Mchepuko umeingia ndani......

Mchepuko umeingia ndani......

Wakanda27

Member
Joined
May 23, 2020
Posts
40
Reaction score
509
Habari wana MMU. Nia ya uzi huu kuomba msaada wenu wa mawazo.

Niko ndoa kwa muda sasa, nilipata mpango wangu wa kando ambao mwanzoni niliuelewa sana. For story writing purposes naomba tumpe jina X. Huyu X nilimkuta kwenye mahusiano na jamaa yake, so wote tulikuwa tunawasaliti wenzi wetu japo yeye hajaolewa. Sasa ilifika kipindi akaachana na huyo jamaa wa kwanza.

Kipindi chote hicho mimi sikuwa na wivu hata chembe. Sasa akaanza mahusiano na mtu mwingine ambae alikutana nae sehemu anayofanyia kazi. Sasa huyu X kwa kweli nilijitahidi sana kumtunza, kuanzia mavazi , muonekano na hata kumbadilishia simu maana jamaa yake alikuwa bado haja settle kiuchumi. Na kipindi chote tokea nimpate huyu X, sikuchepuka tena sehemu nyingine.

Tatizo Liliopo sasa;
Tokea ampate huyu jamaa nimekuwa na WIVU sana. Nampenda mke wangu na najitahidi sana kumheshimu, najua humu mtaleta hoja mbali mbali kupingana na hili lakini ukweli najua mimi. Ila najishangaa kuumia sana alipotokea huyu jamaa mpya. Naona kama anateleza tu, amemkuta amenawiri na anang’aaa yeye sasa anakula kitonga. Sitaki kuwa selfish kwa X kwa sababu najua fika penzi letu litaishia hapa na yeye anahitaji kuwa na familia, lakini the thought ya yeye kuwa na huyu jamaa mpya kinaniuma sana.

Ukicheki jamaa nae ni ovyo tu kiuchumi, not ambitious yaani ni mtu ambae kwa ujasusi wangu wa haraka , ni wale wakupenda vitu ready made. Last time nilidukua simu ya X na kukuta jamaa anamlamikia kuwa amefulia anaomba amkope 50,000. Ila anapewa services zote. Hiki kitu kinaumiza kichwa sana and I don’t know why. Samahani kwa uandishi mmbovu, naombeni mnieleweshe kwa nn napata hasira.

Je ni kwamba nampenda sana huyu dada au ni wivu tu.
 
Upendo sio maneno pekee, na vitendo pia. Ungekuwa unampenda mkeo ungemheshimu, usingechepuka.

It seems to me X anampenda huyo jamaa mpya zaidi yako na wewe unampenda X zaidi ya mke wako.

Kwahiyo upo kwenye love triangle. Pole.
 
Hapo mkeo unakuta anajitahidi sana utulize mawazo kwake na anajua yupo peke yake!!!
 
Njia Ni Mbili Kiongozi Bila Kufuata Hizo Utazua Bhalaa

1. Mwache Aendelee Na Huyo Jamaa Taratibu
2. Rudi Utulie Kwa Mkeo,

* Najua Huyo Mwanamke Ukiongea Naye Zaidi Atakwambia Mbona Wewe Mwenyewe Una Mkeo Na Yeye Hana Wivu Itakuwa Ugomvi

Kwenye Hiyo Company Toa Hisa Zako Iache Kampuni Iendelee Yenyewe Hata Ikifa 😀😁😂😅😄
 
Njia Ni Mbili Kiongozi Bila Kufuata Hizo Utazua Bhalaa

1. Mwache Aendelee Na Huyo Jamaa Taratibu
2. Rudi Utulie Kwa Mkeo,

* Najua Huyo Mwanamke Ukiongea Naye Zaidi Atakwambia Mbona Wewe Mwenyewe Una Mkeo Na Yeye Hana Wivu Itakuwa Ugomvi

Kwenye Hiyo Company Toa Hisa Zako Iache Kampuni Iendelee Yenyewe Hata Ikifa

Sawa mkuu, japo sio rahisi ila inabidi nijitahidi.
 
Hapo unatamani huyo X uwe unamfaidi mwenyewe na wakati una wako nyumbani, huo ni uselfish yaani kubali tu hilo we mwache naye aenjoy hadi apate mume wake.
Na hapo manake unahudumia na hyo njemba.... Ili usiumie zaidi dawa ni kumuacha tu utulie na mkeo sababu wivu ukija kuzidi sana utapachukia kwako, hutaona umuhimu wa mkeo akili itakua kwa mchepuko mda wote.
 
Kuwa na mchepuko ni sawa..lakini kuwa na mchepuko mwenye mtu wake na unafhamu hilo plus kuhudumia ni udhaifu mkuu....me nikijua tu tunashare na mtu mchepuko namuachia jamaa aisee...siwezi hudumia koloni la mtu.Piga chini huo mchepuko mkuu huo wivu utakupeleka kubaya aisee...Kumuonea wivu inamaa unaanza kugenarate hisia kwake...Kufall kwa mchepuko wakati una mke ni hatari kwa ndoa yako.
 
Back
Top Bottom