Mchakato wa kitambulisho Cha NIDA ukoje?

Mchakato wa kitambulisho Cha NIDA ukoje?

Godoro la kioo

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2025
Posts
364
Reaction score
727
Mwanzoni sikukitilia maanani kitambulisho Cha nida lakini baada ya kuona umuhimu wake nimeamua Leo nikakifuatilie

Nimeenda kwenye ofisi ya mtendaji nimepewa fomu zote mbili nimejaza

Mtendaji kaweka mihuri yake pale kanipatia fomu kaniambia nirudi jumatatu

Sasa naomba kuuliza kwenu wazoefu baada ya hapa Nini kinachofuata

Wasalam.
 
Kinachofata ni kuulizwa maswali mengi kama upo police na kupigwa picha kama jambazi pamoja na kukwanguliwa vidole vyako na nyembe hadi damu itoke kidogo ili wapate alama z

Kinachofata ni kuulizwa maswali mengi kama upo police na kupigwa picha kama jambazi pamoja na kukwanguliwa vidole vyako na nyembe hadi damu itoke kidogo ili wapate alama zako.
Mbona kama unataka kunitisha
 
Ko kumbe hivi hivi hamna mpaka chochote kitu
Ufatiliaji wa hiki kitambulisho inakuchukua mda saaana, kama una mishe zako inakuwa ngumu kidogo coz hakuna mda maalum wa kukipata,
wabongo wakaona wajiongeze kuweka dau ili kurahisisha mchakato
 
Kama unajua kutumia mtandao ingia website ya NIDA soma maelezo yote
Unaweza kusoma maelekezo ukafika ofisini ukakutana na mambo mapya, si unajua hizi ofisi za serikali kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake halafu hakuna ufatiliaji wala uwajibikaji
 
Sasa kama sijui alikozaliwa Babu inakuwaje
Ni lazima uwe na cheti chako cha kuzaliwa na mzazi mmojawapo hivyo ndivyo vitu vya muhimu zaidi, kama huna nenda kwa mwanasheria kachukue affidavits. Hivyo vingine sijui vya shule ni mbwembe tu, kama uliishia darasa la sita cheti cha darasa la saba utakipata wapi.
 
Muhimu uwe na documents za cheti cha kuzaliwa, cha form 4. Ujue majina na mwaka wa kuzaliwa wa wazazi wako(kama haujui unaweza ukakadilia tu hawafatilii), mzazi ambae amekufa kitahitaji cheti cha kifo(kama hauna andaa elfu 5 kama grisi ya kulegeza vyuma)

Baada ya hapo utaenda ofisi za uhamiaji watakuuliza maswali mawili matatu halafu kuna sehemu watakugongea muhuri.

Unaenda nida utapigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole vyako. Ukishakamikisha utaambiwa uende kuchukua namba baada ya wiki mbili. Foleni huwa inakuaga kubwa kwaiyo ni suala la kusitisha mishe zako zote ziku nzima

Kitambukisho chenyewe kukipata hakuna muda maalumu lakini inaweza kuchukua hata mwaka mzima. Kwaiyo kama una haraka nacho fuata ushauri wa kwenye comment namba 4.
 
Back
Top Bottom