Mchakato wa katiba; Judge Augustine Ramadhani na Prof. Kabudi

Mchakato wa katiba; Judge Augustine Ramadhani na Prof. Kabudi

Naombeni list nzima ya hiyo tume wadau.Nilikuwa kijijini na hakukuwa na network
 
Ofcourse upo sahihi mkuu, lakini kumbuka ile kamati ina wajumbe wengi ambao hawawezi kumezwa na vichwa viwili tu. Surely hukumu ile ilikuwa ya kisiasa zaidi na iliwapunguzia hadhi magwiji hawa katika taaluma ya sheria. Kumbuka marehemu Mwaikusa alikuwepo, zaidi ya hilo alibobea katika katiba na kesi ile ilikuwa ya kikatiba, unaweza kuona ni namna gani muhimili huu( mahakama ) ulivyoingiliwa na siasa. Ninadhani dawa pekee ni katiba mpya ambayo wajumbe watakaoratibu maoni wengi wao watatanguliza utaifa mbele kama tunavyowafahamu kwa uzalendo wao kwa taifa lao.
Ila nimeshangaa sana amemuacha gwiji aliyeanzisha hili vuguvugu katika midahalo profesa shivji na gwiji la habari Jenerali Ulimwengu, nimeshangaa sana kwa kuwa ndo vinara wa kwanza kabsa kulitafsiri hili suala kwa wanachi kuipitia mdahalo wa wazi pale UDSM.

Mkuu kama kweli wewe ni Mtanzania utajua wazi kabisa kuwa hakuna cha kutegemea kwenye katiba inayotarajiwa na watu. Sidhani kama kweli JK na ni halisi ya kuleta katiba mpya. Alisema aletewe majina halafu ateue hiyo pekee inaonesha kuwa kazi hiyo kwake haina uzito wowote. Kumuweka Palamagamba Kabudi kwenye tume hiyo kunaonesha wazi kabisa kuwa kuna tatizo. Kabudi ndio profesa pekee Tanzania anayesema kuwa CCM imeifikisha Tanzania pazuri, ni mtu pekee anayeona kuwa Tanzania iko safi kutokana na sera na uongozi wa CCM, what do you expect kuwa na mtu ambaye haoni kama nchi ina tatizo kwenye tume hiyo. Shivji kuwekwa pembeni si ajambo la kushangaza, kwa kuwa yeye ni representative wa wanyonge, na katiba hiyo haiwalengi hao.
 
SIKONGE,

Suala halikuwa sheria (an Act of Parliament), bali Katiba. Kwanza mwanzo Sheria ya uchaguzi ndiyo ilikuwa ikipinga independent candidate (IC) huku Katiba ikirusu. Mtikila akapinga hilo, yaani Sheria kumuzuia huku Katiba ibara 21 ikiruhu IC. Mahakama Kuu, THE LATE LUGAKINGIRA, akakubaliana na MTIKILA. MAGAMBA wakaenda Bungeni wakafanyia mabadiliko Katiba ibara za 39, 47 na 67 kuzuia IC. Hapo ndipo KAMANDA MTIKILA akafungua kesi nyingine kabisa akipinga mabadiliko hayo ya Katiba yanayopingana na ibara ya 21: kesi hii ndiyo iliyochakachuliwa na MAGAMBA KABUDI na RAMA

Mkuu NYAMKANG'ILI,

Naomba nikiri wazi mapema kabisa kwamba mimi ni JUMA KILAZA wa Sheria, kwa hiyo ninaweza kuuliza maswali ambayo ni irrelevant kwa mtu mwenye uelewa mkubwa wa sheria.

Nimesoma post ya Sikonge na post yako nikaona mna tofauti ndogo sana. Iwapo Majaji waliosikiliza kesi hiyo wangekubali kwamba mabadiliko ya vifungu ulivyovitaja yalikuwa yanakinzana na kifungu cha 21, je, Mahakama ina uwezo wa ku-nullify hayo mabadiliko? Baada ya ku-nullify, Mahakama ina uwezo wa kurekebisha hizo kasoro au kurudisha Bungeni ambako ndiko sheria hutungwa na pia mabadiliko ya katiba hufanyika?

Kasoro niliyoiona mimi ilikuwa ni kwamba Jaji Augustino Ramadhani na wenzake pamoja na Kabudi, walikataa kuliagiza Bunge wakidai kwamba Bunge ni mhimili ambao uko independent na hautakiwi kuingiliwa kwenye utendaji wake. Lakini kwa maoni yangu naona kwamba hiyo independence ya mihimili ya dola inatumika vibaya. Bunge linatunga sheria na kufanya mabadiliko ya Katiba, Mahakama inatoa interpretation ya hizo sheria, once Mahakama ikishaona kuna utata kwenye hizo sheria zilizotungwa na Bunge ndipo inatakiwa kuirejesha sheria hiyo Bungeni kwa kuliambia Bunge kwamba sheria hii au mabadiliko haya ya Katiba yana kasoro hizi na zile. Kama ni Bunge linalowajibika litafanyia kazi hizo kasoro na kurekebisha sheria au mabadiliko husika kama walivyoshauriwa na Mahakama.

Mfano mzuri ni mjadala unaoendelea huko kwa Obama kuhusu Healthcare Law, Baadhi ya majaji walihoji kwamba je wanaweza ku-nullify sheria nzima au wanaweza kuirudisha kwenye congress ili congress ifanyie kazi vipengele ambavyo vina utata.

Lakini hapa Tanzania, Jaji Mkuu alisema kwamba kuliagiza Bunge lifanye marekebisho ili yaendane na kifungu cha 21 na hivyo kuruhusu mgombea binafsi itakuwa ni kuingilia mhimili wa Bunge. Mahakama isipofanya hivyo, Bunge nalo litajifanya halijui kinachoendelea na serikali kwa kuwa haitaki mgombea binafsi itakaa kimya na mambo yatabaki kama yalivyo. So, the right way ilikuwa ni kuliandikia Bunge (sio kuliagiza) kwamba mabadiliko haya na haya yaliyofanyika wakati fulani yanakinzana na kifungu hiki na hivyo yanaingilia haki ya msingi ya kikatiba ya wananchi. Once Mahakama ikishaandika hivyo, then Bunge linalowajibika na kwa kuwa linajua wananchi wamesikia kila kitu, lingeiagiza serikali kwamba mabadiliko mliyoleta Mahakama imesema yana kasoro hizi na hizi, so zifanyieni kazi ili Bunge liweze kurekebisha hizo kasoro.

Lakini kwa kuwa Tanzania mihimili yote inaendeshwa kishikaji, then tunaishia kudanganyana kwamba Mahakama inaogopa kuandika kwa kuwa itakuwa inaingilia mhimili mwingine (Bunge). Usanii mtupu!
 
Tusubiri tuone japo na mimi nina mashaka na baadhi yao!. Sielewi ni nani kati ya wajumbe wote aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti wao lakini kama bado nashauri warioba!
Nashauri pia tume ihakikishe imezunguka mikoa yote angalau kwa kiwango cha kufikia watu kwa asilimia 75% kila mkoa. Vinginevyo kama itachakachuliwa tutaikataa katika mchana kweupe kabla hata ya kupita!
 
Namba muhimu pale ni Dr. Mvungi na Prof. Baregu. Wengine Kanyaga Twende!

Dr. Mvungi alishanionyesha hadi Rasimu ya katiba Mpya amabyo wameiandika inayoendana na matakwa ya leo. That was 2 years back.
 
Pamoja na ukweli kwamba Judge Augustino Ramadhani ameteuliwa kwa mapendekezo kutoka Zanzibar, bado inaonekana analipwa fadhira kwa utendaje wake ambao ulijionyesha wazi kuipendelea serikali katika maamuzi yake. Hivi sasa ana majukumu yafuatayo

  • Judge wa Afrika Mashariki
  • Judge anayemchunguzi judgee mwingine Kenya


Na hili la makamu mwenyekiti wa tume ya katiba litakuwa jukumu la tatu kubwa

swali ni kwamba yeye amewazidi ma-judge wengine (kama Judge Sammata) uwezo?

Jiulize ni kwa nini katika majaji wakuu Jaji Ramadhani ndiye jaji mkuu pekee ambaye baada tu ya kumaliza muda wake kesho yake alinyang'anywa ulinzi na gari alilokuwa anatumia na serikali?

Tujiulize tena Mahakama ya Rufaa inapokaa je kesi zake zinaamuliwa na majaji wangapi?? Ukishapata majibu ya maswali haya basi utajua nini msimamo wa Jaji mkuu mstaafu Augustino Ramadhani na uhusiano wake na serikali ya JK upo vipi?

Tusiwe washabiki ni ruksa ku-criticise objectively and not subjectively
 
Viongozi wetu hawana nia thabiti ya kuhakikisha kuwa katiba mpya itakayotupeleka miaka hamsini mbele inapatikana. ndio maana walitaka rais achague mwenyewe hiyo tume. Mbona haina mkulima hata mmoja? afya vipi? engineers? Hilo ni kama genge tu la wanasheria.
 
Usiwaongelee wabunge wa CCM, Masrahi binafsi kwanza, hawajui in a near future katiba ikibaki hivi vita, vita, vita! Hawasomi nyakati! Kizazi hiki ni cha tofuti, ukichakachua kitu kizazi hiki hawawezi kukubari!
 
Majina mpendekeze wenyewe halafu wakichaguliwa mnalaumu, kwanini mlipendekeza?
 
TUWAPE NAFASI,Nivizuri tunafahamu huko nyuma wamevurunda nini, hivyo ni bora umewawekea wazi ili nao wajielewe.
 
Wakuu mkiangalia trends za kesi nyingi mtagundua kwamba jaji Ramadhani anaonekana kuipendelea sana serikali na hukumu zake zina sura za kuwafurahisha wanasiasa walioko madarakani. Honestly namkubali sana Samata kuliko Ramadhani kiutendaji.
Hata vyeo anavyorundikiwa sasa ( Ramadhani ) ni kwamba huyu mheshimiwa anarudishiwa fadhila na serikali ambayo ameitetea alipokuwa mtumishi wa umma.
My take;
Dk Sengondo Mvungi, Prof. Baregu na wengine kuweni macho na watu kama Ramadhani mtakapokuwa mnatengeneza "Tanzania Mpya"

Kwa weledi wa sheria Tanzania retired chief Justice Barnabas Samatta is in a league of his own, huwezi kumfananisha na Augustno Ramadhani hata siku moja!! Akiwa jaji mkuu alikuwa na manguli wa sheria ambao hawakuchanganya siasa na taaluma yao nao ni jaji James Mwalusanya na Lugakingira mungu awalaze mahala pema pepono Amina!!
 
Mkuu kama kweli wewe ni Mtanzania utajua wazi kabisa kuwa hakuna cha kutegemea kwenye katiba inayotarajiwa na watu. Sidhani kama kweli JK na ni halisi ya kuleta katiba mpya. Alisema aletewe majina halafu ateue hiyo pekee inaonesha kuwa kazi hiyo kwake haina uzito wowote. Kumuweka Palamagamba Kabudi kwenye tume hiyo kunaonesha wazi kabisa kuwa kuna tatizo. Kabudi ndio profesa pekee Tanzania anayesema kuwa CCM imeifikisha Tanzania pazuri, ni mtu pekee anayeona kuwa Tanzania iko safi kutokana na sera na uongozi wa CCM, what do you expect kuwa na mtu ambaye haoni kama nchi ina tatizo kwenye tume hiyo. Shivji kuwekwa pembeni si ajambo la kushangaza, kwa kuwa yeye ni representative wa wanyonge, na katiba hiyo haiwalengi hao.

SOMA KWA UTULIVU BILA JAZIBA NA KWA FURAHA

RAIS JAKAYA Kikwete, ambaye jana alitangaza kuunda Tume ya kuratibu mchakato wa Katiba mpya Tanzania, amesema wajumbe wa Tume hiyo wataapishwa wakati wowote ili kuwawezesha kuanza safari ya miezi 18 ya kukusanya maoni ya wananchi na kukamilisha kuandikwa kwa Katiba hiyo, inayotarajiwa kutumika ifikapo mwaka 2014.

Rais alisema Tume hiyo baada ya kukamilisha kazi yake ya kukusanya maoni ya wananchi Tanzania na kutengeneza rasimu ya Katiba, zitakuwa zimebaki hatua mbili muhimu ambazo ni kuundwa kwa Bunge maalumu la Katiba na wananchi kupata fursa ya kupiga kura ya maoni.


"Baada ya hatua hiyo kukamilika, rasimu itawasilishwa katika Bunge hilo ambalo litaundwa kwa ajili ya kujadili na kuchambua mambo yanayofaa kuwemo katika rasimu hiyo. Bunge hili litakuwa kwa ajili hiyo tu na likishakamilisha kazi yake muda wake utakuwa umeisha," alisema Kikwete.


Alisema baada ya mambo ya msingi kupitishwa na Bunge hilo, mchakato huo utarejeshwa kwa wananchi ambao watapiga kura ya maoni kama wataona yaliyopitishwa yanafaa au laa.


Rais ametangaza kuunda Tume hiyo kufuatia marekebisho katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mkutano wa Sita wa Bunge la 10, marekebisho ambayo yalizua manung'uniko kutoka kwa wabunge wa CCM.
 
We MOhd, unaju suala la katiba inatakiwa lisiwe la kichama, hapo tutakuwa hamnazo, ni mamba ya msingi kabisa sasa inatakiwa interest za mtu binafsi zisiwepo kabisa nina wasiwasi na hao mabwana!

Mabwana gani waislam au? Na nini hasa unakiogopa? Unadhani wanaweza kuweka sheria za kiislam na kulazimisha wakristo wavae kanzu na kufunga mwezi wa ramadhani?funguka mkuu!
 
Mabwana gani waislam au? Na nini hasa unakiogopa? Unadhani wanaweza kuweka sheria za kiislam na kulazimisha wakristo wavae kanzu na kufunga mwezi wa ramadhani?funguka mkuu!
What is wrong with you?
Shivji kuwekwa pembeni si ajambo la kushangaza, kwa kuwa yeye ni representative wa wanyonge, na katiba hiyo haiwalengi hao.
Sisi tunataka mwenyekiti awe Prof Issa Shivji.
 
SOMA KWA UTULIVU BILA JAZIBA NA KWA FURAHA

RAIS JAKAYA Kikwete, ambaye jana alitangaza kuunda Tume ya kuratibu mchakato wa Katiba mpya Tanzania, amesema wajumbe wa Tume hiyo wataapishwa wakati wowote ili kuwawezesha kuanza safari ya miezi 18 ya kukusanya maoni ya wananchi na kukamilisha kuandikwa kwa Katiba hiyo, inayotarajiwa kutumika ifikapo mwaka 2014.

Rais alisema Tume hiyo baada ya kukamilisha kazi yake ya kukusanya maoni ya wananchi Tanzania na kutengeneza rasimu ya Katiba, zitakuwa zimebaki hatua mbili muhimu ambazo ni kuundwa kwa Bunge maalumu la Katiba na wananchi kupata fursa ya kupiga kura ya maoni.


“Baada ya hatua hiyo kukamilika, rasimu itawasilishwa katika Bunge hilo ambalo litaundwa kwa ajili ya kujadili na kuchambua mambo yanayofaa kuwemo katika rasimu hiyo. Bunge hili litakuwa kwa ajili hiyo tu na likishakamilisha kazi yake muda wake utakuwa umeisha,” alisema Kikwete.


Alisema baada ya mambo ya msingi kupitishwa na Bunge hilo, mchakato huo utarejeshwa kwa wananchi ambao watapiga kura ya maoni kama wataona yaliyopitishwa yanafaa au laa.


Rais ametangaza kuunda Tume hiyo kufuatia marekebisho katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mkutano wa Sita wa Bunge la 10, marekebisho ambayo yalizua manung’uniko kutoka kwa wabunge wa CCM.

Mkuu kuna wakati tunatakiwa kuwa realistic. Haya anayosema Kikwete leo ni yale yale tuliyojadili toka mwaka 2000, tayari yapo kwenye documents na yanajulikana, yeye hakuwa na interest nayo kwa kuwa at that time alikuwa waziri wa mambo ya nje. Wanazuoni wa mambo ya katiba walisema kaubsa kuwa tunahitaji whitepaper, blue paper and bunge la katiba etc....lakini je muundo wake utakuwaje? pamoja na kuwa JK anaonesha utayari wa kufuata utaratibu sahihi ukiangalia composition hiyo ya hatua ya kwanza unakuwa na mashaka. Unaweza kuna na barabara nzuri kama gari ni bovu, safari itakuwa mbaya, unaweza usiwe na barabara kabisa kama gari ni zuri pia huwezi kufika popote. JK anajiweka kwenye mazingira ya machaguo hayo.

Tuna njia nzuri, tunatakiwa tuwe na magari mazuri ili twende.

Unaamini kweli watanzania wanaweza kupigia kura mswada wa katiba? Katiba ya sasa ni watanzania wangapi wanaijua? kuna wabunge ambao hata hawajui katiba yetu, what about mzee kijiini, what about mama ntilie, watu about dereva wa daladala ambaye hata shule mgogoro? are we being realistic here? or just doing it?
 
Hivi jamani hamkupewa muda wa karibia mwezi mzima mpeleke mapendekezo ya watu mnaowaona wanafaa ili wajumuishwe kwenye tume?Je!Mliwapendekeza hao mnaowataka then Rais kawapiga chini?mnauhakika gani kuwa hao mliowapendekeza juu ya utayari wao wa kuwepo kwenye tume?Jamani tuache tume ifanyekazi na tuikosoe pale itakapokosea kuliko kuendekeza majungu!!
 
Back
Top Bottom