GE2025 Mchengerwa: Tutamuomba Rais Rufiji iwe Mkoa

GE2025 Mchengerwa: Tutamuomba Rais Rufiji iwe Mkoa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kama wamekidhi vigezo hamna tatizo
Kama wamekidhi vigezo ok lakini siyo kwenda kumpigia magoti Mh Rais. Tunataka utenganifu wa mihimili ya serikali. Vyote vijitegemee sio kumwomba mwenzake ima judiciary, ima executive ima bunge
 
Ifakala toka muda inaomba kuwa mkoa..lakini hamtaki kisikia...wananchi wanaishi vichochoroni
 
Anachoahidi leo ndo aliahidi miaka 5 iliyopita, na atakiahidi miaka 5 ijayo..,,, kwani hizo stendi na masoko ilishindikana miaka hii 5 iliyopita?
Ishu ya Mkoa ni sawa maana mtu atoke Nangulangwa aje Dar ndo aende Kibaha kwenye Ofisi ya Mkoa ni kupotezeana watu na hela..
Wangeugawa , kwa hichi kipande cha Mkuranga kwenda huko chini mpaka na Lindi kijitegemee na hawa watu wa Kisarawe, Kibaha, Bagamoyo majirani zao wawe na mkoa wao..
 
Mtia Nia ya Ubunge wa Jimbo la Rufiji, Mohamed Omary Mchengerwa ambaye ndiye Mbunge anayemaliza muda wake, akinadi sera zake mbele ya wajumbe na kuomba kura kwa wajumbe wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Mbwara iliyopo katika Jimbo hilo lililopo Mkoa wa Pwani, ameeleza kuwa kutokana na Maendeleo yaliyopatikana wilayani hapo atapeleka Ombi Halmashauri hiyo kuwa Mkoa.

Rufiji haina status ya kuwa mkoa, bado sana. Inabidi msubiri. Acha kudanganya wananchi.
 
Back
Top Bottom