Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 24,441
- 29,987
Chalamila wewe ni tajiri mwenye uwezo wa kumiliki landikruza la bilioni japo umepewa na serikali, inasikitisha mtu anakopa mamilioni ya shilingi ili asafirishe wananchi wewe tajiri unaliita takataka!? Kwa utajiri gani ulionao.
Chalamila wakazi wa Mbagala wanalalamikia malori yaliyojazana barabarani yakikwepa kwenda Kwala, wewe hauyaoni hayo malori unaona mabasi ambayo hayapo Dar mchana, yapo safarini mikoani kwani huandoka alfajiri.
Dharau, unawalazimisha wenye mabasi wawashushe abiria Mbezi eti wakodi teksi, bodaboda na bajaji! Hawa abiria wengine nauli wamekopa au wamechangiwa na ndugu zao au wameuza kuku, wewe tajiri haulijui hilo ni sawa na yule mke wa mfalme aliyewaona wananchi wakilia njaa akashauri wale keki!
Nikirudi kwenye mabasi, mabasi tunayoyaona huku kwetu Mbagala ni ya daladala na ninadra kuona ya mikoani labda limetoka Mtwara linapita kwenda Tanga au Dodoma, sasa kama tatizo ni mabasi nakushauri ondoa mabasi ya daladala ambayo ndiyo mengi yanayofanya safari za nendarudi nendarudi kutwa nzima.
Namaliza kwa kukujulisha tu hizo takataka ndizo tegemeo letu la usafiri mpaka mungu atakapotujaalia tuwe kama wewe.