Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 9,269
- 7,457
Hivi hamchoki kutabiri kifo cha Chadema? Musa aliwatoa waisraeli Misri lakini hakugusa nchi ya ahadi. Pamoja na mchango wake mkubwa, kiburi chake ndicho kilimfanya asifike nchi ya ahadi. Hivyo kwa wakina Halima na wenzake.Ukweli lazima usemwe.
Chadema ilipofikia inaelekea kufa kabisa katika siasa za vyama vingi Tanzania.
Chadema haikujengwa kwa sera bali ilijengwa na umahiri , weledi na uwezo wa mtu mmoja mmoja.
Alipo ondoka Zitto ndani ya Chadema, chama kiliyumba na hakikuwahi kukaa sawa mpaka sasa. Dr Slaah alijitahidi saana kuziba pengo la bwana Zitto.
Alipo ondoka Dr Slaah, Chadema sio kwamba kiliyumba tu bali kilipoteza mwelekeo, kimekuwa Chama cha matukio tu, kila wanachojaribu kufanya wanadondokea pua, movement zao zote zinafeli.
Sasa wameamua kumuondoa Halima Mdee na wenzake.
Hakuna asiyetambua uwezo binafsi wa Halima Mdee katika uwanja wa siasa za Tanzania. Mdee amekijenga chama, amefanya akina mama wengi wajiunge na siasa za upinzani.
Hakuna mwanamke yeyote hapa Tanzania ambaye anaweza lingana na Mdee katika siasa za upinzani. Mchango wa Mdee kwa Chadema ukimtoa Mbowe ni sawa na Wanachama wote waliobaki Chadema.
Katika vita vyote ulivyowahi kupigana Mh. Mbowe hii ya akina Halima Mdee na wenzake umeshindwa.
Ni chuki tu zimewaondoa Chadema akina Mdee na wenzake .
Hao akina Hilda si level ya Mdee.
Chadema kinaenda kuzikwa moja kwa moja kwenye siasa za Tanzania
#MUNGU IBARIKI TANZANIA #MUNGU MBARIKI MH. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA #SSH
Kwa nyie mnaosifia umahiri wake tuelezeni huo umahiri ameuonyesha kwenye ishu gani toka Ndugai amuingize Bungeni? Yeye na wenzake, wamewatetea vipi wananchi wao? Mimi nilichokiona ni pathetic sight ya wao kubezwa na kupuuzwa na vijana wadogo wa CCM.
Ukweli ni kuwa nje ya Chadema hawafurukuti kokote. Wamekuwa waganga njaa tu.
Amandla....