke mdogo. Lete mbegu ya ki-korea Tz kaka. U never know ya mbeleni mana unaweza ukamuacha na akagoma kutoa mimba na itansumbua sana hiyo kitu. Wewe njoo nae ni bora ajulie ukweli akiwa huku tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…