Mchakato wa Serikali kupunguza gharama za matibabu ya afya

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu imekuja na mpango wa "BIMA YA AFYA KWA WOTE" dhamira ya serikali endapo sheria ya bima ya afya kwa wote itapitishwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya bila kikwazo.

Serikali imesema itaweka utaratibu wa kuchangia kwa kuzingatia kaya, na mtu mmoja mmoja asiye katika kaya. Bima ya Afya kwa wote itakuwa na kitita cha msingi na vifurushi mbalimbali vitakavyowezesha wananchi kuchagua kulingana na mahitaji.

Malipo ya bima yanaweza kuwekewa utaratibu wa kulipwa kwa awamu kulingana na uhitaji wa wateja na watoa huduma. Bima ya Afya kwa wote ni muhimu, ni bora kuchangia kidogo uwe na bima kuliko kusubiri ukiugua ukalipa fedha nyingi ili kupata matibabu.

Pia kwa wasio na uwezo Serikali itatumia utaratibu wa TASAF kuwatambua kwa ajili ya kuwapa huduma. Wananchi hawatalazimishwa kujiunga na mfuko mmoja, watakua wa na uhuru wa kuchagua skimu za bima zilizosajiliwa kwa mujibu wa sheria.

Malipo ya bima yanaweza kuwekewa utaratibu wa kulipwa kwa awamu kulingana na uhitaji wa wateja na watoa huduma. Bima ya Afya kwa wote ni muhimu, ni bora kuchangia kidogo uwe na bima kuliko kusubiri ukiugua ukalipa fedha nyingi ili kupata matibabu.

Vile vile serikali ya awamu ya sita imesema hakuna mtu atakayepigwa faini, atakayefungwa au kubughuziwa kwa namna yoyote ile kisa hatakua na bima ya afya, bima ya afya ni hiyari.

Lengo la serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu ni kuhakikisha inapunguza gharama za matibabu kwa wananchi na kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora za afya bila kikwazo cha pesa.
 
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu imekuja na mpango wa "BIMA YA AFYA KWA WOTE"

Lengo la serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu ni kuhakikisha inapunguza gharama za matibabu kwa wananchi na kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora za afya bila kikwazo cha pesa.
Ikitajwa serikali ya awamu ya sita si kila mtu anafahamu inaongozwa na nani au kuna mapinduzi yanaweza kutokea wakati wowote
 
Ikitajwa serikali ya awamu ya sita si kila mtu anafahamu inaongozwa na nani au kuna mapinduzi yanaweza kutokea wakati wowote
Najisikia vizuri kuandika jina la Rais wangu Samia Suluhu alieleta mapinduzi katika sekta ya afya.
 
Back
Top Bottom