ASHA NGEDELE
JF-Expert Member
- Jul 5, 2011
- 784
- 326
Habari zenu wafugaji na maafisa kilimo na ufugaji.
Biashara zote zimegoma kwahio nataka niingize mtaji kufuga kuku wa mayai. Sina experience lakini kwenye mchanganuo wangu wa biashara nimeweka cost ya kumlipa mtaalam wa kusimamia mradi na kuhakikisha kuku wanapata chanjo zote, uwiano sahihi wa chakula na utaalamu wote pamoja na ujenzi wa banda sahihi.
Changamoto yangu kubwa ni kwamba kila hesabu nazopiga, mwisho wa siku napata HASARA na sioni faida.
Naomba uzoefu kutoka kwa wafugaji (wanaoweka rekodi za gharama na mauzo) nijifunze wanafaidika vipi na ufugaji huu.
Naomba kuwashirikisha mchanganuo wangu unaonifanya kuona ufugaji wa Layers hauna faida bali hasara.
1. Gharama
Kuku akianza kutaga, anahitaji chakula 130gm kwa siku ambayo ni sawa na 4kg kwa kuku kwa mwezi
Maana ake ni Tzs4,000 kwa kuku kwa mwezi (kwa bei ya sh1,000 kwa kilo ya chakula)
Kwa mradi wa kuku 1,000 ni 4,000,000 chakula pekee kwa mwezi (wiki nne) bado madawa, chanjo, chakula kabla hawajaanza kutaga (Starter na Grower), kijana wa kazi, mtaalamu, vifaranga na gharama zingine.
Gharama za ujenzi wa banda, cages, vifaa vya kulishia kuku sitazijumuisha hapa sababu kihasibu ni 'capital in nature'.
2. Mauzo
Breed nzuri zaidi zinatoa 250 mayai kwa mwaka maana ake kwa siku wanataga mayai 0.7 (250/360=69%).
Kwahio kuku elfu 1,000 (kama wote watataga, kitu ambacho sio kweli) watatoa mayai 700 kwa siku ambayo ni sawa na trei 23 kwa siku.
Kwa bei Tzs5,000 kwa trei unapata Tz117,000. Kwa mwezi mauzo jumla TZS 3,500,000. Sijatoa gharama zinazoambatana na mauzo hapo.
Kwa mwezi mfugaji ana uhakika wa hasara ya (TZS400,000) ambapo kama kuku watataga kwa miezi 18 mfululizo jumla ya Hasara itakua (TZS7,200,000).
Naomba ushauri tafadhali.
Sent using Jamii Forums mobile app