eddy, kwa akili zako unadhani Mji ule wa kubuni unatosha eneo la Kawe? mji ule ulivyobanywa kwenye Hekari 360 za iliyokuwa Tanganyika packers LTD, including Entrances na maeneo ambayo yalikuwa Pori, kwa sasa hekari hizo 360 hazipo Eddy, kupata hekari 130 tu kwa sasa ni kazi kubwa sana, hivyo mnataka raisi wetu aonekane kopo, asigh mikataba wakati Eneo halipo, mbali na shule za msingi, kuna kituo kikubwa cha Polisi, kanisa katoliki tayari wana miliki eneo lao Kubwa pale, bado Mgiriki huyu anayemniliki shule za Fedha ameshamegewa zaidi ya hekari 40 na serikali, bado waziri wetu Mwinyi na wazitozito huku baharini wameshajijengea mahekalu yao ya vijisenti vya bilioni, unaongelea eneo gani la kawe wewe, hapa tunapochezea pikipiki zetu au vinyumba viwili vitatu mlivyovibomoa vya maskini wafanyakazi Kiwanda alichokiua baba yake Mchechu?>??
pesa laini, hii pesa madalali mnayoitaka kwa Eneo lipi, Tamaa yenu mbaya, mtaitukanisha nchi bure, kule Kigamboni mmegonga mwamba mmekimbilia kawe, maskini eneo wala halipo, mnajitahidi kulisafisha mnatamani kusogeza bahari haiwezekani, Tamaa yenu mbaya, Mji gani wa kisasa unajengwa hali pembeni kuna mitaa ya uswahilini ya maskinbi wa kawe? ..
sogezeni mradi wenu, sikatai wala sitii mchanga kitumbua chenu ila basi mwonyesheni mwekezaji ardhi isiyo na migogoro inayotosha mradi wake kwanini kumgombanisha na raia? eneo halipo, bado lina makesi kibaoo, mnaleta ujanjaujanja tu..