Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 57,243
- 90,302
Vyeti vya shule havina ulazima,Muhimu uwe na documents za cheti cha kuzaliwa, cha form 4. Ujue majina na mwaka wa kuzaliwa wa wazazi wako(kama haujui unaweza ukakadilia tu hawafatilii), mzazi ambae amekufa kitahitaji cheti cha kifo(kama hauna andaa elfu 5 kama grisi ya kulegeza vyuma)
Baada ya hapo utaenda ofisi za uhamiaji watakuuliza maswali mawili matatu halafu kuna sehemu watakugongea muhuri.
Unaenda nida utapigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole vyako. Ukishakamikisha utaambiwa uende kuchukua namba baada ya wiki mbili. Foleni huwa inakuaga kubwa kwaiyo ni suala la kusitisha mishe zako zote ziku nzima
Kitambukisho chenyewe kukipata hakuna muda maalumu lakini inaweza kuchukua hata mwaka mzima. Kwaiyo kama una haraka nacho fuata ushauri wa kwenye comment namba 4.
Kuna watu wengi tu hawana cheti hata cha darasa la saba.