Mchakato wa katiba; Judge Augustine Ramadhani na Prof. Kabudi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchakato wa katiba; Judge Augustine Ramadhani na Prof. Kabudi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasimba G, Apr 10, 2012.

 1. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,568
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Wajumbe hawa wawili ambao Rais amewaingiza katika tume ya kukusanya maoni, wana mushkeri. Judge Ramadhani anatuhumiwa kuhujumu kesi ya mgombea binafsi hivyo kuhujumu demokrasia na kuipa serikari ushindi wa kesi ambayo ilikuwa obvious kwa kuwa mgombea binafsi ni haki ya kimsingi ya kikatiba kwa katiba yetu hii kuukuu!

  Prof Kabudi, pamoja na comments zake nyingi tata, anaonyesha pamoja na kuwa ni prof wa sheria hana msimamo, mfano pia ni kesi hiyohiyo ya mgombea binafsi, akiwa rafiki wa mahakama, alipendekeza pendekezo ambalo kwa mtu wa weredi wake, watu wasingetegemea hata kidogo, yaani alikuwa anapinga uwepo wa mgombea binafsi! Kwa kweli hawa wawili ni janga na tuwaangalie vizuri!

  Kwakweli hawa wawili, na wengine ambao sijatoa wasifu wao kazi yao ni kukusanya maoni, lakini, ninakuwa na wasiwasi na kama ni kweli watakusanya maoni badala ya kishinikiza interest zao, anyway tunawajua wanasimamia msimamo gani, jamani tuweni macho na maoni yetu yasije nayo yakachakachuliwa.
   
 2. E

  ESAM JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hao jamaa awakufaa kuwemo kabisa, lakini tuwape muda tuone kwani hata wakichakakchua na kutunga katiba kimagambamagamba, bado wazalendo tutaendeleea kudai katiba ya wananchi
   
 3. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Wamependekezwa na mh. rais akawateua!
  walaumu waliowapendekeza! Jaji ramadhani ni mteule toka ZNZ.
   
 4. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Chadema wana msemo huwa wanasema mwakilishi mmoja kutoka CDM ni sawa na wawakilishi 50 kutoka vyama vingine. Kwakuwa kuna mtu mmoja wa CDM ukiwatoa hao wawili ambao hujapendezewa nao watabaki watu 98.
   
 5. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,568
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  We MOhd, unaju suala la katiba inatakiwa lisiwe la kichama, hapo tutakuwa hamnazo, ni mamba ya msingi kabisa sasa inatakiwa interest za mtu binafsi zisiwepo kabisa nina wasiwasi na hao mabwana!
   
 6. a

  akelu kungisi Senior Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ofcourse upo sahihi mkuu, lakini kumbuka ile kamati ina wajumbe wengi ambao hawawezi kumezwa na vichwa viwili tu. Surely hukumu ile ilikuwa ya kisiasa zaidi na iliwapunguzia hadhi magwiji hawa katika taaluma ya sheria. Kumbuka marehemu Mwaikusa alikuwepo, zaidi ya hilo alibobea katika katiba na kesi ile ilikuwa ya kikatiba, unaweza kuona ni namna gani muhimili huu( mahakama ) ulivyoingiliwa na siasa. Ninadhani dawa pekee ni katiba mpya ambayo wajumbe watakaoratibu maoni wengi wao watatanguliza utaifa mbele kama tunavyowafahamu kwa uzalendo wao kwa taifa lao.
  Ila nimeshangaa sana amemuacha gwiji aliyeanzisha hili vuguvugu katika midahalo profesa shivji na gwiji la habari Jenerali Ulimwengu, nimeshangaa sana kwa kuwa ndo vinara wa kwanza kabsa kulitafsiri hili suala kwa wanachi kuipitia mdahalo wa wazi pale UDSM.
   
 7. iron2012

  iron2012 JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 358
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  tukianza kuchunguza kwa tanzania hakuna atakayefaaa
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Nafikiri Prof. Kabudi wengi hatukumuelewa wakati ule. Mahakama kama Mhimili mmoja wapo unaojitegemea, hauwezi KULILAZIMISHA BUNGE lipitishe sheria. Mahakama inaweza tu kusema kuwa "hii sheria inavunja haki za binadamu" ila ni Bunge inabidi libadili hiyo sheria haraka.

  Sasa jiulize, baadamu wao walisema hivyo, Bunge letu hadi leo nimeibadili hiyo sheria? Wengi tulijadili hiyo habari kwa munkari sana na kumuona Prof wa Kigogo hafai. Ukishajua mgawanyiko wa hii mihimili, ndiyo utamuelewa Kabudi.
   
 9. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Chadema imeingiaje hapa? au ni addiction
   
 10. Epason

  Epason JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 427
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  ukitaka kumla kuku usimchunguze sana
   
 11. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hawa jamaa ni janga, believe me.
   
 12. M

  Makyomwango JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
   
 13. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #13
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Hao walioachwa watatusaidia kukosoa pale mambo yatapokwenda ndivyo sivyo
   
 14. M

  Makyomwango JF-Expert Member

  #14
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
   
 15. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #15
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  SIKONGE,

  Suala halikuwa sheria (an Act of Parliament), bali Katiba. Kwanza mwanzo Sheria ya uchaguzi ndiyo ilikuwa ikipinga independent candidate (IC) huku Katiba ikirusu. Mtikila akapinga hilo, yaani Sheria kumuzuia huku Katiba ibara 21 ikiruhu IC. Mahakama Kuu, THE LATE LUGAKINGIRA, akakubaliana na MTIKILA. MAGAMBA wakaenda Bungeni wakafanyia mabadiliko Katiba ibara za 39, 47 na 67 kuzuia IC. Hapo ndipo KAMANDA MTIKILA akafungua kesi nyingine kabisa akipinga mabadiliko hayo ya Katiba yanayopingana na ibara ya 21: kesi hii ndiyo iliyochakachuliwa na MAGAMBA KABUDI na RAMA

   
 16. a

  akelu kungisi Senior Member

  #16
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu mkiangalia trends za kesi nyingi mtagundua kwamba jaji Ramadhani anaonekana kuipendelea sana serikali na hukumu zake zina sura za kuwafurahisha wanasiasa walioko madarakani. Honestly namkubali sana Samata kuliko Ramadhani kiutendaji.
  Hata vyeo anavyorundikiwa sasa ( Ramadhani ) ni kwamba huyu mheshimiwa anarudishiwa fadhila na serikali ambayo ameitetea alipokuwa mtumishi wa umma.
  My take;
  Dk Sengondo Mvungi, Prof. Baregu na wengine kuweni macho na watu kama Ramadhani mtakapokuwa mnatengeneza "Tanzania Mpya"
   
 17. w

  warea JF-Expert Member

  #17
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama hawafai kwa nini tusubiri watuletee mchakachuo?
  TUSITEGEMEE KUVUNA ZABIBU KWENYE MICHONGOMA!
   
 18. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #18
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hivi chadema inaingiaje hapa?? unataka nishindwe kukutofautisha na watu wanaojadiri dini za hawa wateule. Mimi nadhani tungeendelea kumchambua mtu mmoja mmoja kama jamaa alichofanya na kama kuna kitu kachemka nadhani ni fursa nzuri sana kumrekebisha. Kuliko kuzungumzia vyama vyao au dini zao. Natafakari tuu
   
 19. A

  Adili JF-Expert Member

  #19
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 1,996
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180


  Basi tusibiri mpaka akipatikana anayefaa.
   
 20. l

  lubaga Member

  #20
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanzania wenzangu wazalendo wana wa afrika mimi mtanzania halisi mwanawaafrika ,nashauri kuwa katika mchakato huo wanahabari na vyombo vya habari vipewe jukumu la kurekodi kila kitu anachochangia mtanzania popote alipo awe kisumba huko kalambo sumbawanga awe kifunda huko lufilyo rungwe mashariki awe paradiso huko mbinga ruvuma awe kilindi tanga ,manyoni singida yaani popote pale sasa picha hizo zipewe kipindi maalumu kirushwe kwenye tv zote bila upendeleo kwa kisingizio kuwa ipo tbc hapana tunataka tv zote zishiriki walipwe muda wa hewani ,radio zote kwenye mitandao ili wananchi wasikie waone kilichonenwa na watu wa bukombe ,watu wa mitumba huko gombe kigoma na kuingineko ,ili siku ya siku hawa wakina ramadhani tuwashitaki wasipotekeleza majukumu sawa na maoni ya wananchi.
   
Loading...