Mchambuzi Farhan: Simba wametupiga kwenye jezi

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,783
24,215
FARHAN: SIMBA WAMETUPIGA.

Labda CEO atusaidie kidogo majibu ni kwamba hakuna Mdhamini mwingine wa kuweka hela ama? MO XTRA zipo mara mbili, juu kulia na moja kubwa mbele kifuani, kabisa hakuna brand nyingine? Jezi moja ina matangazo mawili ya kufanana?

Tajiri anatoa mzigo yes lakini hii ya kutuweka matangazo ya kufanana kwenye uzi mmoja ni kubana fursa nyingine za klabu kuingiza pesa ya kutosha kutokana na platform hii kubwa ya michuano ya kimataifa.

Halafu CEO pia atusaidie hiyo MO SPORT mkataba wake ulisainiwa lini? Ni Kampuni ya nani hii? Inajihusisha na nini hii?

Ni hayo tu kwasasa, ni hayo tu.

[@jr_farhanjr ]
 
Ni kawaida kwa timu yetu adhimu ya Simba kuandika "visit Tanzania" kifuani kwenye jezi za mashindano ya kimataifa ambayo miongoni mwa wadhamini wake ni michezo ya kubahatisha ili kusaidia kuvutia watalii kuja nchi kazi ambayo ni ya mamlaka ya mbuga zetu, TANAPA. Je, msimu huu ni hivyo tena au watabadilisha uelekeo?
 
Simba kuna shida. Tena kubwa tu. Sijawahi kuona timu ina matangazo mawili ya aina moja ndani ya jezi moja tena zote mbele.

Wamekosa wadhamini? CEO kazi yake nn sasa? Hii inapunguza mashabiki wenye akili ila wale wenye akili za kuvukia barabara wanaleta mahaba ila haikubaliki kabisa
 
Wala hakuna shida ni vile TU tumejawa na fikra duni na kudhani kila kitu lazima kifanane. Mara jezi sijui mbovu mara matangazo na blah blah nyingi. Sasa kama yeye atatoa pesa nyingi Kwa matangazo yake hayo.,mnatakaje?

Kama unaona hizo nyingine ndio nzuri, kanunue hizo. Kila kukicha Simba, Simba. Simba that, Simba this, Simba there! Idiots!

Hamna familia za kulisha huko majumbani. Mnarefuka makende TU kila saa. Be men! Yaani mnageuka wambea ghafla. Sijui mnawezaje kuwa hivyo mlivyo!

Aghaghaaa!
 
Wala hakuna shida ni vile TU tumejawa na fikra duni na kudhani kila kitu lazima kifanane. Mara jezi sijui mbovu mara matangazo na blah blah nyingi...
Ameweka pesa zipi ambazo wengine hawawezi kuweka?
Baadae akipata pesa toka CAF anaanza kukalamika eti anapata hasara!
Simba ombeni hata DP world awadhamini muachane na uhuni wa huyu mwekezaji

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Wala hakuna shida ni vile TU tumejawa na fikra duni na kudhani kila kitu lazima kifanane. Mara jezi sijui mbovu mara matangazo na blah blah nyingi...
Hakuna shida Acha mahaba mkuu. Umewahi kuona jezi ina matangazo mawili yanayofanana tena ndani ya sehemu moja. Kama ni jambo la kawaida basi wangweka hata kwa nyuma chini ya kola sio mbele kaka. Fikiria nje ya box
 
Jezi kununua una ona aibu!

Bora watu mkanunue jezi ya Yanga ata kama ni mpinzani ila ana jezi kali, kila mwaka anatoa kitu kizito sana...!

Huku Simba hakupo shwari kabisa kuna tatizo kuanzia Jezi kuwa na mvito mpaka mpira wenyewe papatu papatu...

Jezi papatu
Pira papatu
Kilakitu papatu
 
Simba kuna shida. Tena kubwa tu. Sijawahi kuona timu ina matangazo mawili ya aina moja ndani ya jezi moja tena zote mbele.
Wamekosa wadhamini? CEO kazi yake nn sasa? Hii inapunguza mashabiki wenye akili ila wale wenye akili za kuvukia barabara wanaleta mahaba ila haikubaliki kabisa
Kazi ya CEO ni kufunga na kufungua mikutano
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom