Alhamisi tarehe 28/07/11 Wizara ya Mambo ya ndani itawasilisha hoja/bajeti yake bungeni. Wizara hii inasimamia uhamiaji, polisi, magereza na hata usalama barabarani. Akiwa kama Waziri kivuli naomba Mh Lema aulize/asimamie yafuatayo:
1. Ajali za barabarani
Ajali za barabarani zimekuwa zinaongezeka siku hadi siku na hasa kwa mabasi yanayotoa usafiri wa kwenda mikoani. Idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali hizo inatisha. Sasa Lema atoe hoja kwamba serikali ianzishe DATABASE kwa ajili ya kuweka record sawa majina ya kampuni yanayomiliki mabasi na ajali zake. Mabasi kama Abood, Sumry na Hood yanaonekana kuwa ajali nyingi za kustusha. Kama kampuni inapata ajali na watu kupoteza maisha basi kampuni hiyo isiruhusiwe kutoa huduma ya usafiri hadi pale serikali na hasa wizara itakapofanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa hatua zote za usalama zinaheshimiwa.
Haiingii akilini kwamba kampuni moja ya mabasi inapata ajali mara mbili ndani ya mwezi mmoja, watu wanapoteza maisha lakini bado mabasi yake mengine yako barabarani huku serikali imekaa kimya!
2. Ubora wa mabasi ya abiria
Huko nyuma serikali ilikuwa imetoa muda kwa wamiliki wa mabasi makubwa (kama sikosei ilikuwa 6 months) ili waondokane na tabia cha kuchanga bodi na engine za FUSO. Hili ni jambo la muhimu sana maana linahusu usalama wa maisha ya abiria lakini bila maelezo hakuna chochote kilichofanyika. Kuna ma-lobbyists wameibana serikali na sasa mabasi mengi yanatumia engine za Fuso. Kwangu mimi naona wenye mabasi ya engine za Fuso wanajali zaidi faida kuliko uhai wa abiria lakini kinachosikitisha ni kwa serikali kunyamaza huku watanzania wanakufa. Basi la kubeba abiria lazima limitize masharti yote ya ki-usalama na sharti moja kubwa ni ubora wa engine yake. Lazima liwe na engine ya basi la abiria na si vinginevyo.
3. Uhamiaji
Tanzania imekuwa kama shamba la bibi kwa kuwa na raia wa kigeni wanafanya kazi ambazo watanzania wanaweza kufanya. Maswali hapa:
- Idadi ya raia wa kigeni walioko Tanzania ni ngapi?
- Vibali au visa kwa wageni wanafanya kazi nchini zinapatikanaje?
- Wale wamachinga wa Kichina walioko Kariakoo wamepataje vibali vya kuingia?
- Kuna maduka ya wahindi (airport Dar es Salaam, KIA na Zanzibar) wameajiri wauza wahindi toka India kuja kuuza maduka. Kuna vyumba za kupanga _commercial residents zinazomilikiwa na wahindi ukichunguza wafanyakazi utakuta wanatoka India. Hivi ni kweli Mtanzania hawezi kusimamia usambazaji wa maji (kwa malori) kwenye hizi maflats ya wahindi?
4. Diplomatic passport
Ni watu gani wanatakiwa wawe na Diplomatic passport na sasa hivi ni wangapi ambao wana hizo passport?
(kuna watu wengi tu huku mtaani wana Diplomatic passport)
5. Magereza
Hali ya mahabusu na wafungwa inatisha! Kuna watu wamebambikiwa kesi wako rumande kwa miaka. Ukitembelea magereza unaweza kuzimia kwa uchungu. kuna watanzania (wasio na hatia) na wengine ni watoto wako mahabusu for years!
Hapa Lema ahimize kuundwe timu maalum ya kuchunguza hali ya jela, na mahabusu na pia kupata taarifa kamili juu ya maabusu wanaosubiri kesi kwa miaka!