Kama unaumia sana mchukue umuoe mke wa pili
Habari wana MMU. Nia ya uzi huu kuomba msaada wenu wa mawazo.
Niko ndoa kwa muda sasa, nilipata mpango wangu wa kando ambao mwanzoni niliuelewa sana. For story writing purposes naomba tumpe jina X. Huyu X nilimkuta kwenye mahusiano na jamaa yake, so wote tulikuwa tunawasaliti wenzi wetu japo yeye hajaolewa. Sasa ilifika kipindi akaachana na huyo jamaa wa kwanza.
Kipindi chote hicho mimi sikuwa na wivu hata chembe. Sasa akaanza mahusiano na mtu mwingine ambae alikutana nae sehemu anayofanyia kazi. Sasa huyu X kwa kweli nilijitahidi sana kumtunza, kuanzia mavazi , muonekano na hata kumbadilishia simu maana jamaa yake alikuwa bado haja settle kiuchumi. Na kipindi chote tokea nimpate huyu X, sikuchepuka tena sehemu nyingine.
Tatizo Liliopo sasa;
Tokea ampate huyu jamaa nimekuwa na WIVU sana. Nampenda mke wangu na najitahidi sana kumheshimu, najua humu mtaleta hoja mbali mbali kupingana na hili lakini ukweli najua mimi. Ila najishangaa kuumia sana alipotokea huyu jamaa mpya. Naona kama anateleza tu, amemkuta amenawiri na anang’aaa yeye sasa anakula kitonga. Sitaki kuwa selfish kwa X kwa sababu najua fika penzi letu litaishia hapa na yeye anahitaji kuwa na familia, lakini the thought ya yeye kuwa na huyu jamaa mpya kinaniuma sana.
Ukicheki jamaa nae ni ovyo tu kiuchumi, not ambitious yaani ni mtu ambae kwa ujasusi wangu wa haraka , ni wale wakupenda vitu ready made. Last time nilidukua simu ya X na kukuta jamaa anamlamikia kuwa amefulia anaomba amkope 50,000. Ila anapewa services zote. Hiki kitu kinaumiza kichwa sana and I don’t know why. Samahani kwa uandishi mmbovu, naombeni mnieleweshe kwa nn napata hasira.
Je ni kwamba nampenda sana huyu dada au ni wivu tu.
