Rutunga M
JF-Expert Member
- Mar 16, 2009
- 1,769
- 1,382
Wakuu,nimekuwa tika mzunguko wa kikazi ulionifanya nizunguke nchi yetu takribani mikoa sita mfululizo,mara,mwanza,shinyanga,kagera,kigoma na rukwa.
Kikubwa nilichogundua ni kuwa kuna utitiri wa redio nyingi katika wilaya na mikoa hiyo na wanapiga miziki asubuhi mpaka jioni na vituo vyote hivyo havina matangazo ya biashara.
Mimi najiuliza hivi ni kwa nini tuwe na vituo vingi vya redio visivyo na tija kwani vingi vinajiunga na TBC wakati TBC inasikika vema katika maeneo hayo.
mathalan nimegundua kuwa mkoa wa kagera pekee kuna redio 5,kwizera(ngara),fadeco na karagwe fm(karagwe),kasibante na vision fm(bukoba mjini),
licha ya wingi huo wa vituo vya redio huwezi kusikia issues za maana katika redio hizo mbali na miziki tu.
TUTAFIKA?