Mchango wa Dini katika ustawi wa maisha ya Binadamu

Mkuu napenda sana unavyo tudadavulia mada ngumu Kama hizi
 
Tunaongelea dini hatuongelei watu wa Dini. Kwani Dini gani katika hizi dini zinazo amini uwepo wa Mola muumba zinafundisha unafiki, uzinzi, uongo,kupiga dili, uchawi ?
Uko sawa ila kuna hili la Ubaguzi dhidi ya imani nyingine. Ukisoma baadhi ya mistari ya vitabu hivyo vya dini utayaona hayo.

Na jambo hilo la ubaguzi wa dini moja kujikweza dhidi ya nyinginezo limechochea chuki na hata mauaji.
 
Sasa iweje Mola ni mmoja halafu Dini ziwe nyingi ? Ujue hapo lazima Dini moja ni sahihi na hizo nyingine na fikra za watu kama vile Ubudha, Uhindu, Upagani (Naturalism) , na mfano wao.
 
Unasali ili upate nini?,maana kuna wengine wanasali wapate toyota tako la nyani 😁😁,wengine wapate hela
 
Bila shaka ni kiarabu sivyo?
Nakupa maana nyingine ni hii :

Nanukuu : "Maana ya dini kwa mtazamo wa fani ya Elimu ya jamii: “dini ni idadi maalumu ya itikadi, matendo, alama pamoja vitengo vya kidini ambavyo vimejengwa na wanajamii ndani ya jamii mbali mbali”. Imenukuliwa kutoka kwa Talcott Parsons."
 
Kijana mbona una ruka ruka sana. Kwani Dini kwa Kiswahili ni nini mzee ?

Siyo Kiarabu.

Pili, unapo sema Kiarabu una maanisha ya kuwa Kiarabu kinakosea au Kiarabu siyo Lugha au nini ? Nieleweshe hapo maana naona umeanza kuogopa mapema sana.
Nigeuzie hii kwa kiswahili, najua we ni expert kwenye kiarabu Huwezi shindwa

الإيمان بعبادة قوة خارقة مسيطرة ، خاصة إله شخصي أو آلهة.
al'iiman bieibadat quat khariqat musaytirat , khasat 'iilah shakhsiun 'aw alihat.
 
Elimu ya jamii ni nini?
 
Sijui maana yake.
 
Sasa iweje Mola ni mmoja halafu Dini ziwe nyingi ? Ujue hapo lazima Dini moja ni sahihi na hizo nyingine na fikra za watu kama vile Ubudha, Uhindu, Upagani (Naturalism) , na mfano wao.
Hilo la Usahihi wa dini moja ni tafasiri yako moyoni na imani yako. Kila mmoja ataona dini yake ni sahihi.

Jamii zetu ni tofauti, historia, tamaduni na mazingira. Dini ni 'social construct' tokea enzi hapajawahi kuwa na dini moja na sidhani kama itatokea iwe hivyo.
 
Nakurudi?
 
Tunaongelea dini hatuongelei watu wa Dini. Kwani Dini gani katika hizi dini zinazo amini uwepo wa Mola muumba zinafundisha unafiki, uzinzi, uongo,kupiga dili, uchawi ?

Unawezaje kutenganisha dini na watu wa dini? Kuna dini isiyo na watu?
 
Sasa hii ndio maana halisi ya dini na sio ile yakihuni kutoka uarabuni uliyoiweka awali
 
Swadakta..

Na wachina wanawapiga jamii ya waislam wa Uyghur huko kwao

Waislam na wakristo ndio vinara wa vita za kidini duniani, na hili halijaanza leo. Ndio maana nimesema vita karibu zote za kidini lazima utakuta ni ama mkristo na muislamu, au mojawapo kati ya dini hizo mbili vs dini nyingine.
 
Kwa akili ya kawaida tu, zinaweza vipi dini nyingi zote zikawa sahihi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…