Naam, naam.
Nimejitahidi sana kusoma dini.Binafsi nyumbani kwa mzee wangu alipotokea ni kanisani. Kwa kuwa baba yake alikuwa mchungaji.
Kwa hivyo, yeye alikuwa si tu anaenda kanisani, bali aliishi kanisani...
Kama si dini hii dunia pangekuwa ni uwanja wa vita
Inaonekana hujui maana ya Dini. Kwanza nakupa kazi wakina hawana Dini halafu ni watu wa Amani ? Maana hata "Atheism" nayo ni Dini.Utafiti mdogo tu utakuonyesha kuwa watu wasio na dini kabisa, au wenye dini tofauti na ukristo au uislamu, ni watu wa amani sana. On the contrary, vita zote kubwa duniani, matukio makubwa ya uhalifu wa kila aina, yanafanywa na watu wenye dini!..
Kama si dini hii dunia pangekuwa ni uwanja wa vita
Sasa mbona unajijibu mwenyewe mzee ? Mbona unataja uchache kisha unahitimisha kwa dunia nzima ?Wakati wa vita vya kwanza na vya pili vya dunia dini ilikuwa imejaa duniani,vita vya Mashariki ya kati,Vietnam,Sri Lanka,Congo,Angola,Sudan,Uganda ,CAR,India na Pakistan vimepeganwa na vingine vinaendelea kupiganwa dini ikiwa imejaa tele duniani.
Thibitisha hili. Bali Atheism ni nini ?Atheism sio dini
Dini imeleta mazuri na mabaya ila kimizania mazuri ni mengi zaidi.
Hizi Dini zimesaidia watu wajue kuna nguvu kuu iliyo juu yao (Mungu/mwenye enzi/God/Mulungu) na mwishowe kila mtu atawajibika kutoa majibu kwa yale aliyofanya hapa duniani.
Imani hii ndo muhimili wa Amani tuliyonayo duniani leo hii. Vinginevo dunia ingekuwa sehemu hatari sana.
Nini maana ya dini?Inaonekana hujui maana ya Dini. Kwanza nakupa kazi wakina hawana Dini halafu ni watu wa Amani ? Maana hata "Atheism" nayo ni Dini.
Dini ni tamko lenye asili ya Kiarabu, lenye maana ya njia au mwenendo au mfumo wa maisha anao endana nao mtu fulani katika shughuli zake za kila siku.Nini maana ya dini
Hiyo definition ime base katika muktadha wa kiarabu au in generally?Dini ni tamko lenye asili ya Kiarabu, lenye maana ya njia au mwenendo au mfumo wa maisha anao endana nao mtu fulani katika shughuli zake za kila siku.
Hii kwa ujumla wake. Nimeitoa katika Kamusi "Maajim al Maan".Hiyo definition ime base katika muktadha wa kiarabu au in generally?
Hii tafsiri umeitoa kwenye chanzo kipi?
Inaonekana hujui maana ya Dini. Kwanza nakupa kazi wakina hawana Dini halafu ni watu wa Amani ? Maana hata "Atheism" nayo ni Dini.
Bila shaka ni kiarabu sivyo?Hii kwa ujumla wake. Nimeitoa katika Kamusi "Maajim al Maan".
Nimejitahidi kusoma na kujifunza vingi, na bado nina vingi zaidi vya kusoma na kujifunza.Shukrani mkuu
Upo deep Sana kwenye upambanuzi wa mada tofauti tofauti
Binafsi nakukubali sana Jf,najiulizaga huu uwezo sijui uliupatia wapi!
Tunaongelea dini hatuongelei watu wa Dini. Kwani Dini gani katika hizi dini zinazo amini uwepo wa Mola muumba zinafundisha unafiki, uzinzi, uongo,kupiga dili, uchawi ?Atheists wachache ninaowafahamu wako very peaceful compared na wenye dini wengi ninaowafahamu. Washika dini wengi sana ninaowafahamu nikiwepo na mimi ni wanafki wakubwa, wasengenyaji, waongo, waasherati, wezi, wapiga dili, wachawi, walevi, wagomvi, wabaguzi, wenye wivu, husuda na kila aina ya uovu unaoujua wewe.
Sio hizo mbili tu, Wahindu wanawapiga waislam huko India mkuu.Utafiti mdogo tu utakuonyesha kuwa watu wasio na dini kabisa, au wenye dini tofauti na ukristo au uislamu, ni watu wa amani sana. On the contrary, vita zote kubwa duniani, matukio makubwa ya uhalifu wa kila aina, yanafanywa na watu wenye dini!
Wewe umewahi kusikia wapi vita ya kidini ambayo haihusishi ama wakristo na waislamu, au dini hizo mbili na wasio na dini au wenye dini zingine? Mfano, umewahi kusikia vita kati ya rastafarians na wahindu? Au kati ya wabuddha na wapagani?
Tafakari.
Kijana mbona una ruka ruka sana. Kwani Dini kwa Kiswahili ni nini mzee ?Bila shaka ni kiarabu sivyo?
Maneno yako ni kweli kabisa.Nakubaliana na uliyoyasema, na kwa mtazamo wangu, ili dini itumike vizuri ni lazima wale wanaoitumia wawe na upeo fulani wa uelewa, na kiwango fulani cha maendeleo..